Wanaotafuna Pesa za Jimbo la Kawe ni hawa hapa...

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,946
2,000
Kwa muda mrefu hivi sasa kumekuwa na propaganda kuhusu utafunwaji wa Pesa za Mfuko wa Jimbo huku wengi wakimtuhumu Halima Mdee, Mbunge wa Kawe kuzitafuna pesa hizo!

Ingawaje waendesha propaganda hawa wanataka kuaminisha watu kwamba mkwamo wa Jimbo la Kawe unatokana na ulaji wa fedha za jimbo unaofanywa na Halima Mdee, lakini hawatuambii mkwamo wa majimbo yanayoongozwa na CCM kwa miongo kadhaa hivi sasa unatokana na hizo pesa kutafunwa na akina nani!

Kwa bahati mbaya sana, si kila mmoja anayefahamu utendaji wa serikali yetu na kutokana na hilo, ni rahisi sana watu kuamini kwamba Halima Mdee ndie anayekula pesa za Mfuko wa Jimbo la Kawe!

Aidha, Waswahili hunena kwamba, uongo ukiachwa uendelee hatimae hugeuka kuwa ukweli na watu kuuamini!! Ni hayo mawili ndiyo yamenisukuma kuelezea matumizi ya fedha za jimbo unavyokuwa!

Short version ya maelezo hayo ni hii hapa chini:
Awali ya yote, pesa kutoka Mfuko wa Uchocheaji wa Maendeleo ya Jimbo hutunzwa kwenye akaunti maalumu ya jimbo husika!

Ibara ya 22(2) ya Sheria ya Mfuko wa Uchocheaji wa Maendeleo ya Jimbo inampa mamlaka Mkurugenzi kuteua benki anayotaka Akaunti ya Jimbo ifunguliwe!

Kwa maana nyingine, Mbunge hana hata nafasi ya kusema akaunti ifunguliwe benki ipi lakini wenye nafasi hiyo ni watu wa serikalini!!!

Sasa ndo hapo sasa...akaunti imeshafunguliwa kwenye benki iliyotakiwa na DED mwenyewe... Je, mfumo wa utoaji pesa unakuaje?!

Swali hilo linajibiwa na Ibara ay 22 (3) (a &b) kwamba:-

- Saini 2 zitahitajika katika kufanya malipo au kutoa pesa, na katika saini 2 hizo, saini moja ni ya mtu kutoka Kundi A na nyingine kutoka Kundi B (Mandatory)!

-Kundi A litaundwa na Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Afisa Mipango wa Halmashauri,

-Kundi B litaundwa na Mweka Hazina wa Halmashauri na Mhasibu wa Halmashauri!

Kwa mara nyingine, utaona wanaotia mikono kwenye hiyo pesa ni watu wa serikalini peke yao!!! Na kwa kuangalia ile signing arrangement iliyotajwa hapo juu, maana yake ni kwamba Mkurugenzi pamoja na Mweka Hazina au Mhasibu wanaweza kutoa pesa; au Afisa Mipango na Mweka Hazina au Mhasibu pia wanaweza kutoa pesa.

Kwa maana nyingine, kama kweli pesa ya Mfuko wa Jimbo la Kawe imeliwa basi waliokula pesa hiyo ni watu wa serikalini kwa sababu, Mbunge kama mbunge, pamoja na kuwa ndie mwenyekiti wa kamati lakini ahusiki kabisa na utoaji au ufanyaji wa malipo!

Jimbo4.png

Bila kujali signing arrangement ya hovyo kabisa kuwahi kuiona maishani mwangu, utaona wazi kwamba Mbunge hana ruhusa hata ya kutia pua kwenye hizo pesa!! Na ingawaje Ibara ya 22(5) inasema pesa itatolewa pale tu kutakapokuwa na muhtasari ambao bila shaka Mbunge anaweza kuwepo lakini bado muhtasari HAUWEZI kuzuia pesa kuibiwa!!!

Long version ya maelezo husika:
Ikumbukwe kwamba, pesa za uchocheaji wa maendeleo ya jimbo zinatumika kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Mfuko wa Uchocheaji wa Maendeleo ya Jimbo, Sura ya 96 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2015.

Awali ya yote, Ibara ya 7(1) ya sheria hiyo inasema kwamba "Kila mgao na malipo ya fedha kutoka Mfuko wa Uchocheaji wa Maendeleo ya Jimbo utahidhinishwa na kamati"

Aidha, ibara ndogo ya pili inasema inasema "malipo yote kutoka kwenye kamati yatafanyika kupitia akaunti ya jimbo"!

Jimbo1.png
Hivyo basi, kabla hatujaenda mbali utaona wazi kwamba pesa ni lazima iidhinishwe na kamati na inawekwa kwenye akaunti ya jimbo!!

Sasa tuone muundo wa hiyo kamati na uendeshaji wa akaunti ya jimbo kisha tutumie akili zetu tulizopewa na Mwenyezi Mungu kufahamu ni nani ana nafasi kubwa ya kutafuna hizo pesa kama kweli zimetafunwa!

Ibara ya 10(1) ya sheria husika inataja Wajumbe wa Kamati tajwa hapo juu, ambao ni:-
(a) Mbunge wa Kuchaguliwa, ambae ndie atakuwa Mwenyekiti wa Kamati
(b)Ofisa Mipango wa Wilaya ambae atakuwa Katibu wa Kamati,
(c)Madiwani wawili ambao watakuwa ni wakazi wa jimbo husika,
(d)Maafisa Watendaji wa Kata wawili, na
(e) Mtu mmoja kutoka kwenye NGO

Jimbo2.png

Kwahiyo hapo utaona, role ya kwanza ya mbunge wa kuchaguliwa ni kuwa Mwenyekiti wa Kamati!

Ibara ya 11 inaelezea Majukumu ya Kamati ambayo mwenyekiti wake ndo mbunge! Na kwenye majukumu hayo, hakuna HATA MOJA linalomfanya mbunge awe karibu na pesa za mfuko wa jimbo:-

Jimbo 3.png

Sasa tuje kwenye fedha yenyewe manake hapo juu tumeona pesa kutoka Mfuko wa Uchocheaji wa Maendeleo ya Jimbo inawekwa kwenye Akaunti ya Jimbo; kwa maana hiyo wanaoendesha akaunti husika ndio wana nafasi kubwa sana ya kula hiyo pesa!

Ibara ya 21(1) inasema Mkurugenzi wa Halmashauri atamteua Mweka Hazina kwa maandishi! Bila shaka sote tunafahamu kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri ni mtu wa serikali, na ndio hawa hawa wanaotumika kuhujumu upinzani wakati wa uchaguzi!!

Sasa unless uwe huna akili timamu ndipo unaweza kuamini kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri anaweza kumteua mtu wa upinzani kuwa Mweka Hazina!!

Aidha, Ibara ya 21 (2) inasema Council Director au Officer in Charge atakuwa ndie Accounting Officer!!

Kwa maana nyingine, hapo utaona ni nani anaanza kuwa karibu na pesa za mfuko wa jimbo!!

Ibara ya 22(2) inampa mamlaka Mkurugenzi kuteua benki ambayo anayotaka Akaunti ya Jimbo ifunguliwe... kwa maana nyingine, Mbunge hana hata nafasi ya kusema akaunti ifunguliwe benki ipi lakini wenye nafasi hiyo ni watu wa serikalini!!!

Sasa ndo hapo sasa...akaunti imeshafunguliwa kwenye benki iliyotakiwa na DED mwenyewe... Je, mfumo wa utoaji pesa unakuaje?! Swali hilo linajibiwa na Ibara ay 22 (3) (a &b) kwamba:-
- Saini 2 zitahitajika katika kufanya malipo au kutoa pesa, na katika saini 2 hizo, saini moja ni ya mtu kutoka Kundi A na nyingine kutoka Kundi B!
-Kundi A litaundwa na Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Afisa Mipango wa Halmashauri,
-Kundi B litaundwa na Mweka Hazina wa Halmashauri na Mhasibu wa Halmashauri!

Kwa mara nyingine, utaona wanaotia mikono kwenye hiyo pesa ni watu wa serikalini peke yao!!! Na kwa kuangalia ile signing arrangement iliyotajwa hapo juu, maana yake ni kwamba Mkurugenzi pamoja na Mweka Hazina au Mhasibu wanaweza kutoa pesa; au Afisa Mipango na Mweka Hazina au Mhasibu pia wanaweza kutoa pesa.

Mbunge kama mbunge, pamoja na kuwa ndie mwenyekiti wa kamati lakini ahusiki kabisa na utoaji au ufanyaji wa malipo!

Jimbo4.png

Bila kujali signing arrangement ya hovyo kabisa kuwahi kuiona maishani mwangu, utaona wazi kwamba Mbunge hana ruhusa hata ya kutia pua kwenye hizo pesa!! Na ingawaje Ibara ya 22(5) inasema pesa itatolewa pale tu kutakapokuwa na muhtasari ambao bila shaka Mbunge anaweza kuwepo lakini bado muhtasari HAUWEZI kuzuia pesa kuibiwa!!!
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,360
2,000
Ni jambo la ajabu na aibu kubwa kuwa na Rais anayesema uongo hadharani kuwataja wabunge hasa wa upinzani kuwa ndio wanakula pesa za mfuko wa jimbo wakati anafahamu kuwa sheria haina nafasi kwa mbunge kutumia pesa hizo.

Rais Magufuli kwa kweli hatufai kabisa maana amekuwa msema uongo bila hata aibu hadharani.

Kwa nini ni muongo hivi?
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,946
2,000
Umetumia nguvu kubwa sana kumtetea Halima Mdee!
Swali la kwanza: Kwa mfumo huo, huyo Halima anaibaje ibaje hizo pesa?

Swali la pili: Kama mkwamo wa Kawe unatokana na Halima kuiba pesa za jimbo, je mkwamo wa majimbo yanayoongozwa na CCM kwa miongo kadhaa hivi sasa unatokana na wizi unaofanywa na nani?!

Jibu hayo kwanza, kama huna; piga kimya coz' my style ni kujadili hoja!!!
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
35,684
2,000
Umetumia nguvu kubwa sana kumtetea Halima Mdee!

Ww unaishi ili ule na sio kinyume chake. Huyo kaweka wazi sheria zenu ccm zilivyo, na ww badala ya kuweka mipasho, ulipaswa kuweka vifungu vya sheria wazi vinavyoonyesha kuwa Halima/mbunge anaweza vipi kula hela za jimbo. Mara nyingi hiki kitendo cha watu kutokujua sheria, huwa kinatumika kama sehemu ya kupotosha umma. Wakati mwingine haya hufanyika kwa wahusika kujua au kutokujua sheria. Mimi binafsi nimeongeza elimu kwenye kile ninachokijua kuhusu mfuko wa jimbo.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
35,684
2,000
Rafiki yetu halima ni mwizi kabisa hata umtetee vipi, kibaya hata kuongea na rais au bungeni kuhusu kero za jimbo hajawahi zaidi ya matusi

Mbunge anaongelea mahitaji ya wananchi bungen na kwenye baraza la madiwani huko ndio proper channel, na Halina huwa anafanya hivyo. Unataka akaongee na rais mahitaji ya wananchi kwani yeye ni mweupe?
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
35,684
2,000
Ni jambo la ajabu na aibu kubwa kuwa na Rais anayesema uongo hadharani kuwataja wabunge hasa wa upinzani kuwa ndio wanakula pesa za mfuko wa jimbo wakati anafahamu kuwa sheria haina nafasi kwa mbunge kutumia pesa hizo.
Rais Magufuli kwa kweli hatufai kabisa maana amekuwa msema uongo bila hata aibu hadharani.
Kwa nini ni muongo hivi?

Kwa taarifa yako Magufuli hajuagi sheria bali ana ulevi wa madaraka, na vile katiba ni mbovu anafanya atakacho bila kuulizwa. Rejea siku aliyopokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha, huku jeshi likiwa limetengwa kabisa na siasa kikatiba. Nina uhakika wa 100% hajui sheria hii ya mfuko wa jimbo kama ilivyo ndio maana anaishia kuongea vitu vya aibu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom