Wanaoutafuta urais kwa udi na uvumba ni hatari kwa taifa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaoutafuta urais kwa udi na uvumba ni hatari kwa taifa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Mar 1, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Nimeonelea ni vyema kuonyesha hatari kubwa inayolinyemelea taifa kwa siku za husoni kutokana na uwepo wa Watanzania wenzetu ambao nyoyo zao wamezielekeza katika Kuhakikisha Kwamba wanakuja kuchukua nafasi za uongozi wa Taifa letu.

  Nakumbuka around Mwaka kati ya 2007/2008 Zitto Kabwe akihojiwa na Mwandishi wa Gazeti Moja nchini (TAZAMA bila shaka) katika kipindi ambacho alikuwa kwenye mvutano fulani na spika wa Bunge wa wakati huo Ndugu SAMWEL SITTA, ghafla alibadilisha upepo wa Majadiliano alipotoa kauli kwamba ndugu LOWASA ndio chanzo cha Uendeshaji wa Bunge vibaya kwa kutokuzingatia maslahi ya Taifa, na akasema Kwamba LOWASA alikuwa anatumia nafasi yake kama Waziri Mkuu kuwabana na kuwaelekeza wabunge wa CCM pamoja na speaker wa Bunge katika mambo mbalimbali ya michakato ya Kibunge katika namna iliyokuwa ikikinzana na maslahi ya Taifa, ZITTO akaeleza kwamba na kilichokuwa kikimsukuma Ndugu LOSAWA kufanya Hayo ni NAFASI YA URAI MWAKA 2015.

  Mimi binafsi sikuitilia maanani kauli hiyo ya ZITTO, lakini sasa nimeikumbuka, na baada ya kuichunguza nimegundua ilikuwa ni kauli nzito sana na inayostahili kuangaliwa kwa umakini.

  Sasa bila shaka nakili kwamba ZITTO alikuwa sahihi kabisa kwa kile alichokiona katika Dhamira ya ndugu LOWASA, na tukiangalia harakati zake za sasa ni vigumu sana kubisha kwamba in fact alianza harakati hizi kabla ya mwala 1995 na dhamira hiyo haijawahi kuyeyuka wala kupungua zaidi ya kwamba imekuwa ikiongezeka mara dufu kila kukicha.

  Ukipiga mahesabu ya kukadiria sana, ni kwamba huyu Bwana amekuwa akitafuta nafasi ya urais kwa kipindi cha miaka 17 mpaka sasa, na itapofika mwaka 2015 atakuwa ametimiza miaka 20 katika harakati hizi. 20 YEARS MTU ANATAFUTA URAIS.

  Naamini kutokana na uchanga wa nchi yetu hatujawahi kupata fursa ya kuexperience madhara ya kuwa na watu wa namna hii hasa inapotokea wakafanikiwa kuchukua uongozi wa nchi. naomba nitoe mifano michache.

  KENYA
  Raila Odinga na Uhuru Kenyatta, wakubali au wasikubali, wala haiitaji uchunguzi wa ocampo kutambua kwamba, mikakati yao ya kutaka kuliongoza taifa hilo jirani ya muda mrefu sana ikiambatana na matumizi makubwa ya pesa ndio iliyopelekea kutokea kwa mauaji ya raia mara baada ya uchaguzi mkuu uliopita nchini mwao.

  ZIMBABWE
  Tshvangrai, nae amekuwa chanzo cha machafuko na kuporomoka kwa uchumi ya nchi hiyo kutokana na kuutaka Urai wa nchi hiyo kwa muda mrefu sana.

  SENEGAL
  Huku tukiendelea kufuatilia mchakato wa uchaguzi nchini humo, tukumbuke kwamba Rais Abdoulaye Wade alianza mchakato wa kutaka kuiongoza nchi hiyo akiwa na miaka around thelathini, ameifanya kazi hiyo for about 40 years, sasa ameifanya Ikulu ya Senegal kama roho yake, ataki kuachana nayo. tuiombee senegal ipite kipindi hiki salama.

  UGANDA
  Wanalazimika kuwa makini sana na yule DR wa zamani wa Mseveni ambaye siku hizi anasema "anawalk to work", Jambo lolote baya lenye sura ya kisiasa likitokea Kampala leo, Besigye atakuwa anahusika. Japo anamsakama Museveni kwa kukaa Madarakani Muda mrefu lakini na yeye amekuwa akiutaka urais for as long as museveni has been there.

  NIGERIA
  Atiku Abubakari, sidhani kama harakati za kiinteligensia hazitamkuta na mahusiano na Boko haramu, Wanaigeria sasa wanalia na wanasiasa sababu wanasiasa wenye mahaba makubwa na nafasi ya urais wa Taifa hilo kubwa Africa wanasemekana kufinance kundi la boko haramu, nimemtaja hapa Atiku sababu kuna uwezekano mkubwa akawa ndio mnigeria anayeufikiria Urais wa Taifa hilo kama ndugu lowasa hapa Tanzania. Kwa kifupi ni kwamba Nigeria sasa inapasuka pasuka.Tuiombee Nigeria Jamani.

  Achana na LIBYA, MISRI, YEMENI na sasa SYRIA, ambako wale wanaoutolea denda Urais wa nchi hizo hawakuwahi kuonyesha active intentions, bali hasa kutokana na kubanwa na marais waliokuwapo katika nchi hizo walilazimika ama kuficha, ama kuendesha harakati zao kisiri sana, mwisho wa siku kwa namna moja ama nyingine, huku wakitegemea kuingia madarakani kirais rais tu wamejikuta wanafanya maamuzi ambayo nadhani kutokana na nchi hizo kupoteza kabisa kabisa uwezekano wa kutawaliwa kidemocrasia sasa wanasema "Poa tu, Bora tukose wote"

  Tanzania balaa hizi hazijawahi kutukuta, na hapa nachukua fursa hii kama Mtanzania mzarendo kabisa, kuihasa nchi kwamba tunalazimika kuwa makini na watanzania wenzetu ambao kiu zao za kutaka urai zimepita kipimo, sababu uwezekano wa watu hawa kutuletea matatizo ni makubwa, nawata sasa

  1. Jakaya Mrisho Kikwete
  Huyu tayari yake yametimia, na anaendeleza kuyafanikisha ipasavyo, uchumi wa nchi yetu umeshuka, uchumi
  wa nchi yetu umepoteza virutubisho vya kuuwezesha kukua, maisha kwa watanzania yamekuwa ni magumu sana,
  Dhana nzima ya Uongozi imepoteza maana kabisa na sasa taratibu serikali yake imeanza kufanya mazoezi ya kuua
  raia kwa risasi za moto. Wote tunajua ni kwa muda gani Kikwete alikuwa kwenye mchakato wa kuutaka Urais
  mpaka dhamira hiyo ilipotimia 2005. Kuna watu wanadai kuna kipindi, kabla hajawa Rais, akiwa kwenye moja ya
  ya mikutano ya chama, mapema sana kabla hata muda wa kufikiria kuhusu mambo ya uchaguzi hayajaanza,
  akiubuka na kudai anahujumiwa, kwa machungu sana machozi yalimtoka.

  2. EDWARD LOWASA
  3. ZITTO KABWE
  4.
  5

  Mnaweza mkaweka wengine tuwatambue, lakini Jina la PROFESA LIPUMBA nisilione sababu huyu hajawahi kuutaka Urais. anachokifanya anajua mwenyewe.

  Nawasilisha.
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2

Loading...