Wanaomchukia Paul Makonda wanafuata mkumbo tu

Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,657
3,654
Wakuu habari za Jumapili. Najua mada hii ninayoianzisha nitapata upinzani mkubwa sana na matusi mengi mno. Lakini kabla hamjanitukana nawaomba mfikiri sana na muweke pembeni ushabiki.

Ni kwamba kwa muda mrefu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh. Paul Makonda amekuwa midomoni mwa watu wengi wakimsema kwa mabaya mengi. Tena utakuta mtu anayeonesha chuki kwa mkuu huyu wa Mkoa wa Dar Es Salaam ukimuuliza sababu hataweza kukueleza ni kwa nini anamchukia. Wengi wanafuata mkumbo tu baada ya kuona watu wenye ushawishi na uwezo wa kupanga maneno wanamsema vibaya.

Hebu kaeni chini mjiulize na mfanye uchunguzi kwa kujiuliza kosa la Mh Makonda ni lipi? Kuweni wakweli wakati mkitafakari hayo kama nilivyosema hapo juu kwamba muweke ushabiki pembeni.......!!!

Tulipokuwa chuoni tulikuwa tukiandamana kwenda kudai posho wizarani. Wakati huo usipoandamana wanafunzi wenzako wanakuona mbaya na utapata taabu sana kama hukuhudhuria ama kuungana nao kwenye maandamano. Ndicho kinachotokea kwa Mh Paul Makonda. Ukimuuliza mtu kwa nini anamsema vibaya Mheshimiwa huyu utakuta hata yeye hajui!!!

Wana Dar Es Salaam mjiulize sana ubaya wa Makonda. Hivi kosa lake ni kuwaletea maendeleo? Ina maana ninyi hampendi au hamtaki maendeleo?
Eti mnadai Mh Paul Makonda hana vyeti.....na kwamba eti alifeli......pia eti jina lake si hili la Paul Makonda bali analo jina lingine.........!!!

Mimi nashangaa sana.....
Hivi mlikuwa wapi toka Mh Paul Makonda bado mvulana mdogo kabisa kufichua hilo jina lake? Mmesubiri mpaka amekuwa Mkuu wa Mkoa ndio mnaibuka na kudai hana vyeti na jina lake analotumia si lake? Miaka yote mlikuwa wapi??? Acheni ubabaishaji!!

Yaani unasubiri mtu amepata mafanikio ndio mnaibuka ili mumharibie? Kama ni hivyo basi ninyi ni watu wabaya sana!!! Hamfai..........!!
Nirudi kwenye hili la vyeti.

Kwamba kama ni kweli watu wanayoyasema (kitu ambacho mimi siamini kabisa maana nchi hii ina vyombo vingi sana vya upelelezi vilishindwa kujua hili? Eti mtu mwingine asiye na taaluma ya upelelezi aje atuaminishe na sisi kwa kufuata mkumbo tumeamini uzushi!!!) basi Mh Paul Makonda is a hero!!!

He is a fighter! Badala ya kubezwa angepewa hongera kwa juhudi za ku struggle kutafuta maisha!!! Wangapi wamerudia kusoma darasa la saba bwana na leo hii ni maprofesa? Yaani ku fight kuondoa ujinga ni kosa?

Lakini hoja ya msingi hapa ni madai yanayotolewa na watu eti Mh Makonda jina lake sahihi ni Bashite. Huu ni ujuha wa hali ya juu. Hivi unaamini vipi jina la Bashite na kuacha la Paul Makonda? Yaani jina analotumiia mwenyewe hulikubali bali unakubali jina linalozushwa mitandaoni? Huo ni usomi gani Watanzania mnauonyesha?

Lengo langu si kumtetea Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam bali nasema ukweli mtupu. Tuacheni ubabaishaji!!

Eti kuna madai Mh Makonda alivamia studio za Clouds.......mimi naomba niulize swali.....

Hivi hiyo Laptop na kile chumba alichokuwa akitumia hapo ofisi za Clouds nacho alikiteka? Na hicho chakula alichokuwa akiwekewa na uongozi wa Clouds kisha wanampigia simu chakula kipo tayari anakwenda kula nao meza moja napenyewe aliwateka?

Hiyo Laptop ya Mh Makonda iliyokuwa hapo ofisini kisha baada ya muda wa kazi wanamkaribisha kufanya kazi zake binafsi napo aliwalazimisha kwa nguvu ikae hapo? Mbona haya yote sijasikia mkiyatafakari bali mnatafakari vyeti tu na jina?

Jambo usilolijua huna haki ya kulizungumzia. Hivi mtakuja kupata mkuu wa mkoa mchapa kazi kama Paul Makonda? Kosa lake ni lipi hili la kupambana na maharamia wa madawa ya kulevya? Kwa hiyo mnatakaje sasa? Mnataka Dar Es Salaam na nchi kwa ujumla iwe na mazezeta wabwia unga ndio mnaona sawa?

Hii haikubaliki!!! Msitumie vyombo vya habari na uhuru wa habari kupakazia watu. Kama ni vyeti mbona watoto wenu hawana kabisa mbona hamsemi!!
Huo ugomvi wa Clouds na Makonda ni wa kibinadsi zaidi.

Wanajua ni kipi makonda alikuwa anakifanya. Walimkaribisha wenyewe studio na wala hakuvamia. Wasitake kudhani sisi ni wajinga kiasi hicho.
Makonda ni mchapa kazi.

1. Anataka Dar Es Salaam wanafunzi wafaulu.
2. Anataka Dar Es Salaam iwe ni jiji safi
3. Anataka barabara zote ziwe nzuri
4. Anataka kuwepo amani ya nchi
5. Hataki uonevu kwa raia
6.Ni mtu wa watu
7. Anataka watu wapate ajira
8. Anataka vijana wapewe nafasi za kuongoza nchi
9. Anataka watu walipe kodi
10. Anapiga vita madawa ya kulevya na ufisadi

Sasa huyu mtu ubaya wake ni upi?
Kwa hiyo nimegundua watu wamekuwa overwhelmed na mwangi tu yaani mkumbo wa watu. Hana kosa. Weka ushabiki pembeni kisha waza mwenyewe kwa makini utagundua Dar ina Mkuu wa Mkoa madhubuti sana.

Nampongeza sana Mh Makonda kwa kukaa kimya bila kujibizana na watu maana anajua ni kitu gani wananchi tunataka.

Nasubiri matusi na upinzani mkali kutoka kwa wachangiaji lakini sitajali.......
Mh Makonda chapa kazi!
 
Wengi walikuwa wanamsifia sana Paul Makonda.Ila baada ya vita ya dawa za kulevya kutowaacha salama vipenzi vyao wengi walibadili upepo.Si unawajua watanzania lakini??
 
Makonda tulimchukia tokea akiwa UVCCM. tena tulisema sana mapungufu yake na jinsi alivyofoji elimu yake. sema alikuwa hajafahamika sana watu walikuwa wanapotezea tu. Makonda tulimchukia zaidi alipompiga mzee wetu jaji Joseph Warioba
 
Hahah mtoa uzi anafurahisha kwakwel kaandika maneno mengi Lakini pointless... Eti mnaachaj kuamn jina la paul mnaamn labashite kwaio anajidai hajui mfumo wakufoji vyeti huyu au... Uyo paul alizaliwa akiwa mkuu wa mkoa kwanza yy sio binadam hadi ashindw kufoji vyeti...... Maendeleo yy peke ake ndo kaleta dar ipo hapa ilipo kwasabab kulikua nawakuu wa mkoa huu kabla yake, nawatafata wengi baadae, usisingizie maendeleo kama ww ambavyo humchukii na wapo ambao wanamchukia iwe kwasababu fulani au bila sababu yyte hivo sio lazma kumkubali mtu, ata ww kuna watu ktk jamii yako unawez ukawa huwakubali bila sababu, japo naaamn sababu zipo mbona mara ya kwanza watu kibao walikua wanamkubali, y suddenly change basi ujue kuna sababu. Ivo msihangaike sanaa kuwaamulia watu mtu wakumchukia na wakumkubali yy sio mkuu wa mkoa wa kwanza dar na sio kiongozi wakwanza kuchukiwa
 
Hahah mtoa uzi anafurahisha kwakwel kaandika maneno mengi Lakini pointless... Eti mnaachaj kuamn jina la paul mnaamn labashite kwaio anajidai hajui mfumo wakufoji vyeti huyu au... Uyo paul alizaliwa akiwa mkuu wa mkoa kwanza yy sio binadam hadi ashindw kufoji vyeti...... Maendeleo yy peke ake ndo kaleta dar ipo hapa ilipo kwasabab kulikua nawakuu wa mkoa huu kabla yake, nawatafata wengi baadae, usisingizie maendeleo kama ww ambavyo humchukii na wapo ambao wanamchukia iwe kwasababu fulani au bila sababu yyte hivo sio lazma kumkubali mtu, ata ww kuna watu ktk jamii yako unawez ukawa huwakubali bila sababu, japo naaamn sababu zipo mbona mara ya kwanza watu kibao walikua wanamkubali, y suddenly change basi ujue kuna sababu. Ivo msihangaike sanaa kuwaamulia watu mtu wakumchukia na wakumkubali yy sio mkuu wa mkoa wa kwanza dar na sio kiongozi wakwanza kuchukiwa
Kwa hiyo kumbe zamani walikuwa wanampenda. Ila sasa hivi hawampendi kwa sababu kawaharibia biashara yao ya madawa. Si ndiyo?
 
Umetumwa kuja kumsafisha kweli nimeamini hata kama dunia nzima itakuchukia kwa mabaya yako kuna watu tu bado watakupenda ingawaje wanajua so shameless
 
Aisee nilishaulizag watu wengi sana wanaomchukia makonda kosa lake nini, sijawahi kupata majibu zaidi ya blabla mwenye majibu tafadhali.
Inategemea unamuuliza nani, kama unauliza mataahira wenzako sawa na mtoa mada unategemea nini?

By the way, watu hawamchukii bali watu hawapendezwi na ujinga alioufanya, kuchukia na kutokupenda ni mambo mawili tofauti. Sasa kama wewe unapenda ujinga aliokua anaufanya wa kudhalilisha watu bila ushahidi na bila sababu, kutukana watu wenye taaluma zao kwenye ziara zake wakati hana vyeti alafu ukaona alikua anafanya vizuri basi nina hakika una mtindio wa ubongo.

Ishu kwamba watu walikua wapi muda wote huo wasiseme ana vyeti feki hii ni hoja ya kitaahira kabisa. Kuna waziri mmoja huko ujerumani alikua na Phd feki(alinakili thesis ya mwenzake), akaingia kwenye siasa na hadi kupata uwaziri, ila alipoleta ujinga watu wakamharibia kua ana Phd feki na akajiuzuru.

Tafteni hoja za msingi za kumtetea bwana yenu.
 
Ni mchapa kazi

Kiongozi jembe

Makonda oyeeeeee
7649abd1e6489f249bf3b98699980db7.jpg
 
Back
Top Bottom