Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 255
Siku hizi ni kitu cha kawaida kabisa kukuta vijana wakipita mitaani kutangaza huduma za ttcl broadband na mobile wengine wako na zantel na kampuni zingine zinazotoa huduma ya internet vijana hawa hawajaajiriwa na ttcl wala kampuni hizo na hata hizo kampuni haziwatambui sema wanatambulika na wajanja wachache waliokuwa ndani ya kampuni hizo .
Kama una internet café , ukiongea nao wanakupa aina ya account unazotaka wengine wana mpaka za bure ambazo unaweza kutumia kudownload mambo yako usiku ukimaliza tu basi unaendelea na mambo yako mengine lakini hizo ni bure unaweza kutumia jinsi unavyotaka na kujisikia bila tatizo lolote .
Kuna wale wenzangu na mimi nao wana ttcl broadband na mobile , haswa wa mobile wengi wao wameanza kuikimbia ttcl sasa nakuhamia haswa zantel , kule gharama ni nafuu na internet wana uhakika wa kuipata muda wanaotaka na spidi nzuri sema tu huduma kwa wateja yao ndio hairidhishi wanachoka mapema .
Hawa wenzangu na mimi siku za karibuni simu zao zilikuwa blocked wasiweze kuhamia kwingine kama zantel na kadhalika , wale vijana wanauwezo wa kuflash hizo simu na kukuwezesha wewe kuhamia zantel kwa gharama nafuu sijui kama huu ndio ushindani wa kibiashara au vipi .
Hata na mimi nimekuwa nasumbuka sana na ttcl broadband ukiweka pesa baada ya siku kadhaa zimeisha nikiangalia vitu ninavyofanya kupokea na kutuma naona mahesabu hayako sawa , juzi hapa nikaamua kuongeza salio kwa pesa nyingine asubuhi ya leo imeshaisha kuuliza naambiwa nimeweka kiasi kadhaa wakati sio kiasi kile nilichonunua na kuingiza mimi mwenyewe .
Leo asubuhi nikaamua kwenda pale ttcl tena kuomba niongezewe salio , nilipotoa pesa nikashangaa dada mmoja ananipa kadi aliyoitoa katika mfuko wake ( pochi ) mara ya mwisho huyu dada alitoa tena hivyo hivyo , nikamwomba aniingizie yeye mwenyewe katika account yangu .
Kurudi nyumbani mchana huu kuangalia salio liko kidogo sio kama nilivyonunua kuuliza tena TTCL naambiwa umenunua kiasi Fulani , nikamuuliza yule dada wanaouza hizo kadi ni wakina nani yule katika chumba cha pekee au wale wanaojaza account zetu nikaambiwa yule katika chumba pekee ndio anayeuza kadi .
Kumbe wale wengine waliokaa pale katika mzunguko wanauza vocha zao wenyewe na ambazo wakati mwingi sio sahihi na wanaachiwa siku zote waendelee kuuza hivyo hivyo sasa najiuliza zile camera zilizokuwa pale haziwezi kuona kinachoendelea mule ndani au wanalindana ?
Yaani watu hawana uchungu kabisa na hali watu hawa lazima wadhibitiwe wanaharibu sifa ya TTCL na watendaji wake kwa ujumla .
Wanataka tuwakimbie halafu waanze kulalamika TTCL mbovu haiwezi kujiendesha wakati wao ndio wanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuzamisha meli hii ya TTCL .