Wanaovunja moyo Harakati za ukombozi!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaovunja moyo Harakati za ukombozi!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RedDevil, Aug 8, 2010.

 1. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Ndugu wanaJF wenzangu, kwa mara ya kwanza nimeamua kusema yanayonikera humu ndani kwani kuna watu humu wamekuwa mbele saaana kuvunja harakati za mapambano dhidi ya ukombozi wa nchi yetu.

  Sote tunapenda kuona watanzania wote tuishi kwa amani an upendo bila kuishi kama watumwa. Leo hii watanzania wengi wanaishi kama watumwa kwenye nchi yao, wanapata hata huo mlo mmoja kwa shida, wanauza utu wao kwa waombea lakini moja, elfu kumi kumi ndo usiseme hiki ni kielelezo tosha kuwa watu wanaishi kama watumwa ndani ya nchi yao. Matumaini yamepotea, hawana uhakika wa ,maisha ya baadaye.
  Kutokana na hayo mambo, ndio maana watanzania wengi wenye uelewa wanajaribu kushiriki kwa namna yeyote kuleta mabadiriko ili mradi sote tuweze kuishi kama ndugu na tufurahie maisha ndani ya nchi yetu tanzania.
  lakini humu ndani kuna kikundi cha watu wachache sana ambao sielewi ni vipi basi tunakuwa hatuna huruma kwa hawa watu ambao ni karibu 80% wanaishi kwa kubahatisha.
  Mimi nasema leo hii kuwa!!wanaokatisha tamaa; huenda wao ni Mafisadi DAMU lakini waangalie mamilioni ya watanzania wanaoishi ka watumwa kwenye nchi yao, huu ni muda wa mabadiliko na c muda wa kudhihaki wanamapinduzi, in short waache (kaeni kimya) kuvunja moyo harakati za ukombozi b'se you can ban an organization, you can liquidate people but revolutionary never die "
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Naona thread yako imekaa idol bila jibu lolote kwa hiyo ngoja nitupe jiwe kwenye maji kidogo. Mkuu kwanza hauja bainisha kundi la wana mapinduzi ni lipi na kundi lisilo la wana mapinduzi ni lipi. I'm assuming (I could be wrong) kwamba una maanisha wana mapinduzi ni wanao msupport Slaa na mafisadi ni mtu yoyote asiye kubaliana na Slaa. Am I right? Mjadala utaendelea kadri ya jibu lako.
   
 3. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ndugu Mwanafalsafa,naamini unajua bayana tofauti kati ya mafisadi na wanaharakati wa ukombozi dhidi ya mafisadi.I strongly believe that kila Mtanzania anafahamu hilo.Red Devil,uko sahihi kabisa ktk observation yako.So far,kumekuwa na wimbi kubwa la members wapya ws JF kadri uchaguzi unavyozidi kujongea.And they all seem to share a similar goal:kukejeli jitihada za " uhuru wa pili wa Tanzania".Ni dhahiri kuwa UWT imemwaga watu wake hapa ili waendeleze jitihada zao za kulinda mafisadi.Ushauri wangu ni kuwapuuza watu wa aina hiyo.Kujaribu kuwaelimisha ni sawa na kuwapa attention wasiyostahili.Let's not forget, it's same people waliojaribu kuiua JF huko nyuma.Waliposhindwa wameamua ku- compromise lakini with same devilish agenda.Once wakibaini wanapuuzwa they could disappear all together.As JK said,hii ni vita,na wanajaribu kuisambaza ktk kila front including mtandaoni.Wanafahamu bayana kuwa wakiivuruga JF watakuwa wamefanikiwa sana kubana front hii ya mtandao hasa kwa vile most of our papers and blogs seem to be either supporting CCM na mafisadi or too scared to mention anything kitachowaudhi watawala.Can you imagine blog ya Michuzi imeweza kuweka picha za fiesta lakini ikachunia picha za mkutano wa Chadema Jangwani hapo Jumamosi?
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Waache waje tu wala tusiwaogope. Tutapambana nao hoja kwa hoja. When the going gets tough the tough get going.
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mlalahoi naelewa sana alicho sema. Ila hii thread ilikua ipo domant tokea ianzishwe na nia yangu ilikua watu waione. Mbona muda wote watu wali ignore mpaka nilipo amua kupost? So it worked didn't it? Kwa hiyo mkuu wala usijali hiyo ilikua icebreaker because trust me nisinge andika kitu kama hicho hamna ambae angekuja kujibu.

  Kuhusu usemacho mkuu nime kubaliana na wewe mkuu ila kuna mtindo unao ibuka JF haswa wakati huu wa uchaguzi wa kugeneraliza term za "mkombozi" na "fisadi". Simply put sasa hivi watu wapo kwenye makambi ambapo kila mtu anaona kambi yake ni ya wakombozi na everyone else ambae hakubaliani nao 100% yupo side ya mafisadii. Ndiyo maana nika muuliza kama maana ya mkombozi na fisadi kwake ni nini ili tuwe same page tujibiane vizuri maana kuna watu wanao amini kwamba watu kama Mwakyembe CCM ni mpiganaji na kuna wanao amini kwamba anybody who is pro CCM siyo mpiganaji so ni lazima kuweka terms clear.

  Kuhusu kujaa kwa members wapya mkuu that is expected. Sawa some people wata kuwa mamluki (maybe, kuna njia ya kuprove) lakini wengine ni msisimko unao tokana na kusekwa na wimbi la hisia kwa wakati huu. Hiyo ndiyo demokrasia kwamba yoyote ana weza kujiunga kuchangia. Pia demokrasia ni mtu kuchagua chama anacho kipenda mwenyewe au mgombea anaye mpenda mwenyewe. Sasa kudemonize watu moja kwa moja kwamba if you do not agree with me basi wewe ni mtetea mafisadi naamini huko ni kukandamiza demokrasia. Wazalendo wapo wengi na wana mawazo tofauti ya jinsi ya kuikwamua Tanzania. Wapo wanao amini ukombozi ni CUF, wapo wanao amini ukombozi ni CCM na wapo wanao amini ukombozi ni CHadema na kuna ambao wana amini kwamba bado mkombozi haja tokea. Kinacho tenganisha watu ni kundi lipi lina idadi kubwa zaidi.

  So anyway mkuu I got the ball started and I guarantee you now I have helped the thread starter more then you think because ina wezekana hii thread isinge jibiwa na mtu as evident ya muda iliyo kaa bila kujibiwa mpaka ikashuka chini ya list. Now the ball is rolling kazi ya wana mapinduzi sasa.
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Oh yeah very true mkuu I agree with you. Lakini saa nyingine si nguvu ya hoja inayo shinda bali nguvu za watu. Unadhani mtu mmoja ukiwa kwenye kundi la watu mia wanao kupinga no matter what hata utoe hoja gani utashinda? Maybe ndiyo maana watu wapya wanajaa ili kuequalize numbers na ndiyo utamu uta kapo kuja hapo maana hoja zita shindana kwa hoja na si "Him/her against us".
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ninaposimamia hoja.....mwanafalsafa1 umetoa hoja yenye nguvu.....terms should be made clear...mpambanaji ni yupi na asiye mpambanaji ni yupi.......AU AANGALIAYE KWA JICHO MOJA KAMA KUKU AMBAYE AKIONACHO YEYE NDICHO HICHO TU NA SI ANACHOONA MWINGINE......!
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  RedDevil

  Ndugu yangu RD vita vya ukombozi vinahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana vinginevyo huwa ni ngumu sana kuufikia ukombozi. Afrika Kusini wakati wa mapambano ya kuuondoa ubaguzi still kulikuwa na waafrika wenzao (vibaraka) waliokuwa wanabeza, kukejeli harakati za kujikomboa. Si kwamba walikuwa hawajui ubovu wa ubaguzi lakini kutokana na roho isiyo ya kizalendo(hata kama walilipwa) walidiriki hata kusabotage harakati za wazazi wao(kina Mandela).

  Vivyo hivyo hapa kwetu Tanzania hali ni hiyo hiyo. Kuna makundi ya aina tatu(maoni binafsi), kundi la kwanza ni lile linalofaidika na utawala uliopo(viongozi, wafanyabiashara). Kundi la pili ni la watu wanaotumika bila wao kujijua(wafanyakazi, wanachama wa vyama vya siasa) na kundi la tatu ni lile linalofanyakazi kwa niaba ya kundi la kwanza kifupi niwaite vibaraka(agents kama NEC, Msajili, UWT, Polisi, Media nk). Hili kundi la tatu linajua linachokifanya tofauti na kundi la pili.

  Nafikiri RedDevil utakuwa unazungumzia hili kundi la tatu(vibaraka). Hili kundi ni hatari sana katika harakati zozote zile ziwe za kijamii, kisiasa, kiuchumi, kimaendeleo nk. Hatari kwa misingi kuwa effect yake inagusa moja kwa moja maisha ya binadamu, chukulia polisi au media, tendo moja zuri au baya linalofanywa na vyombo hivi haliishii kwenye ofisi au mitambo yao tu linakwenda hadi kijijini kule kwa mtu anayelima matuta ya viazi.

  Vibaraka hao hao ndio wanaoendesha kampeni humu JF ya kuwakatisha tamaa wanaharakati wanaoonekana kutaka mabadiliko. Waliopo humu JF ingawa wanajitahidi sana kujificha (kutumia posts ofcourse) kwa kutoonyesha upande wowote lakini ukifuatilia posts zao lengo ni lile lile la kukatisha tamaa. Mfano mtu anakuja kuja na post hii ''Slaa ni kiongozi mzuri lakini kafanya makosa kuachia jimbo''. Post kama hii ukiisoma kwa juu juu si rahisi kum pin point mtu wa aina hii yupo upande gani, ila ukiichunguza kwa makini ni sentensi ya kukatisha tamaa(kubomoa) zaidi ya kujenga.

  Kuna mifano mingi ya watu wanaofanya hivyo humu ila sidhani kama ni busara kuwaongelea hapa, it is very sad. Lakini waelewe kuwa historia huwa inajirudia leo watawafanyia wenzao kesho si mbali itakuwa zamu yao kulipa the price. Kama Mlalahoi alivyosema the best thing to do ni kuwa ignore, hata kama kila siku kutakuwa na members wapya wa design hiyo lakini itafikia time wataanza kujiondoa wenyewe, kwa sababu ukombozi haukomi siku ya uchaguzi, navyojua mimi ukombozi unaanza baada ya uchaguzi.
   
Loading...