Wanaposemaga simu inauzwa kwa sh. 199,999 mnaelewaje?

majibu ushayapata, hapo wanacheza na saikolojia za wanunuzi ili waone kama bei ni ndogo. Ni sawa tu na baadhi ya maduka au kampuni zinazopunguza asilimia 50 ya bei za vitu msimu wa sikukuu lakini kiuhalisia huwa wanapandisha bei halisi ili punguzo unalopata liwe chini ya hizo asilimia. Ila ukinunua si unakuwa umefurahi na kufarijika 😊
 
Ni psychological sales trick....Yani wanataka subconcious part ya ubongo wako iamini kua the price was reduced to the maximum..na ndo Mana Bei ikiwa hivo hakuna anaeomba punguzo...lakini pia hawezi kutoa hiyo hela...itamlazimu atoe laki 2....at wewe bidhaa zako weka 15000 watu wataomba punguzo...lakini weka 17350 hapa nakuhakikishia hawataomba punguzo😁😁😁....
 
Na hizo shillingi moja moja si zinajaaga kwao na kuwa faida?

Je hiyo Shilling 1 inakuwa Taxed?
 
Point ya msingi hapo itakua ni kodi tu, ukitaka msaada zaidi juu ya hili pitia mfano wa viwango vya makato vya huduma za kipesa za simu kama tigo pesa, mpesa e.t.c.

Hiyo shilingi moja ukiiongeza tu digits zote zinachange. Let say kipindi cha nyuma kdg tigo pesa ilikua kutoa pesa 5000-9999 makato ni 800 ila 10000-19999 makato ni 1300...so unaona ni jinsi gani shilingi moja inaweza kukuumiza kwa tofauti ya shilingi 500.

Yan ni kwamba ukiwa na 10800 ktk simu njia pekee ya kupata elfu kumi kamili ni kutoa 9999 vinginevyo mpaka uongeze shilingi mia tano.
 
Kuna na hawa wa cc za magari. Utakuta 14.., 18..., 24...; Kwanini wasiweke kitu kamili? 1500; 2000, 2500, 3000 nk?
 
  • Mshangao
Reactions: _ID
Ukitembelea maduka ya simu utakuta simu fulani inauzwa kwa sh. 199999 nyingine labda 149999 au 249999.

Swali linalolitatiza mimi ni kwamba hizi hela zipo kweli au yaani ukishanunua hiyo shilingi moja unaipata wapi.

Au kwa waliowahi kununua je huwaga wanawarudishia chenji iyo shilingi moja au inakuwaje kwenye hii kitu.

Wenye uzoefu mtujuze.
Hio kibiashara inaitwa Psychology pricing
 
Kijana muda mwingi huwa unapost pumba inaonekana huna shughuli ya kufanya nipe namba zako nikupe mshongo nipo serious mkuu natak nikusaidie
 
Biashara ni taaluma,kwa watu wa business watanielewa,hio unasoma hasa kwenye topic wanaita pricing,hio kitu inaitwa pyschological pricing,ni namna ya upangaji bei unaokwepa kutamka namba fulani ili mteja asihisi bei kubwa,

Ukiandindika 99999 ni bora zaidi kuliko kutamka laki moja.

Mfano kampuni kama tigo wakitoa zawadi ya mifuko 40 ya cement wanasema tumetoa zawadi ya cement tani moja badala ya kusema mifuko arobaini ili watu wahisi wametoa mifuko mingi.

Hivyo hayo ni mambo yakitaaluma kwenye biashara,
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Point ya msingi hapo itakua ni kodi tu, ukitaka msaada zaidi juu ya hili pitia mfano wa viwango vya makato vya huduma za kipesa za simu kama tigo pesa, mpesa e.t.c.

Hiyo shilingi moja ukiiongeza tu digits zote zinachange. Let say kipindi cha nyuma kdg tigo pesa ilikua kutoa pesa 5000-9999 makato ni 800 ila 10000-19999 makato ni 1300...so unaona ni jinsi gani shilingi moja inaweza kukuumiza kwa tofauti ya shilingi 500.

Yan ni kwamba ukiwa na 10800 ktk simu njia pekee ya kupata elfu kumi kamili ni kutoa 9999 vinginevyo mpaka uongeze shilingi mia tano.
hii technique nimeipenda asee nkienda kwa wakala ntaitumia
 
Back
Top Bottom