Wanaotaka Chadema ishinde Urais, Ubunge na Udiwani.. .. Waichangie!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaotaka Chadema ishinde Urais, Ubunge na Udiwani.. .. Waichangie!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 23, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mbona wana CCM hawaoni aibu kuchangia chama chao na kuomba fedha kutoka kwa wananchi tena kwa mbwembwe zinazosindikizwa na wasanii wa kizazi kipya waliochakachuliwa?

  Wengi wanaonesha wanataka Chadema ishinde, lakini ushindi una gharama au itashinda kwa kuombewa na kunuiwa na kungojewa? Ushindi hauji, unaletwa! Kama vile wana CCM walivyo na haki ya kukichangia chama chao na wagombea wao, kutoa muda na vipaji vyao, wale wanaounga mkono Chadema au chama kingine chochote na wao wawe tayari kuchangia na hapa nazungumzia fedha kidogo kilichopo chaweza kuwa ni badiliko kati ya ushindi na kushindwa!


  Ndio hayo kwa leo!
   
 2. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Namna ya kuchangia na account namba au kwa simu hizi hapa. kwenye tanzania daima ukurasa wa mbele zinapatikana
  ACCOUNT NAMBA
  CHADEMA NMB 2266600140

  CHADEMA-M4C CRDB 01J1080100600

  KWA NJIA YA SIMU

  TUMA NENO CHADEMA KWENDA 15710 AU SLAA KWENDA 15710 KWA MITANDAO YA ZAIN VODACOM NA TIGO

  AU KWA NJIA YA M-PESA KWENDA 0758 22 33 44 AU 0764 77 66 73

  AU KWA ZAP KWENDA 0789 555 333
   

  Attached Files:

 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,551
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji,
  Thanks for this initiative ya kutukumbusha,
  Kusema ukweli ni muhimu kujitoa kwa moyo kuchangia for a good cause.
  Asante tena kutukumbusha.
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  sote tunaodai kutaka mabadiliko ni lazima tutake ownership of the process, kwa kila mmoja wetu kuplaya his.her part. Dr slaa anagombea urais, wapo wanaogombea ubunge, wapo wanaofanikisha na kuratibu shughuli za chama na sisi wengine tunatakiwa kuhakisha kuwa zinkuwepo resources za kufanikisha the process. Mbona harusi tunachangia sana au kwa sababu tutaendakula na kunywa kile tulikichangia?

  laiti kama watu wote wanaojaa katika mikutano ya chadema na wale ambao wanaamini katika mabadiliko wangechangia shs 5,000 tu kila mwezi katika hii miezi miwili ya kampeni, nakuhakikshia ushindi kwetu ungekuwa dhahiri
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  1. CHADEMA hawana account ya paypal????????? au ndiyo ile sheria mpya kwamba tulio nje ya nchi haturuhusiwi kuchangia. Mwenye kufahamu hili pls tujulishane.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Heshima mbele Mkuu MMKJJ: Usemayo ni ukweli. Hata hivyo watu wanachangia sana isipokuwa tu labda niseme tofauti na CCM, uwezo wao mdogo. Wengi wa wale matajiri wakubwa hawako upande wa Chadema, wako upande wa CCM, na serikali ya CCM ina uwezoi namna ya kuwakamua wachangie. Sina haja kueleza inafanya vipi.

  Sasa hii ya kuchangia Chadema kwa mwananchi mmoja mmoja haiwezi kuleta hela ya kushindana na CCM, chama ambacho ambacho kinaweza kuitisha fundraising pale Kempiski na mafisadi wakachangia mabilioni kwa masaa tu.

  Na ndo maana chama kama Chadema (na iliwahi kutokea huko nyuma kwa NCCR) kinakazania kupata kura za urais zaidi kuliko za wabunge majimboni. Kuna sababu mbili:

  Kwanza katika demokrasia za nchi za Kiafrika power iko Ikulu, mtu asikudanganye. Hebu fikiria -- iwapo Mrema angeshinda urais mwaka 1995 (pamoja na kupata wabunge wachache -- jee CCM ingekuwapo kama ilivyo leo?

  Pili, hata kama Slaa hatashinda urais, lakini idadi ya kura anazoweza kupata, ukijumlisha na idadi ya wabunge na madiwani Chadema itakaopata itaweza kukihakikishia chama hicho mamilioni ya fedha kama ruzuku, fedha ambazo zinaweza kutumika kujiimarisha majimboni katika chaguzi zijazo, kama vile kuajiri makatibu wa kulipwa mishahara -- na siyo wa sasa wa kujitolea ambao ni rahisi kununuliwa na mapesa ya CCM.


   
 7. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena mkuu
   
 8. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nadhani ipo njia. Ukiwa nje unaweza kutuma hela CRDB through Citibank na itafika kwenye akaunti husika. mimi nimekua nikipokea fedha toka nje through Citibank to my account in CRDB
   
Loading...