Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi - 2

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi - 2

Unakubali kuna "Infinity Series" kwa akili yako tu ya kawaida ? Kama ipo naomba ututhibitishie.

Uhalisia unaonyesha wazi kabisa lazima kuwe na chanzo na ukomo.
Ulimwengu ndio chanzo na ndio ukomo
 
Unakubali kuna "Infinity Series" kwa akili yako tu ya kawaida ? Kama ipo naomba ututhibitishie.

Uhalisia unaonyesha wazi kabisa lazima kuwe na chanzo na ukomo.
Namba chanzo chake ni namba ngapi na mwisho wake ni namba ngapi?
 
Watakwambia Hana mwanzo Wala mwisho na hapo hapo ukiwaambia Hata Ulimwengu haukuumbwa na Hauna mwanzo Wala mwisho wanapinga wanasema haiwezekani
(Contradiction)
Wewe usipate tabu, tuthibitishie ya kuwa Ulimwengu haukuumbwa na hauna mwanzo wala mwosho, kisha uonyeshe kutokuwa na mwanzo kwake kupoje ?
 
Onyesha hilo, na utuambie ilikuwaje ulimwengu ukawa hivi ulivyo.

Mtoa mada amejitahidi sana kuwaonyesha, lakini sababu hamufikirii, ndiyo hivyo tena.
Wewe ndio unabidi uonyeshe haiwezekani kwa kuthibitisha ulimwengu sio chanzo
 
Jibu swali nililo kuuliza.

Vyote vimetoka kwa Allah mlezi, baada ya kumuumba Adamu alimfunza majina ya kila kitu.
Thibitisha Allah yupo kweli, na kwamba habari zake si hadithi tupu za watu tu.
 
Kazi yangu nimeshamaliza.

Shukrani.
Hujathibitisha Allah yupo kweli na habari zake si hadithi za watu tu.

Thibitisha Allah yupo kweli, na kwamba habari zake si hadithi tupu za watu tu.
 
Hujathibitisha Allah yupo kweli na habari zake si hadithi za watu tu.

Thibitisha Allah yupo kweli, na kwamba habari zake si hadithi tupu za watu tu.
Nithibitishe mara ngapi ? Hivi kati yangu mimi na wewe mwenye uwezo wa kuthibitisha jambo hili kielimu ?

Nimekukosoa mara ngapi juu ya ukanushaji wako wa kibubusa kwa kutumia "Logic" ? Umekimbia mara ngapi maswali yangu rahisi sana ?

Sasa mwisho wa siku naona hakina haja ya kujadili jambo hili na watu wajinga, watu ambao hawamjui Mola lakini wanamkanushia, watu ambao wanakimbia maswali ? Watu ambao wanaona si jukumu lao kuthibitisha.

Kwa upande wangu kazi yangu nimemaliza, ukijibu swali langu, nitakuja kuendelea hapa nilipo ishia.

Shukrani.
 
Ahsante kwa swali zuri, kwa waliosoma sifa za MUNGU wa imani zenye chimbuko la NABII IBRAHIM au ABRAHAM ambao ni WAKRISTO, WAISLAMU na WAYAHUDI wanafahamu wazi kwamba hili swali ni INVALID - ILLEGITIMATE, kwa nini? kwa kwa sababu MUNGU wao haelezeki kwa muda, MUNGU wetu ni wa mwanzo "alpha = al awwal" na wa mwisho "omega = al akhir", hana mwanzo wala mwisho, ushauri: soma sana majina na sifa za MUNGU: maswali mengi sana ya aina hiyo yanajibika

Ziada: fahamu kwamba vipawa vya mwanadamu havitoshelezi kumuelewa na kumtambua MWENYEZI MUNGU kwa 100%, je ni kwa nini? ni kwa sababu utashi tuliopewa wanadamu una ukomo katika baadhi ya mambo na hususani mambo ya imani, naamini wengi wetu tunajua nini maana ya imani, hivyo kwa upeo wetu wenye kikomo, imani zetu haba na ukosefu wa maarifa sahihi na ya kutosha baadhi ya mambo kamwe hutoweza kuyachambua kwa akili yako na ukapata clue, fahamu hilo na liweke akilini

Uliyeuliza hilo swali, yaonyesha unaifahamu sana nadharia ya muda, naomba nielezee nadharia ya "muda kwa mapana yake" tafadhali na hakikisha naelewa kwa 100%, ahsante
Kwa hiyo unakubali kila kitu kiliumbwa!
Ila ukija kwa Mungu chanzo chake unakubali alikuwepo tu bila muumbaji wake!?
 
Nithibitishe mara ngapi ? Hivi kati yangu mimi na wewe mwenye uwezo wa kuthibitisha jambo hili kielimu ?

Nimekukosoa mara ngapi juu ya ukanushaji wako wa kibubusa kwa kutumia "Logic" ? Umekimbia mara ngapi maswali yangu rahisi sana ?

Sasa mwisho wa siku naona hakina haja ya kujadili jambo hili na watu wajinga, watu ambao hawamjui Mola lakini wanamkanushia, watu ambao wanakimbia maswali ? Watu ambao wanaona si jukumu lao kuthibitisha.

Kwa upande wangu kazi yangu nimemaliza, ukijibu swali langu, nitakuja kuendelea hapa nilipo ishia.

Shukrani.
Weka post namba ya ulipothibitisha Allah yupo
 
Wanaopinga uwepo wa Mungu, ukiwauliza kuhusu asili ya huu ulimwengu na jinsi ulivyo katika mpangilio ambao hauna dosari ndani yake, watakwambia ni nature au coincidence.

Mimi mtu akinambia hivi swali la kwanza linalokuja akilini mwangu, ni je, hiyo nature inaakili(ufahamu)?.

Kinacho mpambanua mwanaadamu, na kumuwezesha kufanya mambo yake kwa mpangilio ni akili yake, hata wanyama nao wanaufahamu hatakama tutasema hawana akili ndio maana na wao kuna mambo wanayafanya kwa mpangilio.

Hivyo jambo/kitu chochote kuwa katika mpangilio kunalazimu uwepo wa kilicho sababisha huo mpangilio, ambapo kwa mambo ya mwanaadamu ni yeye mwenyewe kwa sababu anaakili, na anaevuruga mambo huyo ni chizi(hana akili).

Ndio maana ninauliza je hiyo nature inaakili?

Kwa sababu mpangilio huu wa ulimwengu uliokamilika na usio na dosari, unalazimu uwepo wa akili yenye ujuzi iliyotumika kuweka kila jambo katika mpangilio.

Na kama nature haina akili basi ingelazimu huu ulimwengu kutokuwa katika mpangilio uliokamilika na usio na dosari.

Labda utasema huu mpangilio ni coincidence, ok.

Kwani coincidence ni nini?
Wanasema coincidence of events is the appearance of a meaningful connection when there is none.

Hivyo ni kama kitendo cha kunguru kumnyea mwanaadamu, unaweza ukadhani alikusudia lakini kumbe ni coincidence tu.

Lakini unaonaje mtu akija kukuambia, bwana kila nikipita sehemu fulani kwenda kazini siku fulani, kuna kunguru huja kininyea kichwani.
Kunguru ni yuleyule, sehemu ile ile, Kila akienda kazini, na sehemu anayomnyea ni ile ile.

Asee, atakayekwambia hiyo ni coincidence atakuwa na matatizo ya akili, huyo kunguru ima anaakili ya binadamu au katumwa ndio maana hakosei.

Hivyo coincidence hailazimu kwa huu ulimwengu kuwa na mpangilio uliokamilika na usio na mapungufu yeyote, Bali kama ingekuwa hivyo basi ingetakiwa mambo yawe randomly.

Wote tunafahamu jinsi wanasayansi walivyofanya uvumbuzi wa mambo mbalimbali kuhusu huu ulimwengu, na wametuelimisha jinsi huu ulimwengu ulivyokuwa katika mpangilio usio kuwa na dosari yeyote wala kuingiliana.

The solar system, the internal and external processes of the Earth, na jinsi zinavyofanyika kwa mpangilio.

Na tuache huu mpangilio wa ulimwengu sisi wanaadamu wenyewe tukijiangalia, tunaona jinsi miili yetu ilivyokaa kimpangilio na kufanya kazi kwa mpangilio, na tunajua hatujajiumba wenyewe bali tumeumbwa.

Hivyo kama mtu anasema ni nature basi hiyo nature itakuwa inaakili maana sio kwa kujipangilia huku tuseme ni coincidence.

Wakana Mungu wanasema haya yametokana na nature, basi kama wanasema hivyo itakuwa hiyo nature inaakili na ndio mungu wao, maana wameipa sifa ya uungu, kwa kusema ndio chanzo cha ulimwengu na ndio iliyowaumba, hata kama hawaiabudu au haina dhati.

Maana kwetu sisi waislamu aliyeuumba huu ulimwengu na vilivyomo ndiye tunayemuita Mwenyezimungu (Allah subhaanahu wataa'la) na kumuabudu.

Atakwambia ndio ulimwengu upo katika mpangilio lakini huo sio uthibitisho kwamba mungu yupo............... Umesema kweli kabisa ewe mkana mungu.

Ndio mpangilio wa ulimwengu sio uthibitisho kuwa mungu yupo bali ni alama/ishara ya kwamba kuna aliyeuweka huu mpangilio, na huyo ndiye aliye uumba huu ulimwengu.

Hivyo mwenye akili anakili na kukubali kuwa huu ulimwengu kuna aliyeuweka katika huu mpangilio na anayesema huu ulimwengu umetokea tu basi huyo ni mkaidi tu, na analeta kiburi, ilhali unajua kuwa hiwezekani jambo kama hilo.

Atakuambia thibitisha kama mungu yupo?

Sasa wewe ilikuwaje mpaka ukaconclude kwamba mungu hayupo? halafu hapo hapo hujui ilikuwaje huu ulimwengu upo katika huu mpangilio?

Umezaliwa umeukuta na utakufa utauacha, na ulipozaliwa habari za uwepo wa mungu umezikuta, umeambiwa mungu ndiye aliyeumba huu ulimwengu, ukakanusha ilhali aliye uumba humjui.

Jamani niacheni niendelee kuwaita hawa watu wakaidi.
Anayempinga Mungu atakuwa hana akili timamu
 
Unajuaje kwamba ni lazima iwe finite?

Unaelewa mambo yote ya ulimwengu?

Unaelewa Einstein's relativity?

Unaelewa Dirac's equations za quantum physics? Unaelewa hesabu za kureconcile quantum physics na relativity?

Unaelewa Schrodinger's Cats experiment na implication yake?

Unaelewa double slit experiment na implications zake?

Unaelewa spooky action at a distance na implications zake?

Unaelewa time dilation na implications zake?

Halafu, hata kama kweli process ni finite, hilo halithibitishi chanzo ni Mungu.

Hilo linathibitisha process ni finite.

Process kuwa finite si lazima maana yake inaanzia kwa Mungu.
Sifahamu kila kitu, lakini namshukuru THE ALMIGHTY kwa aliyonijaalia kuyafahamu , ideas za physics ulizowasilisha nyingi si ngeni kwangu, na sijajua umeziwasilisha kwa lengo gani, nyingi hazina mafungamano ya moja kwa moja na mada husika, unahisi zitanitisha au lengo lilikuwa nini haswa?

Swali la kwanza ambalo ndilo nililokuwa nalitolea maelezo kwenye post zangu umeuliza kisha ukalijibu mwenyewe kwenye maelezo yako mwishoni, ahsante kwa msaada, hapa ambacho naweza kukifanya ni kuthibitisha persuasively comment yako ya mwisho, lakini kwa sharti kuu moja, naomba anza wewe kunithibitishia unachopinga kisha mimi nitafuatia, mwenye upeo wa kupambanua mambo atajua zipi ni mbichi na zipi ni mbivu, kwenye nukta ya mwisho unapokuwa unathibitisha hakikisha unaeleza kwa uwazi na siyo mazingaombwe, kubisha ni sanaa nyepesi sana, kuthibitisha ndo huwa kimbembe, karibu.

Ahsante.
 
Wadau mnaandika kwa vidole vya miguu nini? mna speed ya F1
 
Kama tuna mapengo mengi katika ujuzi wetu, hatutakiwi kuwa na kauli za ku conclude kwamba ulimwengu ni lazima uwe na chanzo finite au infinite bila hata kuweka hedge ya framework gani tunayozungumzia.

Mathalani, wanafizikia wanaongelea kuhusu model ya big bang, na kwa mujibubm wao, wameshindwa kujua kilichotokea katika singularity ya big bang ni nini, wanahitaji hesabu mpya kwa model hiyo.

Wengine wanasema kila kitu kilianza katika big bang.

Wengine wanasema big bang yetu ni moja tu katika series za big bang na big crunch zisizo na mwisho.

Wengine wanasema big bang yetu ni moja tu kati ya big bangs nyingi zilizozaa universes nyingi katika multiverse.

Hatujui mengi, tuchunguze tujue. Hizi habari za kukaa na kufikiri na ku deduce tu ndiyo zilimfanya Aristotle aipotoshe dunia kwa karibu miaka 2000, mpaka Galileo alivyotufumbua macho.

Kama unajua chochote kuhusu quantum physics, utajua kwamba kuna mengi sana kuhusu reality hatuyajui. Inatubidi tujifunze sana kuyajua.

Kauli yako ya kwamba ni lazima ulimwengu uwe una chanzo finite, kwa kutumia uzoefu wako wa maisha ya kila siku, ni sawa na mtu kusema ni lazima dunia ni bapa na si tufe, kwa sababu akikaa kibarazani kwake anaona dunia ni bapa na si tufe.

Hizo concepts zote za physics ninekupa kwa sababu zina challenge conventional thinking.

Kuanzia kitu kuwa sehemu moja kwa wakati mmoja, mpaka concept nzima ya cause and effect na nature of time.

In quantum physics, the effect can happen before the cause in an infinite quantum loop.

So, if you don't know all about quantum physics - don't feel bad, no one does- how do you know that the universe/ multiverse has no finite beginning and it exist in a bounded but infinite quantum loop?

Kuhusu "The Almighty", thibitisha kwamba yupo kweli na habari zake si hadithi za watu tu.
 
Kwa hiyo unakubali kila kitu kiliumbwa!
Ila ukija kwa Mungu chanzo chake unakubali alikuwepo tu bila muumbaji wake!?
Tafiti juu ya sifa za UUNGU 'CREATOR' na sifa za CREATION, utajifunza kwamba MUNGU wa ABRAHAMIC RELIGIONS yeye alikuwepo na hakuumbwa - eternal, ama kwa MUNGU aina ya ng'ombe au jiwe basi ni lazima awepo muumbaji wake kama ulivyoandika, vyote hivyo ni material 'matter', kinachomtofautisha yeye na vingine vyote ni sifa zake tu
 
At least kwa Mungu ng'ombe tunaweza tukathibitisha uwepo wake

Mungu wako tunawezaje kumthibitisha?
 
Back
Top Bottom