Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi - 2

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi - 2

Hujathibitisha kwamba huyu Mungu yupo kweli, na habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu.
Challenge umegoma ku-accept, endelea kuabudu nadharia za wanazifikia na wanafalsafa ambao baadhi yao ni waumini wa imani mbalimbali, na ambao wengi wao mwisho walishuhudilia kweli MUNGU yupo, kazi kwako, kila la kheri
 
Challenge umegoma ku-accept, endelea kuabudu nadharia za wanazifikia na wanafalsafa ambao baadhi yao ni waumini wa imani mbalimbali hahahaha, na ambao wengi wao mwisho walishuhudilia kweli MUNGU yupo, kazi kwako, kila la kheri
Your challenge is a logical non sequitur.

Do you know what that is?

Hujathibitisha kwamba huyu Mungu yupo kweli, na habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu.
 
Umeandika mengi lakini hujathibitisha Mungu yupo.

Naona umekuja kutetea upande wako emotionally, unalazimisha supernatural divine ambayo hata huwezi kuieleza ni nini.
Siwezi kuielezea? ALLAH MUSTA'AN, sijataka kueleza moja kwa moja wala kujikita huko delibarately, sicho ambacho tulikuwa tunajadiliana mimi na wewe, mada yetu ilikuwa "je ulimwengu ni finite au infinite?" Acha kuibua mambo na kuwatengenezea watu notion kwamba kuna kitu sijakieleza, maelezo yangu yalijikita kwenye kufafanua maelezo yako, sikuwa na shabaha ya kuthibitisha uwepo wa MUNGU, ningeamua ningefanya hilo, hivi unajua ni wanafizikia vinara wangapi au wanafalsafa vigogo wangapi waliothibitisha kuwepo kwa SPIRIT kwa nadharia za origin of universe, hii nadharia hamna ATHEIST hata mmoja anayeweza kusimama kwa hoja dhidi ya THEIST
 
Siwezi kuielezea? hahahaha, ALLAH MUSTA'AN, sijataka kueleza kwa kusudi, sicho ambacho tulikuwa tunajadiliana mimi na wewe, mada yetu ilikuwa "je ulimwengu ni finite au infinite?" Acha kujitekenya na kucheka mwenyewe kwa kuwatengenezea watu notion kwamba kuna kitu sijakieleza, maelezo yangu yalijikita kwenye kufafanua maelezo yako, sikuwa na shabaha ya kuthibitisha uwepo wa MUNGU, ningeamua ningefanya hilo, hivi unajua ni wanafizikia vinara wangapi au wanafalsafa vigogo wangapi waliothibitisha kuwepo kwa SPIRIT kwa nadharia za origin of universe, hii nadharia hamna ATHEIST hata mmoja anayeweza kusimama kwa hoja zenye dhidi ya THEOLOGIST
Hujathibitisha kwamba huyu Mungu yupo kweli, na habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu.

Huyo character uliyemtaja Allah kajaa contradictions zinazoonesha katungwa na watu tu, hayupo nje ya hadithi.

Bisha.
 
Your challenge is a logical non sequitur.

Do you know what that is?

Hujathibitisha kwamba huyu Mungu yupo kweli, na habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu.
Unanionaje we jamaa? Yaani hicho ndo umeona cha kuniuliza? Kufupisha tu ni kwamba: Hoja karibu zote zinazotumiwa na ATHEIST kupinga UUNGU nazifahamu, na pia naweza kuzisambaratisha

You flip like reciprocal, Quantum Physics imekushinda unakimbilia kwenye Logic - Elimu ya Mantiki "logical non ... ...", unaona ni idea kubwa sana e? Hata hukohuko kwenye mantiki kwa kukariri kwako na hutokujua kujenga hoja naweza kukuangusha vilevile

Hii comment yangu ya mwisho kwako, challenge nilizoweka hujaaccept, nayouliza hujibu, nilivyoeleza umeshindwa kuvitolea ufafanuzi wala kukosoa, badala yake umekimbia kwenye jambo ambalo ilitakiwa uaccept challenge yangu ndo lijadiliwe, ni hivi, sina haja na mtu mwenye pigo za aina hiyo aisee

 
Unanionaje we jamaa? Yaani hicho ndo umeona cha kuniuliza? Kufupisha tu ni kwamba: Hoja karibu zote zinazotumiwa na ATHEIST kupinga UUNGU nazifafamu, na pia naweza kusimbaratisha

You flip like reciprocal, QUANTUM PHYSICS imekushinda unakimbilia kwenye LOGIC - ELIMU YA MANTIKI "logical non blah blah", unaona ni idea kubwa sana e? Hata hukohuko kwenye mantiki kwa kukariri kwako na hutokujua kujenga hoja naweza kukuangusha vilevile

Hii comment yangu ya mwisho kwako, challenge nilizoweka hujaaccept, nayouliza hujibu, nilivyoeleza umeshindwa kuvitolea ufafanuzi wala kukosoa, badala yake umekimbia kwenye jambo ambalo ilitakiwa uaccept challenge yangu ndo lijadiliwe, ni hivi, sina haja na mtu mwenye pigo za aina hiyo aisee

Nimekuuliza "do you know what a logical non sequitur is?".

Hujajibu.

Does that mean you do not know what that is?
 
Hujathibitisha kwamba huyu Mungu yupo kweli, na habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu.

Huyo character uliyemtaja Allah kajaa contradictions zinazoonesha katungwa na watu tu, hayupo nje ya hadithi.

Bisha.

We jamaa bana, hivi unapo-reason issues huwa unazunguka 3 SIXTY "360" au huwa unakurupukia upande mmoja tu?

Hiyo uliyojenga si hoja, ungeanza kwa kuhoji hivi hizi habari za kupinga uwepo wa Mungu si za kutungwa na watu tu? Ukimaliza ndo uhamie dimension nyingine mfano hiyo uliyoandika hapo, lakini kwa kuwa unapinga ili upate umaarufu sawa, mimi ngoja nikuache
 
We jamaa bana, hivi unapo-reason issues huwa unazunguka 3 SIXTY "360" au huwa unakurupukia upande mmoja tu?

Hiyo uliyojenga si hoja, ungeanza kwa kuhoji hivi hizi habari za kupinga uwepo wa Mungu si za kutungwa na watu tu? Ukimaliza ndo uhamie dimension nyingine mfano hiyo uliyoandika hapo, lakini kwa kuwa unapinga ili upate umaarufu sawa, mimi ngoja nikuache
Hujathibitisha kwamba huyu Mungu yupo kweli, na habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu.

Huyo character uliyemtaja Allah kajaa contradictions zinazoonesha katungwa na watu tu, hayupo nje ya hadithi.

Bisha.
 
Nimekuuliza "do you know what a logical non sequitur is?".

Hujajibu.

Does that mean you do not know what that is?
Unajua unachokifanya kweli? mimi nimeuliza maswali mangapi kwenye maelezo yangu hujajibu?

Sijatoa challenge pia, umeikubali?

Wakati mwingine
 
Naomba niwie radhi kama kwenye maelezo yangu kuna sehemu nitakuwa nimeteleza nikakukwaza kwa namna moja au nyingine
 
Unajua unachokifanya kweli? mimi nimeuliza maswali mangapi kwenye maelezo yangu hujajibu?

Sijatoa challenge pia, umeikubali?

Wakati mwingine
Nimekuuliza "do you know what a logical non sequitur is?".

Hujajibu.

Does that mean you do not know what that is?

Hiyo unayoiita challenge ni matokeo ya utapiamlo wako wa ubongo katika kufikiri kimantiki.

Hujui kufikiri kimantiki.

Unatoa logical non sequitur kama challenge.

Lakini, sitegemei ujue hilo.

Kwa sababu unaonekana hujui hata logical non sequitur ni nini.
 
Mungu hakuna au hakuna uthibitisho wa kuwepo kwake? Maana atheists wanadai hakuna Mungu ila ukweli ama uongo wa madai yao hutegemea wanaoamini kuwepo Mungu.
 
siwezi Fanya Huo ujinga unaodai nifanye Ili Hali hata wewe nikikuambia inioneshe ushahidi juu ya Mungu kuumba Ulimwengu na chanzo Cha huyo Mungu utakuja na porojo tu!
Of course, ni vigumu pia kuonyesha kutokuonekana kwa TV inchi 52, na hela kama shs 2m sebuleni, pamoja na kuvunjwa kwa mlango mkubwa, kuwa kumesababishwa na MTU. Kuna uwezekano kuwa vime evaporate hewani au labda nyani waliingia wakavibeba, au aliens fulani wameshuka wakaiba, au sumaku kubwa ilivinyonya, etc.
 
Wanaopinga uwepo wa Mungu, ukiwauliza kuhusu asili ya huu ulimwengu na jinsi ulivyo katika mpangilio ambao hauna dosari ndani yake, watakwambia ni nature au coincidence.

Mimi mtu akinambia hivi swali la kwanza linalokuja akilini mwangu, ni je, hiyo nature inaakili(ufahamu)?.

Kinacho mpambanua mwanaadamu, na kumuwezesha kufanya mambo yake kwa mpangilio ni akili yake, hata wanyama nao wanaufahamu hatakama tutasema hawana akili ndio maana na wao kuna mambo wanayafanya kwa mpangilio.

Hivyo jambo/kitu chochote kuwa katika mpangilio kunalazimu uwepo wa kilicho sababisha huo mpangilio, ambapo kwa mambo ya mwanaadamu ni yeye mwenyewe kwa sababu anaakili, na anaevuruga mambo huyo ni chizi(hana akili).

Ndio maana ninauliza je hiyo nature inaakili?

Kwa sababu mpangilio huu wa ulimwengu uliokamilika na usio na dosari, unalazimu uwepo wa akili yenye ujuzi iliyotumika kuweka kila jambo katika mpangilio.

Na kama nature haina akili basi ingelazimu huu ulimwengu kutokuwa katika mpangilio uliokamilika na usio na dosari.

Labda utasema huu mpangilio ni coincidence, ok.

Kwani coincidence ni nini?
Wanasema coincidence of events is the appearance of a meaningful connection when there is none.

Hivyo ni kama kitendo cha kunguru kumnyea mwanaadamu, unaweza ukadhani alikusudia lakini kumbe ni coincidence tu.

Lakini unaonaje mtu akija kukuambia, bwana kila nikipita sehemu fulani kwenda kazini siku fulani, kuna kunguru huja kininyea kichwani.
Kunguru ni yuleyule, sehemu ile ile, Kila akienda kazini, na sehemu anayomnyea ni ile ile.

Asee, atakayekwambia hiyo ni coincidence atakuwa na matatizo ya akili, huyo kunguru ima anaakili ya binadamu au katumwa ndio maana hakosei.

Hivyo coincidence hailazimu kwa huu ulimwengu kuwa na mpangilio uliokamilika na usio na mapungufu yeyote, Bali kama ingekuwa hivyo basi ingetakiwa mambo yawe randomly.

Wote tunafahamu jinsi wanasayansi walivyofanya uvumbuzi wa mambo mbalimbali kuhusu huu ulimwengu, na wametuelimisha jinsi huu ulimwengu ulivyokuwa katika mpangilio usio kuwa na dosari yeyote wala kuingiliana.

The solar system, the internal and external processes of the Earth, na jinsi zinavyofanyika kwa mpangilio.

Na tuache huu mpangilio wa ulimwengu sisi wanaadamu wenyewe tukijiangalia, tunaona jinsi miili yetu ilivyokaa kimpangilio na kufanya kazi kwa mpangilio, na tunajua hatujajiumba wenyewe bali tumeumbwa.

Hivyo kama mtu anasema ni nature basi hiyo nature itakuwa inaakili maana sio kwa kujipangilia huku tuseme ni coincidence.

Wakana Mungu wanasema haya yametokana na nature, basi kama wanasema hivyo itakuwa hiyo nature inaakili na ndio mungu wao, maana wameipa sifa ya uungu, kwa kusema ndio chanzo cha ulimwengu na ndio iliyowaumba, hata kama hawaiabudu au haina dhati.

Maana kwetu sisi waislamu aliyeuumba huu ulimwengu na vilivyomo ndiye tunayemuita Mwenyezimungu (Allah subhaanahu wataa'la) na kumuabudu.

Atakwambia ndio ulimwengu upo katika mpangilio lakini huo sio uthibitisho kwamba mungu yupo............... Umesema kweli kabisa ewe mkana mungu.

Ndio mpangilio wa ulimwengu sio uthibitisho kuwa mungu yupo bali ni alama/ishara ya kwamba kuna aliyeuweka huu mpangilio, na huyo ndiye aliye uumba huu ulimwengu.

Hivyo mwenye akili anakili na kukubali kuwa huu ulimwengu kuna aliyeuweka katika huu mpangilio na anayesema huu ulimwengu umetokea tu basi huyo ni mkaidi tu, na analeta kiburi, ilhali unajua kuwa hiwezekani jambo kama hilo.

Atakuambia thibitisha kama mungu yupo?

Sasa wewe ilikuwaje mpaka ukaconclude kwamba mungu hayupo? halafu hapo hapo hujui ilikuwaje huu ulimwengu upo katika huu mpangilio?

Umezaliwa umeukuta na utakufa utauacha, na ulipozaliwa habari za uwepo wa mungu umezikuta, umeambiwa mungu ndiye aliyeumba huu ulimwengu, ukakanusha ilhali aliye uumba humjui.

Jamani niacheni niendelee kuwaita hawa watu wakaidi.

===
Iliyotangulia soma Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Muendelezo soma Wanaopinga uwepo wa mungu ni.....-3
Wao siyo wakaidi! ndivo walivyo ni sahihi kuwa ivo!!...... sasa km Mungu amewafunga ufahamu je?? hawasaidii kumuona hawatamjua kamwe!hata hao walioko kanisani wengine hawamjui pyuuuu!

ni sawa na mie eti nikwambie baba yangu Msonjo sijui nyarusare ambaye simjui inakuja kweli? hata kma namjua lkn mwingine hamjui!.......dunia ni ya viumbe vyote!...wasio mjua na wanao mjua....Mfano cain, Esau hao swana vizazi vyao vingi sana humu Duniani!
 
Wanapinga kwa ushahidi wa sayansi. Lakini wameshindwa kuelewa kwamba sayansi haina majibu kwa KILA kitu. Hadi SAsa sayansi imeweza kujibu asilimia 10 tu ya mambo yote duniani. Bado sayansi ni asilimia 10 tu elimu mbalimbali zilizopo duniani zenye uwezo wa kujibu maswali ambayo sayansi imeshindwa kutupa majibu.
Mfano sayansi imeshindwa kutupa majibu kuhusu Roho, Ndoto, mawazo, nguvu ya imani, viumbe visiovyoonekana, nk
 
Back
Top Bottom