Ni miezi michache tu tangu bibi yetu achukue kijiti hiki.Mwanzoni alionekana kukubalika saana hasa na wapinzani na wenye mlengo tofauti na aliye kuwa rais wakati huo.
Lakini hali imebadilika ghafla na kila mmoja wetu ana hofu nna mashaka juu ya hatima ya kesho.
Wengine wanajaribu hadi kumpinga hadharani nawengine wapo wanapinga chini kwa chini.
Nchi sio kisiwa cha amani tena,ni majuto,na tozo kubwa kubwa,sambamba na kutishiwa kuhama nchi ambayo kimsingi sisi ndo wenyenayo
Najaribu kufikiria na kuchambua hoja mbalimbali za kwanini mambo yanabadilika na kuzidi kuharibika kila uchwao?
Je,ni legacy ya JPM bado imo kichwani mwa wa tz walio wengi??
Je,ni kivuli/remote inayo m control Rais Samia?
Je, Ni usaliti na kampeni mbaya zidi yake ndani ya serikali yake?
Je,kuna watu wanamasilahi juu ya haya anayoyafanya?
Ama pengine hali ipo sawa,tofauti na fikra za wengi?
Karibu tujadili hili kwa manufaa ya wengi hasa hasa wale tuliopigwa na kitu kizito!
#magema jr
#uvccm taifa