Ibrahim K. Chiki
JF-Expert Member
- Apr 5, 2011
- 594
- 163
Duh, naona hoja ambayo ni intellectual argument ni mbili
1. inayohusiana na gharama za kuendesha kesi katika mahakama ya kadhi!
2. Waanzishe waislamu pekee
Majibu:
1. Gharama za kuendesha kesi hizo ni vema zitoke serikalini kwakuwa kadhi courts itakuwa pia imepunguza kwa kiasi kikubwa kesi za waislamu zinazofanywa na mahakama za serikali (inabidi tufanye calculation ili tupate kiasi hasa ni kesi ngapi za waislamu kwa sasa zipo mahakamani ambazo zinatakiwa kupelekwa kadhi courts na gharam yake ni shilingi ngapi each case..tukipata tuna transfer kiasi hicho kadhi courts
2. Ni muhimu kuanzishwa kisheria ili watu walioamua kufuata sheria hiyo wakubaliane na hukumu ya kadhi, kama itakuwa haitambuliki kisheria itakuwa haina maana kwasababu itakuwa hakuna tofauti ni kutokuwa na mahakama..kutambulika ni jambo la lazima ili iweze kuitwa mahakama..lakini kuhukumiwa huko ni optional siyo lazima..lakini unapokubali mahakama hiyo lazima ukubali hukumu zake..ok
tuache jazba nataka intellectual arguments ok
J
Sijui nieleze vipi ili nieleweke vema. Nitajaribu.................... mleta mada amejielezea vizuri kuwa: Ndoa ya Kiislaam inatambulika kisheria, Je kwanini kataika mirathi iwe ni suala lisilo tambulika kisheria ? Ndoa na Mirathi vinaweza kutenganishwa ? (elewa Kiislaam ndoa ni Ibada na kufanya mirathi katika misingi ya kidini ni ibada pia) na linapokuja suala la uchangiaji gharama ndio inakuwa nongwa. Kwani Kodi inalipwa na jamii moja au na wengine wanalipa ? kwanini jamii moja ijifanye yenyewe ndio ina ultimantum ? Hapa ndio makubaliano ya Wakristo na Serikali (MoU) yanapoingia, kwanini kodi ya Watanzania kwa ujumla wao zilipie Taasisi za Kikistro ? Katika hili jamii zingine zilihusishwa ? consider yourself that ur an Interllectual and u a now answering the above arguments !
............!bado huna hoja ya ushawishi
Inategemea nani anataka kushawishika na utayari wa kushawishika.Ikiwa wewe tayari una opinion yako na unachotaka ni kujisikiliza kwa kupitia midomo ya watu wengine, ni dhahiri hoja yangu haitakushawishi asilani.
,Hukumu za kesi wakati mwingine Majaji huzitoa kufuatia reference ya kesi nyingine
Kweli Stare decis na doctrines of precedent ni part of case law.Sasa wewe unataka kusema Tanzania itakurupuka tu kwenda kuchukua hukumu toka Kenya na Uganda? Na hata kama, hizo hukumu siyo binding but merely persuasive!
huongozwa na busara na mazingira ya kufanana na tukio ua kesi husika.
Still not binding.
Hili liko pia katika ushahidi, ambapo Wakili unaweza kujenga hoja (Authority) kufuatia maamuzi ya kesi fulani inayofanana na hiyo na Jaji akashawishika na kutoa hukumu (hata kama kesi ni ya 1920 !). Hivyo bado Mifano ya Kenya na Uganda matters !
Rejea my earlier argument
Mbona Wakoloni wa Kiingereza walikubali hii Mahakama ?
Ni wao, na jinsi walivyoona inawafaa.Umesahau pia kuzungumzia "native courts" chini ya mfumo wa kikoloni.
hebu onyesheni threat, yaani ambaye hahausiki atapoteza nini ?
Hakuna threat as such bali ni the way nchi ilivyo - secular state haiwezi kuburuta dini ya kila mtu ndani ya mifumo ya serikali.Mbona huzungumziii sheria za wakatoliki za ndoa chini ya sheria za kanisa?
Ndio maana mleta mada alileta angalizo la "Interllectuals" hivyo fuata ushauri wake kwenye kujenga hoja !
Hii "interllectuals" mi inaniacha hoi maana ukijaribu kuweka intellectual argument, kuna akina Anheuse wanaponda na kusema ni kimbelembele! Bora mleta mada aondoe hilo neno kwenye mada kuu!
Kama kweli unataka so called "Intellectual Arguments" basi ungeweka hii mada kwenye jukwaa la sheria ili watu wajadili kisheria sheria na kikatiba katiba. Zaidi ya hapo itakuwa n i hisia na ushasbiki wa kidini. ukichanganywa na siasa.( mleta hoja aliiweka hii mada kwenye jukwaa la siasa. na bado akawa anasema intelectual. May be inteleectual aliymmaanisha ni ya KISIASA)
Mimi comment yangu moja tu kwenye uzi niulize wachangaji wote watakapenda kuchangia na mleta mada
je wewe kama ungekuwa mwanasheria mkuu wa serikali uko tayari kurushu na kumshauri raisi akubali kuingiza rasmi mfumo wa mahakama za mila za wajaruo, wahaya, na makabila mengine kwenye mahakama ya JMT.
NB
Agalizo kuna mila zina utaratibu wao mfano wa mirathi
Sasa angalia mtu anayetaka inteectual argument alivyjibu
ni makosa kulinganisha wahaya na uislam ok..
Kama kweli uanzishwaji wa mahakama za adhi ni kwa ajili ya mirathi tu, basi hapo hakuna haja ya kupigishana kelele, msisi uelekezwe katika mafundisho ya dini juu ya namna ya kujenga familia na kugawanya mirathi.
Hapo tutakuwa tumepiga hatua katika kuzuia tatizo, badala ya kung'ang'ania mfumo wa kusubiri matatizo
Kanisa Katoliki linazo mahakama zake na zinahusiana na masuala ya Ibada, ndoa na talaka vile vile. Na zinaendeshwa na Wakatoliki wenyewe na wapo watu wamesomea sheria hizo na kuna mfumo wa rufaa hadi Vaticani. Maamuzi yake yanaheshimiwa na sheria za nchi zilivyo sasa na serikali haiwezi kuingilia maamuzi ya mahakama hizo. Zina majaji na mawakili na zinafanya kazi miaka nenda rudi na hazijahitaji hata mara moja kuingizwa kwenye katiba ya nchi au kutengewa fedha za serikali. Hakuna sheria yoyote iliyotungwa yenye kuzitambua mahakama hizi kwa sababu ni sehemu ya ibada ya Wakatoliki na hatuhitaji sheria ya Bunge kutambua ni sehemu gani ya ibada yetu ni halali. Ninaamini Waislamu wakianzisha mahakama ya kadhi na kuwa ni sehemu ya ibada yao hakuna mtu atawauliza.
Mahakama za kadhi zinaweza kufanya kazi kwa mtindo huu huu. Vinginevyo, na watu wa dini nyingine nao wakitaka kuanzisha mahakama yao inayogharimiwa na Watanzania wote itakuwaje; hatuna uwezo wa kuendesha mahakama za kidini. Binafsi ninaamini (nilishalionesha hili miaka karibu mitatu nyuma) kuwa Waislamu wanaweza kabisa kuendesha mahakama zao na wanaweza kutumia serikali kufanikisha hivyo kwa mfano.
a. Taasisi za Kiislamu ziunganike na kufanya mazungumzo na serikali (kitu ambacho tayari kinafanyika) jinsi ya kuendesha mahakama hizo.
b. Waislamu wote na watu wengine (kama wapo) ambao wangependa kuona mahakama ya kadhi inakuwepo wapewe nafasi ya kuchangia kwa kukatwa mishahara yao kila mwezi ili kujenga mfumo wa kulipia hilo. Serikali inaweza kukata mishahara ya watumishi Waislamu wote (au wenye majina ya Kiislamu) unless wakatae. Kwa mfano, kama kila mfanyakazi Muislamu akikatawa shilingi 20,000 kwa mwezi na tuseme wapo wafanyakazi 200,000 tu basi kwa mwezi the Kadhi Fund itakuwa na shilingi 4,000,000,000 (shilingi bilioni 4).
c. kwa vile si Waislamu wote wako kwenye ajira rasmi basi kila msikiti wa Tanzania utatakiwa kuwa na sadaka ya Mfuko wa Kadhi ambapo Waislamu watatoa wenyewe (sijui utaratibu wa kuchangia mambo ukoje) na kwa vile tumewambiwa hiki ni kilio cha Waislamu nina uhakika fedha nyingi tu zitaweza kupatikana kila wiki au kila mwezi kuchangia ule mfuko wa kadhi.
d. Waislamu wataweza kuajiri na kulipia gharama zote za mahakama ya kadhi, serikali inaweza kusaidia kuadminister mfuko huo (kwa malipo siyo kama hisani). Kwa mfano, kwa mfano kila makato yanayosimamiwa na serikali kutakuwa na gharama ya kama shilingi 1500. Hivyo, Waislamuw wanapata fedha za kuendeshea na serikali nayo inanufaika kwa kukusanya mapato.
How on hell are you going to conduct intellectual debate on non-intellectual issue? Wewe una maoni yako ambayo unataka watu waanzie hapo (kwenye calculation) wakati wengine hata concept yenyewe tu ya kuanzishwa hiyo mahakama inawatia kichefuchefu. Reading your mind, unakereka kweli kweli na ndio maana kila sentensi yako inaishia na 'OK' which means 'that is it'.
Unapowaambia wanaume unahitaji maoni halafu unachagua waseme nini ni ukosefu wa akili. Ikiwa concept yenyewe tu ni kichefu chefu, kuna haja gani ya explore second phase ambayo inainvolve calculations za hoja hewa? Wanufaikaji wa uanzishwaji wa hii mahakama ndio wanatakiwa waianzishe na kuigharamia.
Jana nilikushauri kitu, ila kwa hulka ya mtu dhaifu hukuupenda ushauri wangu na acha niurudie tena: Dini ni imani. Utekelezaji wa misingi ya imani hiyo ndio kipimo cha uhiari wa mtu kuwa wa dini hiyo au lah. Ikiwa mnachohitaji kuamuana kwa misingi ya dini yenu, basi hiyo ni sehemu ya ibada zenu na mnaweza kuyafanya hayo huko huko mnakofanyia ibada zingine. Mimi naamini Muislamu wa kweli atafanya maamuzi kwa mujibu wa sheria za kiislamu na ikiwa hataki basi huyo si muislamu, sasa kama mna mpango wa kulazimishana kuwa na imani, si mlazimishane kwa gharama zenu! Kwa mfn: Kanisa Katoliki lina mabaraza ya ndoa na ustawi wa jamii. Mambo yote yanayohusu matatizo ya ndoa na mahusiano hujadiliwa huko kwa misingi ya imani ya kikatoliki. Ikiwa mtu atapingana na maamuzi hayo ambayo yanaendana na imani ya dini, basi suala hilo litaenda mahakamani. Sasa inatuhusu nini sisi tusio waislamu kuchangia uendeshwaji wa mabaraza ya uamuzi wa ndoa za kiislamu as if ugomvi wenu unatuathiri na sisi?
Wewe umekazana kuzungumzia bajeti as if hizi hela unazozizungumzia ni za msikiti. What if Wakurya tukiamua kesi zetu wa kuwatia mkong'oto kina wife ziundiwe mahakama zake binafs kwa kuwa majaji wa mahakama za sheria hawajui mila zetu?
Intellectual gani usiyejua sheria za nchi yako? Kwanza nijuavyo mimi, Waislamu mambo yao huamuliwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za kiislamu. Ni heri ungeniambia mnaandaa mchakato wa kuboresha uelewa wa majaji juu ya sheria za dini yenu kuliko kunilazimisha nishiriki calculation za kodi yangu kuamua matatizo yako ya wewe kuwa na wake 6 na watoto 18. Mtakuwa mna yenu, wala si dini.
Leta hoja ya msingi juu ya kwa nini wasio waislamu wawajibike kuchangia mambo yenu, sio hii.
Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu..umefariki
Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam
Kwanini mali yake isigawanywe kiislam?? tunataka kadhi wawasaidie hao wanawake, watoto kuhusu mgawanyiko wa mali ya muumini huyu.. siyo voluntarily iwe sheria kabisa na hukumu itolewe na mahakama..ok
Ndio maana tunataka mahakama ya Kadhi..
NB: Naomba wale wenye hasira na uislam na waislamu watuache kwanza tuseme kwanini tunataka mahakama ya kadhi ili mtuelewe
Madhehebu mengine yanaweza vipi, how?Ni kwanini waislamu hawawezi ku enforce laws zao wenyewe za kiibada kwenye mahakama zao mpaka wasaidiwe na serikali lakini madhehebu mengine ya dini yanaweza?
Ninachosema mimi ni kwamba mambo ya ibada inabidi yabaki kuwa ya ibada bila kuihusisha serikali. Kama mtu(muislam) kaamua kutotii sheria za kiislam(ambazo ni ibada) hauwezi kumlazimisha kutii hizo amri kwa kutumia chombo cha serikali kwa sababu katiba yetu inatupa uhuru wa kuabudu au kutoabudu kitu chochote. Kwa hiyo kama muislam yeyote kaamua kutozifuata hizo amri ni uamuzi wake na hauwezi kumlazimisha kwa sababu huko ni kuvunja katiba. Mkuu kwa tanzania yetu, amri za dini zetu siyo mikataba ambayo ni lazima kuifuata...tunao uhuru wa kuzifuata hizo sheria kama wacha Mungu wa kweli au kutumia sheria za serikali kama tumeamua kumuweka Mungu pembeni...!Madhehebu mengine yanaweza vipi, how?
Mahakama ya kanisa ikiamuru, kwa mfano, mali ya mtaliki iende kulipia ada na malezi ya mtoto, na wewe ukakaidi wanakufanya nini, wanakufukuza kwenye fellowship ya maombi ya Jumatano? Padri, Shehe, Kadhi Mkuu, hana dola, ana enforce vipi amri yake?
We si unaona jamaa wamekomaa hawataki na kodi yao ! Maana wanalipa peke yao na wana ultimatum nani wa kumpa !mkuu topical, malengo ya uzi wako yametimia?
Ninachosema mimi ni kwamba mambo ya ibada inabidi yabaki kuwa ya ibada bila kuihusisha serikali. Kama mtu(muislam) kaamua kutotii sheria za kiislam(ambazo ni ibada) hauwezi kumlazimisha kutii hizo amri kwa kutumia chombo cha serikali kwa sababu katiba yetu inatupa uhuru wa kuabudu au kutoabudu kitu chochote. Kwa hiyo kama muislam yeyote kaamua kutozifuata hizo amri ni uamuzi wake na hauwezi kumlazimisha kwa sababu huko ni kuvunja katiba. Mkuu kwa tanzania yetu, amri za dini zetu siyo mikataba ambayo ni lazima kuifuata...tunao uhuru wa kuzifuata hizo sheria kama wacha Mungu wa kweli au kutumia sheria za serikali kama tumeamua kumuweka Mungu pembeni...!
Mwanakijiji
a. Wakristo wenyewe watataka mahakama sasa kwa vile waislamu wameomba?? au wanataka sidhani kama itakuwa ni mahitaji yao kwakuwa kutofauta hiyo hukumu za kikristo ni dhambi kwa wakristo..kama ni dhambi then wanaogopa nini kuomba kuanzishwa siku zote?? wala hatujaona huo mfano kwa nchi nyingi za kikristo duniani mbona sijaona hiyo sheria na hukumu zikitumika? kadhi courts ambazo zipo hata kwa nchi za kikristo kwa ajili ya waislamu kwasababu ni ibada...kwa hiyo hoja yako ni uwongo au uchoyo na chuki tu kwa waislam wa Tanzania
b. Waislamu wa Tanzania wanalipa kodi kama wananchi wengine kuna kuwa na shida gani kuhudumia na pesa za serikali kwakuwa hata sasa kuna kesi za kiislamu katika mahakama za kawaida ambapo hakimu analipwa lakini anahukumu kesi ambazo hana ujuzi nayo??..kazi ya serikali ni kuhudumia wananchi wote kwahiyo hawa waislamu wanaotaka mahakama ya kadhi pesa zao zinatakuwa hizo hizo zinazoenda katika mahakama zetu ..ndio maana nikasema serikali inatakiwa kupeleka kwenye kadhi funds pesa equivalent na kesi ambazo zingeenda mahakama za sasa not otherwise..
Sijaona mantiki ya waislamu kulipia huduma ambayo serikali inatakiwa kutoa kwa wananchi wake..
hivi kazi ya serkali ni kuchonga Misalaba na kugaramia watu kwenda hija maka! Mbona unalazimisha mbuzi kula nyama?