Wanaoongea peke yao wanazidi kuongezeka

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,868
730,470
Maisha yana maajabu mengi na mojawapo ni hili la watu kuongea pekeyao achana na mazungumzo ya kimya achana na mawazo ya kawaida hiki ni kitu kilichojengwa katika wizara nyingine kabisa wizara ya mawazo halisia.

Sio wendawazimu sio vichaa hawajarogwa hawajalewa ni watu wana akili zao timamu na familia zao na kazi zao lakini wanaongea pekeyao barabarani

Ni changamoto za maisha na mikwamo mingi ndio husababisha yote haya

Migogoro kwenye mahusiano
Changamoto za kipato
Matumizi ya kila siku
Watoto Shuleni
Kodi za nyumba
Madeni
Ndugu...!

d729d3f53c6c09178ec38b59a2ae8e4b.jpg


Inafika mahali mtu anawaza kwa sauti anaongea na kujijibu mwenyewe, yani katengeneza nafsi mbili kwenye moja anauliza anajijibu anabisha anabisha anashangaa yeye huyo huyo anafikia maamuzi au anasonya au anatukana yeye huyo huyo.

Anaweza kutoka ubungo mpaka kimara bila kujijua. Anaweza kukujibu kuwa na fahamu kamili. Ukikutana na mtu kapatwa na ajali ya kugongwa au kugonga usikimbilie. kumlaumu watu wamebeba mizigo mingi kichwani.

Pamoja na changamoto zote ulizo nazo jitahidi Usiwe mmoja wao.
 
Maneno kuntu kuna jamaa mmoja yeye alikuwa akitembea barabarani anaongea peke yake anarusha hadi mikono kwa ishara na anatoa sauti hadi akikutana na mtu ndo anashtuka sisi tukiwa wadogo tulikuwa tunajificha mahali tukiona anapita tunamsikiliza tunacheka ila sasaivi nshakuwa mkubwa naelewa kwanini watu huwa wanaongea peke yao.
 
Back
Top Bottom