Wanaotafuna Pesa za Jimbo la Kawe ni hawa hapa...

Ni jambo la ajabu na aibu kubwa kuwa na Rais anayesema uongo hadharani kuwataja wabunge hasa wa upinzani kuwa ndio wanakula pesa za mfuko wa jimbo wakati anafahamu kuwa sheria haina nafasi kwa mbunge kutumia pesa hizo.

Rais Magufuli kwa kweli hatufai kabisa maana amekuwa msema uongo bila hata aibu hadharani.

Kwa nini ni muongo hivi?
Ashajua nyiny hamjui kitu mnafuata tu mkumbo rejea ile kujenga na kununua kwa pesa zetu nilicheka sn angekuwa nch zilizostarabika anheshapigwa na mayai viza
 
:D Hizi siyo spana tena bali ni nyundo..

Zama za kudanganyana zilishaisha!

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Bwashee unaniangusha! Na wewe ulikuwa huujui huu utaratibu? Na ufafanuzi huu, ni kumtetea Mdee, au ni kuwafunua macho watu wote ambao walikuwa wanawatuhumu Wabunge wao kuwa wanazifanya fedha hizo kuwa zao?

Nilikuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu mfuko wa jimbo, ila sio kwa kiwango hicho cha kisheria. Ndio raha ya kuwa hapa jukwaani kwa ajili ya elimu pana.
 
Mimi bado nashangaa kama majimbo ya upinzani ndo hayana maendeleo kwanini JPM hajaja kwenye majimbo yetu CCM hasa huku Ukonga ili tujimwambafai nae kwa hayo maendeleo hewa tuliyonayo? Kwanini sisi ndo atutumie watu wengine tena hapa hapa dar anatembelea kwa upinzani huko kuendelea kuwaongozea maendeleo huko? Na sisi wa CCM tena tuliokimbiwa na Mbuge Waitara kashindwa kuja kutupa maendeleo na kuona shida zetu.
 
Umetumia nguvu kubwa sana kumtetea Halima Mdee!
MaCCM jipangeni upya na mtumie mbinu za kisasa kuwashawishi WANANCHI,tatizo mnafikili watanzania wa leo ni wazama za mawe,hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu anaweza kumchagua Gwajima,
Hata wale alipokuwa anawaona kama wajinga kwa sasa wameshituka hawaendi tena kanisani.
Cc.
Zimebaki wiki mbili mjitokeze tena kuwa Chadema na Mdee wamewaibia kura za hawala yenu Gwajima.
 
Ni jambo la ajabu na aibu kubwa kuwa na Rais anayesema uongo hadharani kuwataja wabunge hasa wa upinzani kuwa ndio wanakula pesa za mfuko wa jimbo wakati anafahamu kuwa sheria haina nafasi kwa mbunge kutumia pesa hizo.

Rais Magufuli kwa kweli hatufai kabisa maana amekuwa msema uongo bila hata aibu hadharani.

Kwa nini ni muongo hivi?
Magufuli ni kituko.
 
Nyambiti mkubwa, hivi kazi ya mbunge ni ipi pimbi wewe? Je ni kuruka ruka au kutukana? Gwaji boy ana bonge la PR na connection, na nina uhakika Gwaji atashinda
Siku zote nasema hakuna mwenye monopoly ya matusi. Kuniita Nyambiti au Pimbi hakukusaidii lolote wala haliendelezi mjadala kuwa na tija. Nani atashinda kati ya Halima na huyo umuitae Gwaji siyo issue kwangu. Soma kwa umakini uelewe hoja yangu kama utataka, ukifanya hivyo lete mrejesho wa kisomi, vinginevyo tufunge huu mjadala.
 
Chige,

..nashukuru kwa ELIMU uliyonipa.

..haswa kuhusu kamati inayoelekeza matumizi ya fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo.

..mimi kilio changu ni kwamba fedha hizo ni kidogo sana kuweza kuwa na impact ktk maendeleo ya wananchi.
 
Rafiki yetu halima ni mwizi kabisa hata umtetee vipi, kibaya hata kuongea na rais au bungeni kuhusu kero za jimbo hajawahi zaidi ya matusi
Kaja bunju wiki mbili zilizopita na kabla ya hapo alionekana 2010.

Jamaa kaandika mbwembwe nyingi. Zikijadiliwa mada zenye kuyahusu maslahi ya kawe huyo mbunge na wenzake wanavaa vitambaa midomoni na kutoka nje.

Rais anajua anachoongea kuwahusu hao jamaa wa CDM na wabunge wengine wa upinzani.
 
Kaja bunju wiki mbili zilizopita na kabla ya hapo alionekana 2010.

Jamaa kaandika mbwembwe nyingi. Zikijadiliwa mada zenye kuyahusu maslahi ya kawe huyo mbunge na wenzake wanavaa vitambaa midomoni na kutoka nje.

Rais anajua anachoongea kuwahusu hao jamaa wa CDM na wabunge wengine wa upinzani.

..Na Ndugai anapofungia wabunge wa upinzani kuhudhuria vikao vya bunge hajui kwamba kuna maslahi ya wananchi yatakuwa yanajadiliwa? Na majimbo yanayoongozwa na ccm maeneo mbalimbali lakini yamekithiri kwa umasikini mna utetezi gani?
 
Umetumia nguvu kubwa sana kumtetea Halima Mdee!
Hajamtetea Halima sababu Halima hana hatia yoyote. Ameeleza ukweli jinsi hiyo pesa inavyotunzwa na kupangiwa na kuidhinidhishiwa matumizi. Kila mwenye akili timamu anajua wazi kiongozi yeyote wa upinzani angekula hata senti moja ya huo mfuko hangekaa hata siku ipite kabla ya kuburuzwa mahakamani. Majizi makubwa nchi hii ni wanaccm. Shangaa kwa nini mahakama ya mafisadi haina wateja (wengi). Weka jimbo la Kawe pembeni, jaribu kuangazia mjimbo mengine ambayo wabunge wao ni wa ccm- mfano Kongwa. Mbona majimbo hayo kuna umaskini mkubwa na hatusikii propaganda za ovyo kwamba pesa imeliwa na mbunge? Propaganda hizi lengo lake ni kuendelea kuwapumbaza Watanzania waendelee kuichagua ccm ambayo imetawala nchi hii miaka 60 sasa bila nchi kupata maendeleo yanayolingana na rasilimali zilizopo.
 
Ume elimisha sana lakini ukweli unabaki, Wabunge wote waliokaa majimboni kwao kwa zaidi ya miaka 10 au vipindi viwili wanatengenezewa sana mizengwe.

Watu wa Kawe wamemchoka Halima na sio vinginevyo.
Kwa mara ya kwanza naona umetumia kichwa chenye ubongo kuandika,si kama kawaida yako ya kutumia kichwa kubebea masikio,macho,pua na mdomo.
Kongole kwa hilo.
Wabunge wanatengenezewa zengwe. Hapa naamini ni wa vyama vya upinzani.
 
Chige,

..nashukuru kwa ELIMU uliyonipa.

..haswa kuhusu kamati inayoelekeza matumizi ya fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo.

..mimi kilio changu ni kwamba fedha hizo ni kidogo sana kuweza kuwa na impact ktk maendeleo ya wananchi.
JK,

Unajua siku chache zilizopita nilibaki nacheka mwenyewe hapa JF nilipoona thread moja ikisema eti Mdee katafuna zaidi ya Bilioni 3!!

Nikawa najiuliza hivi huyu mtu anafahamu hata kiwango chenyewe cha pesa ya jimbo!!! So, nakubaliana na wewe kwamba kiwango ni kidogo mno!!
 
Back
Top Bottom