Kumekuwa na wimbi la wanaume wengi kuwa na stress kiasi kwamba wanapopata msongo mwingi wa mawazo wanafikia hata kuongea barabarani peke yao

Refrector

Senior Member
Mar 13, 2014
187
117
Kumekuwa na wimbi la wanaume wengi kuwa na stress kiasi kwamba wanapopata msongo mwingi wa mawazo wanafikia hata kuongea barabarani peke yao kiasi kwamba ameshindwa wa kumshirikisha jambo lake hasa la kindoa Ili kupata suluhu ya anayoyapitia kwa wakati huo.

Pia kunawimbi la wanawake wengi wamekuwa wakiwanyanyasa waume zao either kwa kipato au kwakuwa anahisi yeye ni mzuri na huyo aliye naye Hana vigezo vya kuwa naye na wao kwa kushindwa kuwa na msimamo yaani kukaa kwenye nafasi yake Kama mwanaume anaishia kuwa mdhaifu na ndipo anapoanza kuwa na mawazo lakini hawezi jinasua kwani anahofia watu watamuangaliaje.

Pia wanaume wengi wakishakuwa na msongo wa mawazo hupatwa na kuishiwa na nguvu za kiume na kujikuta anatukanwa na kurushiwa vijembe kiasi kwamba atashindwa kupata ujasiri wa kuwa kwenye nafasi yake akihisi ni atatangazwa kwa ndugu na kujikuta ananyanyasika na mkewe maana asije toa siri kwa watu.

Kwa wasomi kuwa na mtazamo wa kupenda wasomi wenzao hata Kama hao wawapendao hawana pendo la kweli kwao, hiyo imekuwa shida sanaa na kuona wanaume wengi wakilalama kuwa tumekosea kuoa na kosa likiwa lilishindikana kugundua mwanzo kabisa ulipokuwa unatafuta mwenza aweje na usioe kazi ,Mali au Kitu chochote cha nje jaribu kupata mtu wa ndani yupoje maana kasha la nje mala zote huwa la kuvutia lakini ndani ya kasha huwa Kuna aina nyingi ya ujazo ulichojaza kasha.

Hofu ya muda kwenda mtu anakurupuka popote Kambi Ili akimbizane na mda itakugharimu muda sio mrefu maana vitu ulivyokuwa unatarajia kuvipata utavipata kwa 20% au ukaanza kugundua makosa ndani ya mda mfupi pata mda wa kujiridhisha hasa kujua mapungufu ya mwenza zaidi kuliko mazuri Ili upime Kama mapungufu yake utayamudu..!!wengi huona mazuri zaidi siku akipata jaribu hakulitarajia kulipata anamwacha siku hiyo hiyo...

Kiwango cha muhusika kutokana na atokako ni level flani huyu ni mtoto wa mbunge au waziri na mm ni Professor huo ni ufinyu wa mawazo maana unaweza pata mtu mkawa vizuri mkaendana na ukaishi bila msongo wa mawazo na Amani,furaha na heshima vikawa ndio sehemu yenu ya maisha na matunzo yako kwake atakuja kuwa level yako kabisa .

Pia naona wimbi kubwa Sana la wanaume wanakimbia familiar zao hata kama kajenga yupo radhi kwenda kupanga chumba kimoja na kujiweka kipekee kana kwamba ni single na ikiwa anafamilia yake na anaona upweke ndio suluhu jibu kukimbia tatizo sio mwisho wa tatizo maana tayari ukiumizwa kwa point ya juu saana sumu inakuwa moyoni mwako usipotafuta mapatano yako na muhusika maana mwanaume mwerevu asipotumia nguvu nyingi kwa mwanamke Mambo yanaweza Kaa vizuri na kuwekana sawa ABC zenu na Kama mmoja atakuwa amejaza makosa ya mwenza moyoni na kuhesabu Mambo ya kale anaishi nayo Hilo tatizo la suluhu itakuwa ngumu na kukimbia pia sio suluhu maana familiar nyingi zinakosa mwelekeo wa wazazi kwa kutoelewana kwa wazazi pia Kila siku uanze maisha mapya nayo ni kupoteza mda wako,..Hata umpate mpya bado shida itakuwepo palepale maana hakuna mkamilifu chini ya jua hivyo hata Mungu mwenyewe alishasema kwamba kiumbe hiki nilichokiumba kwa mkono wangu nimekushindwa....!!
 
Hata hapo umeongea peke yako........piga PUNYETO upunguze stress blaza.........
 
Niliandika heading nzuri na fupi but nilipo upload heading nazani ni system tu ikawa hivyo lakini ujumbe utaeleweka tu Asante
 
Kuongea barabarani haitokani na stress Bali kuwaza kwa sauti. Anaweza kuwa anawaza Mambo mema akacheka na Kama scene Ina majibizano atauliza na kujibu suala mazungumzo yakamilike
 
Kumekuwa na wimbi la wanaume wengi kuwa na stress kiasi kwamba wanapopata msongo mwingi wa mawazo wanafikia hata kuongea barabarani peke yao kiasi kwamba ameshindwa wa kumshirikisha jambo lake hasa la kindoa Ili kupata suluhu ya anayoyapitia kwa wakati huo.
Umefanya research hii wapi.
 
Back
Top Bottom