Mwinue Mwingine Anapokuwa Dhaifu

Mwinue Mwingine Anapokuwa Dhaifu

Sozo_

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2022
Posts
3,267
Reaction score
6,183
2 Wakorintho 13:9
Maana twafurahi, iwapo sisi tu dhaifu, nanyi mmekuwa hodari. Tena twaomba hili nalo, kutimilika kwenu.

Katika safari hii ya wokovu kwa wana wa Mungu, kuna wakati wapo wanakuwa dhaifu, na wengine wanakuwa imara au hodari.

Yule anayekuwa dhaifu anapaswa kuimarishwa na aliye imara, hii itakuwa nzuri zaidi kama yule aliye dhaifu atalifahamu hili, na yule aliye hodari atakuwa anajua sehemu yake.

Hatuwezi kuwa imara kila siku, kuna wakati unaweza kukutana na changamoto mbalimbali katika maisha yako ya wokovu, utahitaji aliye imara akutie moyo na kukuombea.

Kama binadamu hatuwezi kujua kila kitu, kuna maeneo ni dhaifu na wengine ni hodari au imara, yule aliye imara usione vibaya kumtumia kwenye eneo usiloliweza.

Tunaweza kufikiri tunaweza kufanya kila kitu peke yetu, huo ni uongo, tunapaswa kutumia viungo vingine vya Mungu kuwajibika katika maeneo ambayo kiungo kingine hakiwezi kufanya.

Tukijua hatuwezi kuwa hodari kila eneo, tutakuwa na wasaidizi watakaosimama kwenye maeneo ambayo sisi hatuwezi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom