Wanaposemaga simu inauzwa kwa sh. 199,999 mnaelewaje?

Babumawe

JF-Expert Member
Sep 12, 2014
2,556
2,560
Ukitembelea maduka ya simu utakuta simu fulani inauzwa kwa sh. 199999 nyingine labda 149999 au 249999.

Swali linalolitatiza mimi ni kwamba hizi hela zipo kweli au yaani ukishanunua hiyo shilingi moja unaipata wapi.

Au kwa waliowahi kununua je huwaga wanawarudishia chenji iyo shilingi moja au inakuwaje kwenye hii kitu.

Wenye uzoefu mtujuze.
 
Hoo
Ukitembelea maduka ya simu utakuta simu Fulani inauzwa kwa sh. 199999 nyingine labda 149999 au 249999...
Hii ni lugha ya kibiashara kwaajili ya kumvutia mteja as wateja wengi wanapenda vitu vizuri kwa Bei rahisi. So 199,999 ni sawa na 200,000 mkuu.

Kama utataka uilipe hiyo amount sahihi basi fanya manunuzi electronically.
 
Ukitembelea maduka ya simu utakuta simu Fulani inauzwa kwa sh. 199999 nyingine labda 149999 au 249999,

swali linalolitatiza mimi ni kwamba hizi hela zipo kweli au yaani ukishanunua hiyo shilingi moja unaipata wapi

au kwa waliowahi kununua je huwaga wanawarudishia chenji iyo shilingi moja au inakuwaje kwenye hii kitu
Wenye uzoefu mtujuze
Acha ubahili
 
Hichi kitu nimewahi kukitumia kwenye kutoa pesa kwa mawakala wa simu(M-Pesa, Tigo-Pesa).

Hata viwango vya miamala vimewekwa katika range kama hiyo ya kuanzia kiasi fulani hadi kiasi fulani cha matisa tisa.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Hoo

Hii ni lugha ya kibiashara kwaajili ya kumvutia mteja as wateja wengi wanapenda vitu vizuri kwa Bei rahisi. So 199,999 ni sawa na 200,000 mkuu.
Kama utataka uilipe hiyo amount sahihi basi fanya manunuzi electronically.
Si bado utakatwa hela kwenye kulipia tena itazidi hata hiyo amount waliyoweka. Kikubwa wewe mteja unawapa 200,000 then hakikisha unadai chenji yako ya shilingi moja.Ni haki yako kama hawana hiyo shilingi moja kwanini waandike bei hiyo?
 
Mm huwa nina round off.

Hichi ni kitu cha mda mrefu sana. Tafiti zinaonesha kuwa kwasababu tunasoma kuanzia kushoto kwenda kulia tunaona kwanza 240,.... kwahyo akili zetu zinakua na illusion kuwa hichi kitu ni bei ndogo. No technique ya mda mrefu sana. Kma ukiona 999,999 utaona ni bei rahisi kuliko 1,000,000 kwasababu ya ubongo wako unavyosoma hizo namba.

Ila hyo hela huwezi ipata hasa ukilipia kwa cash. Ukilipia kwa electronic money pia huwezi ipata sababu kuna makato ya transactions. Kwahyo wewe round off tu hyo bei. No technique ya kuvutia watu tu

Unaweza soma zaidi hapa: Why Do Most Prices End in .99? | Live Science
 
Si bado utakatwa hela kwenye kulipia tena itazidi hata hiyo amount waliyoweka. Kikubwa wewe mteja unawapa 200,000 then hakikisha unadai chenji yako ya shilingi moja.Ni haki yako kama hawana hiyo shilingi moja kwanini waandike bei hiyo?
Tudai chenji au vipi? 😆👍
 
Ukitembelea maduka ya simu utakuta simu Fulani inauzwa kwa sh. 199999 nyingine labda 149999 au 249999,

swali linalolitatiza mimi ni kwamba hizi hela zipo kweli au yaani ukishanunua hiyo shilingi moja unaipata wapi

au kwa waliowahi kununua je huwaga wanawarudishia chenji iyo shilingi moja au inakuwaje kwenye hii kitu
Wenye uzoefu mtujuze
Ni sehemu ya upuuzi tu wa wanadamu
 
Back
Top Bottom