Dawa ya Mjinga
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 382
- 147
Sijui kwa nini upoteze muda kumtetea mwanamume mwenzio kiasi hiki! Hivi unafikiri katika hali ya kawaida tu kusingekuwepo na ongezeko la mahitaji ya umeme na hivyo ongezeko katika ugavi? Unajua ni kwa kasi gani watanzania wanakimbilia solar power? Je inatokana kuwa na waziri (kwa jina lolote utakalompa) wa Nishati?
Ni upungufu wa fikra kufikiria maendeleo katika nyanja yeyote ile itategemea mtu kama mtu akiwa waziri. Bila shaka anaweza akawezesha na hivyo kuongeza kasi. Lakini kasi gani kwenye sekta ya umeme tumeona. Ni kidogo mno na juu ya hayo angalia takwimu za TANESCO, mapato yao yalivyo athiriwa na kukatika katika umeme, adha wanayopata wananchi kutokana na umeme usio na uhakika, madeni makubwa ya TANESCO licha ya kashfa yote haya wakati wa huyo unayemwona wewe mwanamume!
Wanajamvi,
Nilielezea siku zilizopita mambo mawili. Kwanza ni tabia mbaya ya viongozi wetu kutokujua kwamba cheo ni dhamana. Hutakiwi kukivaa cheo ulichopewa kama nguo ya ndani. Dhamana ifanye koti. Tena kwa sehemu kama Dar ukivaa koti halafu mwenyewe akalitaka, kakupunguzia bughudha ya joto. Matatizo yanatokea kwa sababu viongozi wengi huvaa dhamana ya uongozi kama chupi. Sasa wanatakiwa kuvua (madarakachupi) hadharani inakuwa shida. Ndiyo shida anayopata prof. Ameamini kuwa yeye ndiye waziri na waziri ni yeye. Inakuwa shughuli nzito kumvua chupi hadharani. Anatia huruma. Laiti cheo hicho angekifanya koti saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine. Akumbuke tu kuwa mwanadamu wa damu na nyama hana dhamana. Wakati wowote anaweza kuondoka duniani na Tanzania kama nchi ikaendelea kuwepo (kwa miaka mingi tu). Watu wazuri na wachapa kazi kuliko Muhongo, wapo!
Pili, nilielezea jinsi ilivyo kazi kubwa kutengeneza pilau na uzuri wa mlo ule. Mtu akipika pilau utamhurumia jinsi anavyohangaika huku na kule kuhakikisha kuwa mambo yanakuwa. Kwa upande mwingine mlaji wa pilau itakuwa patashika akiingiwa na riha ya mlo huo kwa kutamani kuupata. Lakini nikatahadharisha kuwa kama pilau likiingia kinyesi (japo kidogo) ni nani atakayekuwa tayari kula? Prof. ni sawa na pilau. Hata hivyo pilau limeingia kinyesi. Halifai hata kutupwa jalalani, bali chooni tu. Inashangaza kuwa bado wako wenye roho ngumu wanataka kulibugia pilau lililoingia kinyesi. Mimi simo!
Sema usemalo, andika uandikalo, ukweli ni kuwa pilau limeingia kinyesi, mlaji tumpe jina gani? Aliyeanazisha mada hii ni mmoja wa watu wenye roho ngumu kupindukia kutuhimiza tuendelee kula pilau lililoingia kinyesi.
