Wanaotumia usafiri wa anga hapa Tanzania soma hapa

ThinkPad

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,843
1,250
Wanajamii tuliunge mkono shirika la ndege la Tanzania kwa kupanda ndege zake (yake) sasa hivi precission na 540 wameshusha bei baada ya kuona wings of Kilimanjaro wanatozo ndogo sasa siku zote walikuwa wapi kushusha gharama mpaka wakafanya usafiri wa ndege kama anasa.

Wito kwa watanzania wote wana jambo forum wote tuichangie air Tanzania.

Kwanza ndege yao ni nzuri na ya uhakika tuinue shirika letu linalo endeshwa kwa kodi zetu ili lifanikiwe.

Chizi kajitahidi sana ilikuwa aibu sana kuwa hatuna ndege kubwa.

Ndege zingine zinachangiwa lakini uzalendo hakuna so tuijaze ndege yetu kwanza kisha ndio twende kwa hao wengine.
 
Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,721
2,000
Kweli precission air inamanyanyaso sana nakumbuka hata kipindi 540 wameingia wakashusha bei...Nimekusikia na nitabadili njia na kukamata Wing of Kilimanjaro.
 
Jungumawe

JF-Expert Member
May 2, 2009
248
225
wanajamii tuliunge mkono shirika la ndege la tanzania kwa kupanda ndege zake (yake) sasa hivi precission na 540 wameshusha bei baada ya kuona wings of kilimanjaro wanatozo ndogo sasa siku zote walikuwa wapi kushusha gharama mpaka wakafanya usafiri wa ndege kama anasa. Wito kwa watanzania wote wana jambo forum wote tuichangie air tanzania. Kwanza ndege yao ni nzuri na ya uhakika tuinue shirika letu linalo endeshwa kwa kodi zetu ili lifanikiwe. Chizi kajitahidi sana ilikuwa aibu sana kuwa hatuna ndege kubwa. Ndege zingine zinachangiwa lakini uzalendo hakuna so tuijaze ndege yetu kwanza kisha ndio twende kwa hao wengine.
bei yake shilingi ngapi mza - dar, dar - kia
 
Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,306
2,000
usalama uko vipi.......nimekuwa nikisikia mara kwa mara kuwa zinalala chali.......vipi hilo tatizo....limerekebishwa.....? naogopa jamani....
 
MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,000
usalama uko vipi.......nimekuwa nikisikia mara kwa mara kuwa zinalala chali.......vipi hilo tatizo....limerekebishwa.....? naogopa jamani....

Preta you're there. Mi ninachojali kwenye ndege siyo bei bali usalama wa ndege na marubani competent ambao hawaifanyi safari kuwa HOFU angani. Je security na comfortability ya huu usafiri wa Air Tanzania ukoje na wanaweza ku maintain au ahadi za ki-CCM za nguvu ya soda?
 
bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,386
2,000
Waungane waTanzania kwa bei hiyo ya promosheni, kwa taarifa yako hiyo ATCL sijui ATC hawana lolote hiyo ni bei ya promosheni kuitambulisha hiyo ndege yao ya kukodi na siku si nyingi wataweka bei ya ukweli, otherwise kama ndo itakua bei yao pamanent nawapa miezi mitatu tu hiyo ndege itakua haioparate tena, take it or leave it.
 
webondo

JF-Expert Member
Apr 29, 2012
1,715
1,500
Wanajamii tuliunge mkono shirika la ndege la Tanzania kwa kupanda ndege zake (yake) sasa hivi precission na 540 wameshusha bei baada ya kuona wings of Kilimanjaro wanatozo ndogo sasa siku zote walikuwa wapi kushusha gharama mpaka wakafanya usafiri wa ndege kama anasa.

Wito kwa watanzania wote wana jambo forum wote tuichangie air Tanzania.

Kwanza ndege yao ni nzuri na ya uhakika tuinue shirika letu linalo endeshwa kwa kodi zetu ili lifanikiwe.

Chizi kajitahidi sana ilikuwa aibu sana kuwa hatuna ndege kubwa.

Ndege zingine zinachangiwa lakini uzalendo hakuna so tuijaze ndege yetu kwanza kisha ndio twende kwa hao wengine.
Umenena vyema kabisa! Uzalendo kwanza!
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,934
2,000
Atcl inatuahibisha,jay z,50 cent wana ndege zao binasfi na boti,yani sirikali inashndwa kununua ndege hata 5?? Kweli? Wanashindwa hata na lil wayne?
 
RC.

JF-Expert Member
May 24, 2012
444
0
maisha magumu sana mlo mmoja kwa siku,twaweza kupanda ndege kweli?
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
2,000
Atcl inatuahibisha,jay z,50 cent wana ndege zao binasfi na boti,yani sirikali inashndwa kununua ndege hata 5?? Kweli? Wanashindwa hata na lil wayne?
acha utoto wewe, hapa point ni kupanda ndege za atcl sio kulinganisha, hao wakina jz wanayo ndege kama ya jakaya?
 
ThinkPad

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,843
1,250
Air Tanzania ya sasa sio ile tulio izoea yaani ni ndege ya uhakika.
mapilot wako fit sio wale walio idundisha ile ndege iliyolala pale mwanza eti hali ya hewa.
 
ThinkPad

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,843
1,250
Waungane waTanzania kwa bei hiyo ya promosheni, kwa taarifa yako hiyo ATCL sijui ATC hawana lolote hiyo ni bei ya promosheni kuitambulisha hiyo ndege yao ya kukodi na siku si nyingi wataweka bei ya ukweli, otherwise kama ndo itakua bei yao pamanent nawapa miezi mitatu tu hiyo ndege itakua haioparate tena, take it or leave it.

yaani hatukatai kuwa inaweza kupandishwa tunachosema nikwamba pamoja na kila kitu mfano makampun mengine kushusha nauli za ndege tuipe kipaumbele ATC shirika la Serikali yetu.
 
Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
25,402
2,000
Hivi kumbe TTCL wanandege?? aa sore ATCL!! kama hivyo poa..basi na waweke nauli buku kazaa tu na kinasie tukasalimie makwetu fasta ..lakini chonde chonde msituingize baharini tu..
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,169
2,000
usalama uko vipi.......nimekuwa nikisikia mara kwa mara kuwa zinalala chali.......vipi hilo tatizo....limerekebishwa.....? naogopa jamani....

pamoja na kuwa umesababisha nicheke, ila point ya msingi sana tu, juzi kati ilianguka kiwanjani huko kigoma, vipi usalama wake?
 
Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,952
2,000
Mpaka sasa hatujawekwa sawa kuhusu ajali ya Mwanza na ya Kigoma, na hatujaelezwa jinsi gani ile Airbus iliyokuwa imekodiwa awali ilivyoondolewa kiaina. Na zaidi ya yote ATCL ndege yao hiyo moja ni ya kukodi wakati Precission ndege zao ni za kununua wenyewe, je kwa kuchangia kwetu kutawasaidia kwa upeo gani wajikomboe ili wanunue yao?.
 
Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
1,500
Waungane waTanzania kwa bei hiyo ya promosheni, kwa taarifa yako hiyo ATCL sijui ATC hawana lolote hiyo ni bei ya promosheni kuitambulisha hiyo ndege yao ya kukodi na siku si nyingi wataweka bei ya ukweli, otherwise kama ndo itakua bei yao pamanent nawapa miezi mitatu tu hiyo ndege itakua haioparate tena, take it or leave it.

Very True!!!!!!
 
RealMan

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,367
2,000
Moyo wa kuisupoti ATCL upo ila serikali hii haiaminiki.
ATCL ikipata faida JK nae si ataongeza trip za Ulaya?

Kwanza kwa nini wameajiri cabin crew (ma air hostes) wa kigeni, je hakuna watz wenye sifa (warembo) stahiki??

Waonyeshe uzalendo wao kwanza ndipo tutawaunga mkono.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom