Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.

======
Kuna uchungu na chuki kubwa kati ya Polisi na Raia, namna ya kutatua chuki hizi ni kurekebisha fikra zenu na matendo yenu kwa Raia.

Ni jambo la kusikitisha sana ila pia maoni mbali mbali kinyume chenu yachukuliwe kama changamoto ya kurekebisha pale palipo na kasoro.

Ni muhimu mkajua wote sisi tunategemea ulinzi wa polisi, ni mtu mjinga tu ambaye ataogopa akiona polisi ameuwawa na kuporwa bunduki.

Mungu awatie nguvu wakati huu mgumu.

Waziri Kivuli Mambo ya Ndani.
 
wanashindwa kutazama walipojikwaa wanatazama walipoangukia, imekuwaje chuki kwa sasa tu? kwanini isiwe toka enzi?
jitathmini upya tatizo liko wapi?
na hakuna sehemu mabavu yametumika yakafaulu hata sehemu moja,
 
Wajiulize wamekosea wapi... Hakuna anyependa police wetu apigwe na kuuawa. Inapotekea amepigwa alafu watu wakashabikia aliye piga police waje na majibu wamewakosea nini watanzania.
Umeweka kisu kwenye mfupa. Ni vyema kujirekebisha na sio kutumia vitisho. Ukweli uko wazi kwamba wanatumika vibaya dhidi ya upande wa pili. Wanaweza kufanya wapendalo lakini ukweli uko wazi kwamba wanaowatuma wanawatumia ndivyo sivyo.
 
Jeshi la Polisi linapaswa lijiweke mbali kabisa na haya matamko. Kaeni kimya kabisa mfanye kazi zenu kwa utulivu. Natambua mnatimiza majukumu yenu katika mazingira magumu sana, lakini hiyo isiwafanye mchanganyikiwe maana uwepo na huduma yenu tunaihitaji sana.
Achaneni na hayo matamko yenu na msimame imara. Mkiruhusu kuchanganyikiwa hivi sasa sidhani kama tutafika. Jiulizeni mlipokosea ili muweze kusimama.
 
Polisi wetu wanafanya kazi nzuri sana. Nawashangaa sana wale wanaolibeza
 
Kumshitaki Mtu Ni Rahisi Sana Kazi Ipo Kwenye Kushinda Kesi, Polisi Wajitafakari Kwanza Kabla Hawajawashitaki Watu. Wasije Wakashindwa Kesi Wakalitia Taifa Hasara.
Polisi siku zote wapo sahihi. Nyie mnaowabeza mna ajenda zenu za siri
 
Polisi siku zote wapo sahihi. Nyie mnaowabeza mna ajenda zenu za siri

Wewe ndio unawapotosha baada ya kuona kile mlichokuwa mkijisifia juzi leo chuki za watu ziko dhahiri. Mjifunze wale mnaowatishia kwa silaha leo wamejibu mashambulizi kwa kuonyesha chuki zao kwa maneno tu imewauma ile mbaya. Na msipoangalia huko tuendako watu wataacha hata kuzikana. Jirekebisheni acheni jeshi la polisi litekeleze sheria na sio matakwa ya chama ama kiongozi fulani. Hebu tuambie juzi polisi kwenye mkutano wa cuf walitoa ulinzi stahiki? Mbona kwenye mkutano wa ccm walilinda mpaka mwisho. Haki huinua taifa na sio upendeleo. Hili ni fundisho na msidhani bundiki itazuia hisia za watu, upendo hujengwa na wala haulazimishwi.
 
Katika taifa ambalo polisi wanasifika kwa mauaji, majeruhi, mateso, na kubambika watu kesi, wasitegemee raia wawapende.! Hicho kitisho hakitasaidia polisi kupendwa na raia. Watu lazima wawambie wawajibike kwenye usalama na si kujiandaa na mazoezi barabarani kwa lengo la kujiandaa kuua ama kujeruhi raia wasio na hatia.
 
Hehehe, ukiongea chochote tu unapigwa mkwara, kuna sheria gani inazuia mtu asitoe maoni ya event kama ile?
Yaani sa hivi tushaipita China na Zimbabwe kwenye kubana mambo, tunafukuzana na north korea tu, tusijefika hatua tukalingana nao, tuwe makini sana.
 
Kuna uchungu na chuki kubwa kati ya Polisi na Raia, namna ya kutatua chuki hizi ni kurekebisha fikra zenu na matendo yenu kwa Raia.

Ni jambo la kusikitisha sana ila pia maoni mbali mbali kinyume chenu yachukuliwe kama changamoto ya kurekebisha pale palipo na kasoro.

Ni muhimu mkajua wote sisi tunategemea ulinzi wa polisi,

Mungu awatie nguvu wakati huu mgumu.

Waziri Kivuli Mambo ya Ndani.
 
Back
Top Bottom