Wanaolalamika kwamba TCU imepandisha madaraja ya kwenda Vyuo Vikuu hawana vigezo

Afixa0

JF-Expert Member
Jun 16, 2015
464
485
Anayetaka aende chuo kikuu asome kwa bidii na ajitume ili akidhi viwango vilivyowekwa na TCU. Haiwezekani mlalamike kwamba iachwe nafasi kubwa ili mpite tuu bila kuwa na ufaulu bora eti kwasababu mnataka kwenda vyuo vikuu.

Hivi mnafikiri ukifika chuo kikuu ndio umefika kwenye maisha mazuri au mnafikra gani kuhusu suala hili? Kipindi kile mlilalamika kuhusu kidato cha nne kwa suala la GPA, Ndalichako akarekebisha leo hii wameweka vigezo bora mnalalamika. Hivi mnataka mfike vyuo vikuu au mpate maarifa? au mnataka nini?

Mwenye uelewa kuhusu elimu hawezi akaishutumu TCU hata kidogo kwasababu vyuo binafsi vimeharibu elimu ya Tz kwa kiasi kikubwa na vya kutosha.

TCU nawapa pongezi sana, mmesababisha vijana wajitume na wasome zaidi, hongereni maana mmewazibia milango wanaopenda njia za panya ili wafike kileleni.

Hivi kwa akili ya kawaida unataka ufike chuo kikuu kwa point 2 halafu we nae ujiite mwanachuo? Na ndio maana hao wamejazana vyuo binafsi mahali wanakojua kuna point ndogo na ukienda hakuna kusapu wala kudisko, pesa ndio inafanya kazi.

Asiyetaka vigezo vya TCU akalime, akafanye biashara nk maana nafasi bado ni kubwa mno. Najua kuna wachache watakaokurupuka kushadadia mada na kutoa hoja nyepesi kama uji wa ngano maana wamezibiwa nafasi kwa viwango bora wasivyotaka,, lakini sijali nazidi kuwapa hongera TCU na kama Ndalichako ndio kafanya haya basi basi asiitwe prof, tumwite Sir Ndalichako.

Najua haitochukua muda mrefu kuna wanasiasa fulani watapanua midomo yao na kuipinga TCU kwamba haitaki Vijana wasome wakati hao hao ndio wanaolalamikia elimu ya Tz kwamba haina ubora na imeshuka thamani.
Nawasubiria wanasiasa, wataalamu wa elimu nk watakao washutumu TCU au watakaowapinga TCU ili nile nao sahani moja maana mmezidi unafiki.

Elimu sio kampeni wala bungeni mahala ambapo kila mmoja anasema anachojiskia. Elimu ni moyo wa Taifa inahitaji watu wenye ufaulu bora ilia tupate wataalam sahihi.

TCU asanteni sana wasio na vigezo ndio wanaoshangaa madaraja mlioweka vipanga hawana shida.

# WASOMI WA TZ NI WANAFIKI TU. UKILETA HIKI WANATAKA KILE UKILETA KILE WANATAKA HIKI.
 
Afixa0

Point nzur sana za mara hii wenye vigezo ndo wanaenda chuo tungekuwa mbal sana kielimu na kiuchumi mamilion yamepotea kuwasomesha watu hawana cfa za kutosha mwisho wa cku wanadisco na wanaograduate ajira mgogoro pesa walizokopeshwa zinakua zimeenda bure bt this year salute to all undergraduate students 2016/2017
 
Umemaliza kila kitu nilichotaka kusema. Kwa hili naipongeza sana serikali, ilikuwa ikipoteza pesa nyingi kuwasomesha wanafunzi wenye ufaulu hafifu kwenye vyuo uchwara. Hizo pesa si bora zingepelekwa kwenye huduma za msingi kama maji na umeme ambapo kila mwananchi anakuwa anafaidika.
 
Naomba kujua walau Elimu yako
 
Deploma ya education hakuna mwenye GPA ya 3.5 so sidhani wamekusudia nn haisee!!
 
Good grades don't mean a good education.
MANENO YA WALIOFELI NA WANAOJIPA MOYO.....HUO NDO UKWELI KUFAULU VIZURI NA KUWEKA GRADE NZURI NDIO MFUMO WA DUNIA,,,WE NENDA KATAFUTE CHUO CHAKO UKASOME UFELI ILI UJE UMUHIMU WA GRADE NA ELIMU
 
MANENO YA WALIOFELI NA WANAOJIPA MOYO.....HUO NDO UKWELI KUFAULU VIZURI NA KUWEKA GRADE NZURI NDIO MFUMO WA DUNIA,,,WE NENDA KATAFUTE CHUO CHAKO UKASOME UFELI ILI UJE UMUHIMU WA GRADE NA ELIMU

Wewe mwenye akili nyingi hata kuandika hujui.
 
Sio kweli hiv mbona wenzeti wapo mbali kielimu na hawabani ni hivo sema bac tu but east Africa tutabaki kuwa na watu wachache wenye degree coz kumbe Kenya wamerahisisha kinyama mitaala
 
Back
Top Bottom