Ondoa habari za Tundu Lissu. Ukitaja jina la Tundu Lissu tu tayari kuna watu wana bias. Hata akija msibani watu watasema kaja kisiasa.Edward Snowden alivujisha siri za serikali lakini kwa usalama wake akakimbilia Hong Kong ambako ndiko alikofanyia hiyo "whistle blowing" kwa kumpa data mwandishi wa the Guardian ambae kwake ni source ya habari yake.
Baadae akifahamu madhara ya alichokifanya akaomba hifadhi ya ukimbizi nchini Russia na akatoroshwa na kuingia Moscow na hadi leo ni "most wanted man" na wamarekani.
Sasa Marekani ipo sheria na inakataza kuvujisha nyaraka na taarifa pamoja na siri za serikali, sheria hizi zimewekwa kwa makusudio fulani.
Je, kwa Tanzania twaona hali hiyo ni sawa kwasababu tu alevujisha amempa hizo taarifa Tundu Lissu?
Tuzungumze ukweli tusiwarubuni wasomaji wengine hapa.
Ondoa habari za Tundu Lissu. Ukitaja jina la Tundu Lissu tu tayari kuna watu wana bias. Hata akija msibani watu watasema kaja kisiasa.
Tuache specifics za case ya Tundu Lissu kiporo. Tutalirudia. Twende kujiuliza maswali kama ya Socrates ngazi kwa ngazi pole pole. Tutafika kwa Tundu Lissu. Lengo si kumtetea au kumuumbua Tundu Lissu. Lengo ni kupata ukweli.
Nimekuuliza swali hapo juu hujalijibu.
Mfanyakazi wa serikali anayefichua ubaya wa serikali kwa kuvujisha nyaraka za siri za serikali anastahili kutetewa kama whistleblower anayetuonyesha ubaya wa serikali au kuhukumiwa kama mfanyakazi msaliti aliyevunja maadili ya kazi yake kwa kuvujisha siri za serikali?
Sent from my Kimulimuli
Sidhani kama TISS wanajihusiaha na siasa.
Isitoshe kuna tetesi kwamba kuna jamaa wapo kwenye mikono salama saa hii wakiwasaidia TISS kuhusiana na hili la juzi.
Unaposema TISS ndiyo wanahuska kuvujisha hizo nyaraka na taarifa kwa maslahi mapana ya nchi unamaanisha nini?
Kwamba nchi itataifishwa? are you serious?
Tufafanulie kiongozi.
Nyaraka zipo katika computer yenye encryption ambayo mfanyakazi wa serikali tu ndiye anaweza kuzipata.Kwanza anaacha kazi na pili anatafuta mahali pa kujihifadhi na mwisho anatoa hizo nyaraka.
Mtumishi wa serikali huwa anakula kiapo cha kulinda siri za serikali kama masharti ya kuajiriwa.
Nchi zilizoendelea na kuwa na sheria nzuri hawa watu wana sheria za kuwatetea.Kama wana vujisha kwa maslahi ya nchi,nawaombea Mungu wazidi kupata zingine nyingi zaidi
Soma tena mkuu nadhani wewe ni wa kwanza kuuliza suali hilo.
Nimemtumia DT kama mfano.
Baaada ya taarifa kuwa zinavuja sana serikali ya Donald Trumpo iliamua kuomba kibali cha mahakama ambayo inaitwa US Foreign Intelligence Surveillance Court cha kufanya upelelezi kwa wandishi wote wa habari ambao wanaandika taarifa ambazo zinatokana na habari zilizovujishwa kutokea White House.
Iliaminika kuwa taarifa hizo zilikuwa zikivujishwa na ofisa wa serikali mstaafu, mwenye cheo cha juu ambae alikuwa ni mkuu wa moja ya idara za ujasusi wa Marekani.
Na huyu jamaa alikuwa alipata taarifa hizo kutoka kwa watumishi mbalimbali wa serikali ambao walikuwa chini ya raisi aliepita bwana Barak Obama.
Sasa kuna mtu hapa ametumia reference ya TISS kwamba wanavujisha taarifa na nyaraka.
Je kama ni hivyo je hii imekaa sawa kweli.
Suala ni kuvujishwa kwa nyaraka za serikali na watumishi wa serikali je, ni halali kulingana na miiko yao ya kazi?
Hivi kitu kama hichi nayo ni top secret au madudu ya serikali,...kuna watu nao wanachoka wanapenda nchi yao hawawezi kaa kuficha madudu, wafiche vitu vyaa maan sio madudu kama haya...tena watumishi kama hawa ndo tunao wataka maan sometimes serikali inapenda sana uongoo usio na tija si wangesema hadharani na hili ili tuwaunge mkono na tuoneshe uzalendoTundu Lissu wa Chadema amethibitisha kwamba anazo taarifa na nyaraka mbalimbali ambazo amepewa na baadhi ya watu wanaoaminika kwamba ni watumishi wa serikali.
Tundu Lissu amepewa nyaraka hizi na watu hawa kwa minajili ya kuzitumia kwa manufaa yake yaani kupalilia safari yake kisiasa na kujipatia umaarufu.
Ni hivi majuzi tu raisi wa Marekani Donald Trump alichukua hatua ya kurekebisha hilo ambapo baadhi ya wasaidizi wake wametuhumiwa kuvujisha taarifa mbalimbali kutoka ndani ya White House kwa waandishi wa habari na wapinzani wake.
Taarifa nyingi za serikali zina utaratibu wake wa kuzihifadhi na hupewa jina maalum la "top secret" au "classified information" kuzuia uwezekano wa kudukuliwa au kuibiwa,
Je, sheria inasemaje juu ya hili la kuvujisha taarifa na nyaraka za serikali kwa watumishi wa umma?
Je, yapi majukumu ya mdhibiti mkuu wa nyaraka za serikali na msemaji wa serikali au maofisa habari "information officers" kwamba labda kuna mahali wanapwaya?
Karibu tujadili bila kuingiza siasa.
Tunapojadili tuzingatia umuhimu wa kuhifadhi nyaraka na taarifa za serikali na wajibu wa maofisa habari na mdhibiti mkuu wa taarifa na nyaraka za serikali.
Mungu akubariki sana mkuu .Wee unadhani TISS wanafanya kazi na ccm tu????
Waliotoa hizo secret Info we unadhani ni raia wa kawaida????
Usalama wanafanya hivyo kwa maslai mapama ya nchi.... Huo ndio uzalendo nchi ikija kutaifishwa kwa madeni ya kizembe nani atakae laumiwa?? Serikali, jeshi la polisi, jwtz au usalama nani atakae laumiwa???
Siyo sahihi kabisa ila swala la kujiuliza kwanini inatokea what went wrong, weledi wa kiutawala unatakiwa, nafikiri ni wakati sasa viongozi wetu wa juu wakae kitako na kutafakari kwa kina kujua watumishi wake wanalalamika nini na shida zao ni zipi la sivyo tutakuja kupinduana kama siyo siri kuendelea kuvuja. Mungu bariki Taifa languSuala ni kuvujishwa kwa nyaraka za serikali na watumishi wa serikali je, ni halali kulingana na miiko yao ya kazi?
Hapa si walileta longolongo bungeniNchi zilizoendelea na kuwa na sheria nzuri hawa watu wana sheria za kuwatetea.
Sheria ya Wamarekani kutetea whistleblowers hii hapa.
Whistleblower Protection Act - Wikipedia
The Whistleblower Protection Act of 1989, Pub.L. 101-12 as amended, is a United States federal law that protects federal whistleblowers who work for the government and report agency misconduct. A federal agency violates the Whistleblower Protection Act if agency authorities take (or threaten to take) retaliatory personnel action against any employee or applicant because of disclosure of information by that employee or applicant. Whistleblowers[1] may file complaints that they believe reasonably evidences a violation of a law, rule or regulation; gross mismanagement; gross waste of funds; an abuse of authority; or a substantial and specific danger to public health or safety.
Sent from my Kimulimuli
Bunge letu ukiiangalia ile sheria ya makosa ya mtandao ni the opposite of whistleblower protection.Hapa si walileta longolongo bungeni
Ndio maana Nchi za kiAFRICA zimekuwa na Watawala wajinga Sana....yaani Hata akiona Twiga wanapakiwa kwenye Ndege asiseme Sababu ameapa...duh...Kwanza anaacha kazi na pili anatafuta mahali pa kujihifadhi na mwisho anatoa hizo nyaraka.
Mtumishi wa serikali huwa anakula kiapo cha kulinda siri za serikali kama masharti ya kuajiriwa.
mkuu, kama bosi mkuu mwenyewe anakiuka si maadili tu bali kuvunja katiba kabisa...wengine wafanyeje?Sasa kama unachoshwa unajiondoa na baadae unasemea pembeni badala ya kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kuvujisha nyaraka na taarifa?
Ndio maana yake Mkuu..ndio hali ilivyo au wewe huioni kaka.Kwa hiyo watu wamekata tamaa wanaamua kujilipua siyo?
After all that is for the benefit of our nation and not otherwiseHATA SERIKALINI KUNA WATU WANACHOSHWA NA MADUDU MKUU.AFU USISAHAU KUWA SERIKALI NI WATU NA WATU NDIO SISI
Hakuna nyaraka za siri zinazohusu wizi, nyaraka itakuwa siri iwapo hakutakuwa na wizi, kama ni hivyo hata escrow tusingeijuaTundu Lissu wa Chadema amethibitisha kwamba anazo taarifa na nyaraka mbalimbali ambazo amepewa na baadhi ya watu wanaoaminika kwamba ni watumishi wa serikali.
Tundu Lissu amepewa nyaraka hizi na watu hawa kwa minajili ya kuzitumia kwa manufaa yake yaani kupalilia safari yake kisiasa na kujipatia umaarufu.
Ni hivi majuzi tu raisi wa Marekani Donald Trump alichukua hatua ya kurekebisha hilo ambapo baadhi ya wasaidizi wake wametuhumiwa kuvujisha taarifa mbalimbali kutoka ndani ya White House kwa waandishi wa habari na wapinzani wake.
Taarifa nyingi za serikali zina utaratibu wake wa kuzihifadhi na hupewa jina maalum la "top secret" au "classified information" kuzuia uwezekano wa kudukuliwa au kuibiwa,
Je, sheria inasemaje juu ya hili la kuvujisha taarifa na nyaraka za serikali kwa watumishi wa umma?
Je, yapi majukumu ya mdhibiti mkuu wa nyaraka za serikali na msemaji wa serikali au maofisa habari "information officers" kwamba labda kuna mahali wanapwaya?
Karibu tujadili bila kuingiza siasa.
Tunapojadili tuzingatia umuhimu wa kuhifadhi nyaraka na taarifa za serikali na wajibu wa maofisa habari na mdhibiti mkuu wa taarifa na nyaraka za serikali.