Wanaoitwa viongozi ni akina nani hawa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaoitwa viongozi ni akina nani hawa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tegelezeni, Aug 24, 2011.

 1. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naomba niwaambie jambo moja ambalo wengi mnajifanya kutolijua. Ni kwamba rais wa nchi na viongozi wa nchi ni binadamu kama tulivyo sisi, hawana tofauti yoyote, na wala hawastahili kuhofiwa eti kwa sababu ni viongozi. Hawa ni binadamu tu ambao bila sisi wananchi wasingeweza kushika nafasi hizo. Nina maanisha kwamba sisi ndio tuliowapa nafasi hizo za uongozi.

  Kuwaita waheshimiwa au watukufu ni ujinga wa karne nyingi sana nyuma. Mimi naamini kwamba kila binadamu ni mtukufu na mheshimiwa kwa ukamilifu wake na mtu kuwa kiongozi hakumuongezei ukamilifu hadi kustahili yeye kuwa mtukufu na mwingine kuwa lofa.

  Heshima hizi zote kuanzia urais, uwaziri, ubunge na nyingine ni binadamu wamezibuni na kwa makusudi wakaamua wawape binadamu wengine. Ukweli ni kwamba hawa wanaadamu waliopewa, hawana sifa hizi na wala sio zao. Nasema sio zao kwa sababu ni za wale waliowapa, kwa sababu leo au kesho wakiamua kuwapoka sifa hizo watabaki kuwa makabwela au malofa fulani mitaani.

  Imefika wakati ambapo tunapaswa kujua kwamba tunapoteza muda mwingi katika kuwasujudia binadamu wenzetu kwa sifa ambazo sisi ndio tuliozibuni na kuwapa. Hakuna kitu cha ajabu mtu kuwa rais, waziri au mbunge kwa sababu vyeo hivyo tumevibuni wenyewe na havina maana yoyote katika hali halisi.

  Tunapaswa kujali zaidi nini mtu anazalisha katika jukumu fulani tulilomkabidhi au alilokabidhiwa na watu wengine au alilojikabidhi mwenyewe. Kuna idadi kubwa ya viongozi katika nchi hii kama ilivyo katika nchi nyingine hapa duniani, lakini kila siku binadamu amezidi kufukarika na kujawa na hofu na mazonge.

  Hivi mpaka leo tumeshindwa kubaini kwamba, hapo ndio mwisho uwezo wao, kama wameshindwa kwa miaka 50, tunatarajia muujiza gani!
   
 2. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  hivi umeuliza swali au umetoa mwongozo?
   
Loading...