mjukuum
JF-Expert Member
- Dec 8, 2014
- 5,254
- 2,823
Ungesema ni uongo ingekuwa sawa lkn kama kweli mmmmmTundu Lissu wa Chadema amethibitisha kwamba anazo taarifa na nyaraka mbalimbali ambazo amepewa na baadhi ya watu wanaoaminika kwamba ni watumishi wa serikali.
Tundu Lissu amepewa nyaraka hizi na watu hawa kwa minajili ya kuzitumia kwa manufaa yake yaani kupalilia safari yake kisiasa na kujipatia umaarufu.
Ni hivi majuzi tu raisi wa Marekani Donald Trump alichukua hatua ya kurekebisha hilo ambapo baadhi ya wasaidizi wake wametuhumiwa kuvujisha taarifa mbalimbali kutoka ndani ya White House kwa waandishi wa habari na wapinzani wake.
Taarifa nyingi za serikali zina utaratibu wake wa kuzihifadhi na hupewa jina maalum la "top secret" au "classified information" kuzuia uwezekano wa kudukuliwa au kuibiwa,
Je, sheria inasemaje juu ya hili la kuvujisha taarifa na nyaraka za serikali kwa watumishi wa umma?
Je, yapi majukumu ya mdhibiti mkuu wa nyaraka za serikali na msemaji wa serikali au maofisa habari "information officers" kwamba labda kuna mahali wanapwaya?
Karibu tujadili bila kuingiza siasa.
Tunapojadili tuzingatia umuhimu wa kuhifadhi nyaraka na taarifa za serikali na wajibu wa maofisa habari na mdhibiti mkuu wa taarifa na nyaraka za serikali.
Sent using Jamii Forums mobile app