masdinero masproblemas
JF-Expert Member
- Mar 19, 2022
- 224
- 178
Kuna vituko sana lakini hakuna zaidi ya ujinga wetu binadamu.Bila Wakaidi na Wapingaji tungekuwa hatuna maendeleo huku tukiishi kwenye sayari yetu ambayo ni tambalale na jua linaizunguka....
Na wala tusingehoji wala kutafuta / kujua mazingira yetu ili tupambane nayo sababu tungekuwa tunakengeuka kama waliotaka kujenga mnara wa Babeli (Na bila hao kutaka kujenga huo Mnara huenda hizi lugha tofauti zingekuwa hazipo)
Hence binafsi ninapenda uwepo wa hao so called wakaidi
Kusema hayupo hakufanyi asiwepo.
Hayupo kwa sababu hayupo
Wapi nimesema hivyo?Huwezi kusema watu wanaohoji ni wajinga... utakuwa una mtanzo kinyume na uhalisia wa mambo!
Nilijua lazima kwenye huu uzi uwepo.Thibitisha Mungu yupo, na kwamba hizo habari za kuwepo kwa Mungu si hadithi za kusadikika zilizotungwa na watu tu.
Twende pointi moja bada ya nyingine katika uthibitisho wako.
Unajua kama mungu yupo?Eti mtu anakwambia, katika plane Euclidean geometry:
Duara lina nyuzi 360.
Pembetatu ina nyuzi 180.
Hivyo, pembetatu haiwezi kuwa duara, na duara haliwezi kuwa pembetatu.
Halafu, anakwambia kuna duara moja special ambalo hapohapo ni pembetatu.
Anataka ukubali tu.
Ukikataa, unaitwa mkaidi.
Wewe siku ya kiama ni moto tuuuNakwambia hivi, hata kama mimi sipo.
Bado hujathibitisha Mungu yupo.
Na huwezi kuthibitisha Mungu yupo.
Kwa sababu hayupo.
Mungu yupi? Kwa msingi upi? Kwa chanzo kipi? Mungu huyo anataka nn? Ana msaada gani?Unajua kama mungu yupo?
Ametoka wapi? Anaenda wap? Thibitisha kwa maelezo ya kina.Mungu yupi? Kwa msingi upi? Kwa chanzo kipi? Mungu huyo anataka nn? Ana msaada gani?
Uwe unasoma kijana, aya ya 53 katika sura ya 20 ni hii :Quran haiwez kutumika kam reference ya uhakika
mfano mungu wenu naona alijichanganya au alisahau jinsi alivyoiumba dunia
20:53 - tunaambiwa dunia iko kama carpet
79:30- tunaambiwa dunia Ina umbo la yai la mbuni
Inakuaje muumbaji wa dunia anashindwa kutambua umbo sahihi anajichanganya namna hii
Naomba unionyeshe inavyo jipinga yenyewe.Kwanza kabisa, dhana ya kuwapo Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote, inajipinga yenyewe kabla mtu yeyote hajaipinga.
Wengine wanaonesha tu dhana inavyojipinga yenyewe.
Unaelewa hilo?
Hii haiwezi kuwa sababu. Sasa sisi tutakuuliza umejuaje kama hayupo ? Kwenye jibu la swali hili ndiyo kuna sababu ila hiyo uliyodai si sababu kiuhalisia bali ni mpangilio mwepesi wa sentensi isiyo kamili, yaani hiyo ni sehemu ya sentensi yenye kuihitaji kielezi kufidisha sentensi kamili au ili iwe kamili.Hayupo kwa sababu hayupo.
Kingine hii si dhana bali ni uhalisia, dhana unasema wewe kutokana na uchachefu wako wa maarifa juu ya jambo hili.Na hili utaliona kwa kuangalia logical inconsistencies na self contradiction katika dhana ya uwepo wake.
Huu mfano si sahihi, sababu unalinganisha vitu viwili visivyo lingana wala kukaribiana. Una tatizo kubwa la kulinganisha mambo.Uwepo wa Mungu huyo ni sawa na mtu akuambie kwamba kuna duara ambalo hapo hapo ni mraba katika plane Euclidean geometry.
Naomba uthibitishe ya kuwa hizi ni stori tu za watu.Hakuna kitu hicho, ni stories tu za watu.
Kama Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, hawezi kuachia viumbe wake aliowaumba mwenyewe katika dunia yake mwenyewe wachomwe moto.
Duuuu umeongea fact tupu Hawa wajinga hudhani Dunia ni special sana na hizo nadharia za Mungu hubase hapa hapa tu Sasa unajiuliza kama huyo Mungu wao yupo Ndio ashindwe kujua formula za ulimwengu zilivyo Mpaka atoe hekayq za kijuha kwenye maandiko aliyoshisha yeye (according to Qureshian mythology/Islam)Kuna vituko sana lakini hakuna zaidi ya ujinga wetu binadamu.
Yaan kama sio wachache kuhoji na kukataa kushikiwa akili dunia ingekuwa bado ndio katikati ya ulimwengu. Kila kitu kinazunguka sayari hii maalum, na sisi wanadamu ndio tungekuwa tumeekewa vitu vyote(sayari za kila aina gesi na jiwe, nyota za kila aina, mawingu yanayozaa nyota, miundo mbalimbali ya vikundi vya nyota n.k) ulimwenguni. Ili tu kuwaaminisha na kushangaza viumbe binadamu uwezo wa mwenyezi mungu. Lengo tuabudu huyo mungu. Mambo yote mwisho ibada!
Lakin wap... sayari yetu ni ndogo, ya kawaida mno. Jua letu nyota kubwa kiasi, isiyo na maajabu yeyote. Mtaa wetu wa nyota umedorora, hamna matukio yoyote makubwa ya kiulimwengu yanayotokea au kuendelea ukitoa kijamii chetu kinachojiita cha pekee. Knachodai kuumbwa na muumbaji wa ulimwengu wote unaotuzunguka sisi(sio kweli). Kwa ajili tu ya kumpunguzia upweke na kumuabudu huyo mungu. Baadae auangamize na wachache wachaguliwe kuendelea na huo utumwa milele kwake, kusikojulikana. Hakuna anayepajua.
Ujinga mtupu!