Wanaomchukia Paul Makonda wanafuata mkumbo tu

Wanaomchukia Paul Makonda wanafuata mkumbo tu

Yaani umekaa ukaona ufungue thread na kuandika ujinga?? Una mambo ya kufanya????
 
Foolishness, mi nilidhani unaxungumzia alichokifanya kwa wananchi toka vyombo vya habari vilivyommute lakini umekuja na bla bla.
Hakuna mtu anayechukiwa katika dunia hii ila vitendo vya muhusika ndio hata wewe ulipokuwa mtoto kila mtu alikuwa anakusifia ila ulipoanza kutafuta sifa za kijinga kama hizi nadhani kuna watu wanakuchukia

Hakuna mwenye shaka na uchapakazi wake ila kama binadamu tulioumbwa na utashi tunaamini mtu anayekemea wenzake yeye hana hata doa ni imani tu kama dini zetu zilivyo tunavyoziamini.
Ajabu yeye alithubutu kutaja waovu hadharani na mimi kama mtanzania mzalendo nikamuunga asilimia mia kwa kusema kijana mwenzangu anaonyesha kazi iliyitukuka

Ooooh kila kwenye mapambano hapakosi mashambulizi, aliposhambuliwa kuhusu tuhuma hizo hajajitokeza hadharani kama kijana shupavu na jasiri kupinga na hata kuonyesha wazungu wanasema evidence.
Mimi nakubari na nitaendelea kukubari kuwa alikuwa analipigania taifa dhidi ya uovu lakini na yeye alishamuumiza mtu binafsi (kwa kushindwa kukanusha kwa vithibitisho tuhuma zaidi ya kuruka ruka na kugeuza hoja ya kitaifa kuwa kuchaka chake)
Mkuu kiuhalisia hakuna anayemchukia RC binafsi tatizo vitendo.
 
Inategemea unamuuliza nani, kama unauliza mataahira wenzako sawa na mtoa mada unategemea nini?

By the way, watu hawamchukii bali watu hawapendezwi na ujinga alioufanya, kuchukia na kutokupenda ni mambo mawili tofauti. Sasa kama wewe unapenda ujinga aliokua anaufanya wa kudhalilisha watu bila ushahidi na bila sababu, kutukana watu wenye taaluma zao kwenye ziara zake wakati hana vyeti alafu ukaona alikua anafanya vizuri basi nina hakika una mtindio wa ubongo.

Ishu kwamba watu walikua wapi muda wote huo wasiseme ana vyeti feki hii ni hoja ya kitaahira kabisa. Kuna waziri mmoja huko ujerumani alikua na Phd feki(alinakili thesis ya mwenzake), akaingia kwenye siasa na hadi kupata uwaziri, ila alipoleta ujinga watu wakamharibia kua ana Phd feki na akajiuzuru.

Tafteni hoja za msingi za kumtetea bwana yenu.
Respect ni kitu muhimu sana, wafanyakazi ukiwaonyesha heshima utaona mabadiliko ya utendaji wao, sio kila kitu unajua.
 
Wakuu habari za Jumapili. Najua mada hii ninayoianzisha nitapata upinzani mkubwa sana na matusi mengi mno. Lakini kabla hamjanitukana nawaomba mfikiri sana na muweke pembeni ushabiki.

Ni kwamba kwa muda mrefu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh. Paul Makonda amekuwa midomoni mwa watu wengi wakimsema kwa mabaya mengi. Tena utakuta mtu anayeonesha chuki kwa mkuu huyu wa Mkoa wa Dar Es Salaam ukimuuliza sababu hataweza kukueleza ni kwa nini anamchukia. Wengi wanafuata mkumbo tu baada ya kuona watu wenye ushawishi na uwezo wa kupanga maneno wanamsema vibaya.

Hebu kaeni chini mjiulize na mfanye uchunguzi kwa kujiuliza kosa la Mh Makonda ni lipi? Kuweni wakweli wakati mkitafakari hayo kama nilivyosema hapo juu kwamba muweke ushabiki pembeni.......!!!

Tulipokuwa chuoni tulikuwa tukiandamana kwenda kudai posho wizarani. Wakati huo usipoandamana wanafunzi wenzako wanakuona mbaya na utapata taabu sana kama hukuhudhuria ama kuungana nao kwenye maandamano. Ndicho kinachotokea kwa Mh Paul Makonda. Ukimuuliza mtu kwa nini anamsema vibaya Mheshimiwa huyu utakuta hata yeye hajui!!!

Wana Dar Es Salaam mjiulize sana ubaya wa Makonda. Hivi kosa lake ni kuwaletea maendeleo? Ina maana ninyi hampendi au hamtaki maendeleo?
Eti mnadai Mh Paul Makonda hana vyeti.....na kwamba eti alifeli......pia eti jina lake si hili la Paul Makonda bali analo jina lingine.........!!!

Mimi nashangaa sana.....
Hivi mlikuwa wapi toka Mh Paul Makonda bado mvulana mdogo kabisa kufichua hilo jina lake? Mmesubiri mpaka amekuwa Mkuu wa Mkoa ndio mnaibuka na kudai hana vyeti na jina lake analotumia si lake? Miaka yote mlikuwa wapi??? Acheni ubabaishaji!!

Yaani unasubiri mtu amepata mafanikio ndio mnaibuka ili mumharibie? Kama ni hivyo basi ninyi ni watu wabaya sana!!! Hamfai..........!!
Nirudi kwenye hili la vyeti.

Kwamba kama ni kweli watu wanayoyasema (kitu ambacho mimi siamini kabisa maana nchi hii ina vyombo vingi sana vya upelelezi vilishindwa kujua hili? Eti mtu mwingine asiye na taaluma ya upelelezi aje atuaminishe na sisi kwa kufuata mkumbo tumeamini uzushi!!!) basi Mh Paul Makonda is a hero!!!

He is a fighter! Badala ya kubezwa angepewa hongera kwa juhudi za ku struggle kutafuta maisha!!! Wangapi wamerudia kusoma darasa la saba bwana na leo hii ni maprofesa? Yaani ku fight kuondoa ujinga ni kosa?

Lakini hoja ya msingi hapa ni madai yanayotolewa na watu eti Mh Makonda jina lake sahihi ni Bashite. Huu ni ujuha wa hali ya juu. Hivi unaamini vipi jina la Bashite na kuacha la Paul Makonda? Yaani jina analotumiia mwenyewe hulikubali bali unakubali jina linalozushwa mitandaoni? Huo ni usomi gani Watanzania mnauonyesha?

Lengo langu si kumtetea Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam bali nasema ukweli mtupu. Tuacheni ubabaishaji!!

Eti kuna madai Mh Makonda alivamia studio za Clouds.......mimi naomba niulize swali.....

Hivi hiyo Laptop na kile chumba alichokuwa akitumia hapo ofisi za Clouds nacho alikiteka? Na hicho chakula alichokuwa akiwekewa na uongozi wa Clouds kisha wanampigia simu chakula kipo tayari anakwenda kula nao meza moja napenyewe aliwateka?

Hiyo Laptop ya Mh Makonda iliyokuwa hapo ofisini kisha baada ya muda wa kazi wanamkaribisha kufanya kazi zake binafsi napo aliwalazimisha kwa nguvu ikae hapo? Mbona haya yote sijasikia mkiyatafakari bali mnatafakari vyeti tu na jina?

Jambo usilolijua huna haki ya kulizungumzia. Hivi mtakuja kupata mkuu wa mkoa mchapa kazi kama Paul Makonda? Kosa lake ni lipi hili la kupambana na maharamia wa madawa ya kulevya? Kwa hiyo mnatakaje sasa? Mnataka Dar Es Salaam na nchi kwa ujumla iwe na mazezeta wabwia unga ndio mnaona sawa?

Hii haikubaliki!!! Msitumie vyombo vya habari na uhuru wa habari kupakazia watu. Kama ni vyeti mbona watoto wenu hawana kabisa mbona hamsemi!!
Huo ugomvi wa Clouds na Makonda ni wa kibinadsi zaidi.

Wanajua ni kipi makonda alikuwa anakifanya. Walimkaribisha wenyewe studio na wala hakuvamia. Wasitake kudhani sisi ni wajinga kiasi hicho.
Makonda ni mchapa kazi.

1. Anataka Dar Es Salaam wanafunzi wafaulu.
2. Anataka Dar Es Salaam iwe ni jiji safi
3. Anataka barabara zote ziwe nzuri
4. Anataka kuwepo amani ya nchi
5. Hataki uonevu kwa raia
6.Ni mtu wa watu
7. Anataka watu wapate ajira
8. Anataka vijana wapewe nafasi za kuongoza nchi
9. Anataka watu walipe kodi
10. Anapiga vita madawa ya kulevya na ufisadi

Sasa huyu mtu ubaya wake ni upi?
Kwa hiyo nimegundua watu wamekuwa overwhelmed na mwangi tu yaani mkumbo wa watu. Hana kosa. Weka ushabiki pembeni kisha waza mwenyewe kwa makini utagundua Dar ina Mkuu wa Mkoa madhubuti sana.

Nampongeza sana Mh Makonda kwa kukaa kimya bila kujibizana na watu maana anajua ni kitu gani wananchi tunataka.

Nasubiri matusi na upinzani mkali kutoka kwa wachangiaji lakini sitajali.......
Mh Makonda chapa kazi!
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] siku nyingine usipende kuonyesha njaa yako kwa magreat thinkers kama humu....kama kakuweka kitengo kula kimya kimya, makonda kwa dar ni kochekesho kila anapopita....
 
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] siku nyingine usipende kuonyesha njaa yako kwa magreat thinkers kama humu....kama kakuweka kitengo kula kimya kimya, makonda kwa dar ni kochekesho kila anapopita....
Mimi ni mtu mdogo sana wala hata nikitaka appointment nimwone sitaweza. Pia hata sura yangu haijui. Haya niliyoyasema ni kwa kuwa hatendewi haki.
 
Kama wewe tu bwana makengeza ulivyofata mkumbo kumpenda na sisi hivyo hivyo tumefata mkumbo kumchukia .OVER
 
Kwani hujui sababu? Alipambana na Mayor na Mbunge Kubenea (Viongozi wa CHADEMA) na hakuonyesha kuteteleka hata kidogo. Sababu ya pili alimtaja mwenye chama kwenye issue ya madawa.

Makonda ni jembe, nikimlinganisha na wakuu wa mikoa wengi kawazidi sana kwa ubunifu na uchapakazi. Anastahili pongezi.

Kwa nini anachukiwa kama unavyodai? Hizo ni propaganda zisizo na mashiko, ndo maana angalia wote wanaomponda hawana cha maana zaidi ya kurudia kuonyesha chuki zisizo na sababu.

Hii mbinu ya kutaka kuchafua viongozi kwa kupakazia makosa yasiyo na mashiko, na kisha mazezeta wasiojielewa kuendeleza kelele inatumiwa sana na CHADEMA sasa hivi. Kumbuka issue ya rambirambi kwa mkuu wa mkoa wa Arusha. Lema alidanganya umma kwamba fedha za rambirambi zimeliwa na mkuu wa mkoa. Baadaye mkuu wa mkoa akaweka mambo wazi. Badala ya kumlaani Lema kwa kuwadanganya, wameendelea kuimba nyimbo Kama mazezeta, eti rambirambi zimeliwa, au kuhamisha magoli kwamba zimeenda kukarabati hospitali!
 
f7f5e071385d1c7088bc7a86a3213e2f.jpg
 
Mleta mada hujui usemalo
Eti Bashite analeta maendeleo Dar es salaam,Ni maendeleo gani hayo?
Ni lipi alilikianzisha limefanikiwa? Ni vita ya Shisha,Dadapoa,Waalimu kupanda mabasi bure,upandaji miti,nini....
Yupo hapo kwa ulinzi wa Baba yake mpenzi tuu otherwise angasharudia kazi yake ya kuchoma mkaa
 
Mimi ni mtu mdogo sana wala hata nikitaka appointment nimwone sitaweza. Pia hata sura yangu haijui. Haya niliyoyasema ni kwa kuwa hatendewi haki.
Alivamia clouds TV au hakuvamia? Na je unaona ni sawa au si sawa?
 
Sasa kama ana watoto mbona sijawahi kusikia wanalalamika baba yao kupigwa na Makonda?
Sio lazima walalamike usikie,kuna mwisho wa hizi kazi na ujue ukuu wa mkoa pia utaisha tu, na kisasi sio lazima kulipa kwa muda huohuo.Kisasikinalipwa hata kwa kizazi cha pili cha tatu na hata cha nne take care wewe na bashite
 
Ili niendelee nahitaji niwe na bidii Sio kumpenda Makonda Usitake kujua sababu maana hata wewe sababu ulizo orodhesha sio za msingi maendeleo hayawezi kuletwa na Makonda maana keshapoteza sifa za kuwa kiongozi bora ila sasa ni "Bora awaongoze hivyo hivyo mtake msitake " Nasikia mnaandamana kumuunga mkono Rais hapa ndipo napata kigagasika kama kweli nitaweza pata ile NOAH yangu itakuwa kama ya ESCROW account mlivyokuwa mnabishana mara oh hizi ni za pmhuyo erikali oh mara hizi si za serikali mpaka leo tushapigwa changa na haya makanikia ni kiini macho ila kama unampenda huyo bashite wako hamia kwake asituchoshe.
 
Back
Top Bottom