Wanaovujisha taarifa na nyaraka muhimu za serikali, hii imekaaje?

Ni mawazo yangu tu, Mh Rais John Joseph Pombe Magufuli ,ni rais ambaye ana kila sababu ya Kupendwa na wananchi wa Tanzania.

Rais huyu aliingia madarakani akiikuta CCM ukiwa ktk khali mbaya,licha ya juhudi kubwa zilizofanywa na Mh Kinana na Mh Nnauye

Hawa magwiji wawili walijipanga kwa ufahamu mkubwa wa nn wananchi wanataka juu ya serikali yao, mpaka kuna baadhi ya mawaziri waliwaita Mizigo.

Kwa hakika hapa upinzani ulipigwa bao bila kujitambua wenzao walianza kampeni mapema ya kukinadi chama chao,kwa kuikosoa na kuipongeza serikali pale ilipostahili.

Baada ya purukushani zote,za upinzani kwa maana ya CHADEMA kuwa na operesheni sangara na CCM kuwa na ziara ndefu ya kuimarisha chama.


CHADEMA kwa maana ya UKAWA wakaibuka na neno MABADILIKO huku CCM wakiibuka na MABADILIKO YA KWELI, mpaka hapo unaona wote wanakubaliana Taifa linahitaji MABADILIKO ili lisonge mbele.

Kampeni zikapigwa mwisho mshindi akapatikana.na Mara moja tukaingia ktk shughuli za maendeleo,sio siri ni kujidanganya kwamba eti huwa tunasahau yalyopita ktk chaguzi.

Kwa hakika kabisa huwa tunahama na majigambo,matusi,majivuno,kejeli,visasi,upendo ,vurugu na kila kitu tunahamishia kwenye ushindi na kushindwa.


Ndo maana licha ya mafanikio ya serikali ya awamu ya 4 na madudu ya serikali hiyo upinzani ulipongeza na kuikosoa kwa nguvu zote.huku CCM wakipiga makofi ya kupongeza tu.

Sasa serikali ya awamu ya 5 iliyoingia kwa kauli mbiu ya MABADILIKO YA KWELI ilianza kwa kutoa kauli iliyoonesha kweli MABADILIKO mkuu aliwaambia CCM wenzake kubalini kushindwa.

Kauli hili aliitoa pale alipoona CCM, wanajitahidi kupindisha Hata palipo pagumu juu ya umeya wa jiji la Dar es salaam, baada ya kauli yske uchaguzi ukafanyika na maisha yakaendelea.

Naamini hili halikuwapendeza wana CCM wengi saana ndipo mbinu mbalimbali zinaandaliwa kumrejesha Mkuu kwenye ile CCM ISIYOPENDA MABADILIKO.

Ndo maana licha ya upinzani kuwa wa kwanza kuikosoa na kukemea juu ya mikataba mibovu juu ya Madini wizi wa ESCROW serikali haitaki kuwashirikisha kwa lolote.

Na ushauri wowote watakapoutoa popote haukubaliki zaidi ya kuonekana ni uchochezi hapa ndipo vile visasi,kejeli za uchaguzi zinapoendelezwa.

Naamini Mh Rais angeendelea na msimamo wake wa MABADILIKO ya kweli + MABADILIKO na kuamua kuuishi msemo wake Maendeleo hayana CHAMA.

Angependwa saana na kila upande angefahamu mengi na angetumbua wengi na nchi ingekuwa imepaa zaidi na zaidi.neno upendo likizingatiwa na Rais basi.
 
Siri ni pale kunapokuwa na taarifa zinazohatarisha usalama wa nchi, kukamatwa ndege nayo ni siri? fedha ni za watanzania wote hivyo wananchi wanahaki ya kujua zinatumikaje.
 
Sidhani kama TISS wanajihusiaha na siasa.

Isitoshe kuna tetesi kwamba kuna jamaa wapo kwenye mikono salama saa hii wakiwasaidia TISS kuhusiana na hili la juzi.

Unaposema TISS ndiyo wanahuska kuvujisha hizo nyaraka na taarifa kwa maslahi mapana ya nchi unamaanisha nini?

Kwamba nchi itataifishwa? are you serious?

Tufafanulie kiongozi.
Hivi Jack zoka alikuwa na cheo gani vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama TISS wanajihusiaha na siasa.

Isitoshe kuna tetesi kwamba kuna jamaa wapo kwenye mikono salama saa hii wakiwasaidia TISS kuhusiana na hili la juzi.

Unaposema TISS ndiyo wanahuska kuvujisha hizo nyaraka na taarifa kwa maslahi mapana ya nchi unamaanisha nini?

Kwamba nchi itataifishwa? are you serious?

Tufafanulie kiongozi.
Hivi Jack zoka alikuwa na cheo gani vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushabiki, chuki, tamaa, urafiki, ukabila na mengine mengi tu. Pia kukomoana kumbe wanajiabisha wenyewe, ndivyo mwananadamu alivyo.
Haya mambo ya kuvujisha si ya leo ila umekuwa "ugonjwa" sasa, alafu ni ngumu kujua nani yupo na wewe na mbinu zinabadilika kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu jibu umalo kuwa NI KINYUME NA MAADILI YA UTUMISHI, ila serikali ni watu (not ANGELS) so kuvuja kwa nyaraka/siri kutakuwepo hadi mwisho wa dunia. Kuhusu Trump,the guy amem-fire Chief Strategist wake kwa 'KUHISI KUWA ANAVUJISHA TAARIFA KWA WANA HABARI'. If JPM anaweza KUHISI fine,afukuze watu tu but siyo suluhu.
Maadili ya utumishi Tanzania si mwisho wa kipimo cha maadili.

Kwenye Nuremberg Trials, wanajeshi wa Hitler NAZI wa Ujerumani walishitakiwa kwa kuua. Wakajitetea kwamba wao hawakutaka kuua, ila walikuwa wanafuata maagizo ya wakubwa wao kazini na kwa mujibu wa maadili ya kazi yao ya kijeshi, mkubwa akisema ua, unaua. Usipoua, umevunja maadili ya kazi ya jeshi kwa kutotii amri ya mkubwa (insurbodination).

Majaji waliusikiliza utetezi ule na kuutupilia mbali kwa kusema kwamba, ingawa kazi ya kijeshi ina maadili yake, kwamba anachosema mkubwa lazima kifuatishwe, ama sivyo unavunja maadili kwa insurbodination, kila mtu anachukua jukumu la matendo anayofanya yeye mwenyewe, hata kama anafanya mambo kwa kufuata amri ya mkubwa au sheria ya kazi tu.

Kwa hiyo, kama kuna mkataba unaohalalisha sumu ya cyanide kutoka mgodi wa dhahabu iingie katika mto, halafu wanakijiji wanywe maji ya mto na kufa kutokana na sumu hiyo, halafu mfanyakazi wa serikali akauona mkataba huo na kujua hilo, halafu asiseme wala kuvujisha habari hizo watu wajue, mfanyakazi huyo atakuwa anashiriki katika mauaji hayo.

Kwa hivyo, kitu cha kuzingatia hapa ni kama kuna public good inapatikana na iko warranted kwa mfanyakazi kuvujisha nyaraka. Kama ipo, mfanyakazi actually morally atakuwa na makosa kama hajavujisha habari hiyo.

Sent from my Kimulimuli
 
Watumishi wenyewe mmewapuuza na matusi juu mnategemea waende wapi.?

kwa sasa wanalilia tumboni hakuna wa kuwasikiliza, wako kimya.

Ni vyema mkaona umuhimu wao kwa taifa!!

Madai yao ya kishenzi ila umuhimu wao??

Kupigwa moja tu mnalia. Wao mmewapiga for two years now wako kimya.

Wenda pia njaa zao na vilio vyao ndo vinavyo waadhibu.

Ukitenda haki utaishi kwa amani hata kama u masikini

Usipohaki utaishi kwa wasiwasi sana hata kama u tajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzalendo kuvujisha taarifa na nyaraka za serikali?

Mkuu unaelewa maana ya serikali?
Tangu lini deni kama hilo likawa siri.
Kwa utawala bora bunge linatakiwa lijue manunuzi na kupanga bajeti
Haya yanatofauti gani na yale ya RICHMOND zabuni za siri.
Acheni fikra mgando
Kuna siri ila sio hili la manunuzi bila utaratibu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inabidi uchunguzi ufanywe ijulikane wanao vujisha siri,hili jambo linaweza kutughalimu baadae kwa usalama wa taifa,kama mtu anavujisha siri kiurahisi anaweza kutumiwa hata na maadui na kusababisha matatizo,ila kama taarifa haina athari watoe tu.
Ni wazo zuri lakini kwa mwenye akili pia ataona
si vyema kiongozi mmoja kuwa na mamlaka makubwa kiasi cha kuitia nchi katika hatihati na madeni makubwa kiasi hiki kuna haja ya mabadiliko ili kuwe na usawa
Mbali na hapo haya yataendelea na serikali mpaka itashindwa kuendesha miradi yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu Lissu wa Chadema amethibitisha kwamba anazo taarifa na nyaraka mbalimbali ambazo amepewa na baadhi ya watu wanaoaminika kwamba ni watumishi wa serikali.

Tundu Lissu amepewa nyaraka hizi na watu hawa kwa minajili ya kuzitumia kwa manufaa yake yaani kupalilia safari yake kisiasa na kujipatia umaarufu.

Ni hivi majuzi tu raisi wa Marekani Donald Trump alichukua hatua ya kurekebisha hilo ambapo baadhi ya wasaidizi wake wametuhumiwa kuvujisha taarifa mbalimbali kutoka ndani ya White House kwa waandishi wa habari na wapinzani wake.

Taarifa nyingi za serikali zina utaratibu wake wa kuzihifadhi na hupewa jina maalum la "top secret" au "classified information" kuzuia uwezekano wa kudukuliwa au kuibiwa,

Je, sheria inasemaje juu ya hili la kuvujisha taarifa na nyaraka za serikali kwa watumishi wa umma?

Je, yapi majukumu ya mdhibiti mkuu wa nyaraka za serikali na msemaji wa serikali au maofisa habari "information officers" kwamba labda kuna mahali wanapwaya?

Karibu tujadili bila kuingiza siasa.

Tunapojadili tuzingatia umuhimu wa kuhifadhi nyaraka na taarifa za serikali na wajibu wa maofisa habari na mdhibiti mkuu wa taarifa na nyaraka za serikali.
Kwani Serikali kudaiwa ni Siri kwasababu anayelipa ni mimi na wewe kwa kodi zetu
 
Edward Snowden alivujisha siri za serikali lakini kwa usalama wake akakimbilia Hong Kong ambako ndiko alikofanyia hiyo "whistle blowing" kwa kumpa data mwandishi wa the Guardian ambae kwake ni source ya habari yake.

Baadae akifahamu madhara ya alichokifanya akaomba hifadhi ya ukimbizi nchini Russia na akatoroshwa na kuingia Moscow na hadi leo ni "most wanted man" na wamarekani.

Sasa Marekani ipo sheria na inakataza kuvujisha nyaraka na taarifa pamoja na siri za serikali, sheria hizi zimewekwa kwa makusudio fulani.

Je, kwa Tanzania twaona hali hiyo ni sawa kwasababu tu alevujisha amempa hizo taarifa Tundu Lissu?

Tuzungumze ukweli tusiwarubuni wasomaji wengine hapa.
Unakifahamu alichovujisha snowden?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza anaacha kazi na pili anatafuta mahali pa kujihifadhi na mwisho anatoa hizo nyaraka.

Mtumishi wa serikali huwa anakula kiapo cha kulinda siri za serikali kama masharti ya kuajiriwa.
Ipo siku sheria za kutia watu upofu ili kuhalalisha maovu , ubadhilifu na ufisadi zitazeeka na kufa.

Na nina imaani zitazaliwa sheria mpya zenye kuwapa watu uwazi wa serikali yao na matumaini mapya yenye kuvutia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom