Wanaoishi katika mapipa ya taka UK waongezeka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,814
34,195
160301074811_waste_2.jpg

Watu wanaoishi katika mapipa nchini Uingereza

Idadi ya watu wasio na makao na ambao sasa wanaishi katika mapipa ya taka inaendelea kuongezeka nchini Uingereza kulingana na kampuni kubwa ya kuzoa takataka nchini humo.

Lakini ni kwa nini hili linatokea?

''Katika barabara unatukanwa na hata kunyanyaswa.Usiku uliopita vijana wachache walikuwa wanatembea karibu yangu na mwengine akanipiga teke la uso.Lakini katika mapipa unaweza kujificha ili watu wasikuone.Kuna joto hakuna mtu anayejua ulipo,''George analezea kuhusu barabara ya Bristol.

Amekuwa bila makao tangu alipopoteza kazi yake ya uhandisi kabla ya krisimasi,na kumfanya kushindwa kulipa kodi ya nyumba.

160301074652_waste_512x288_bbc_nocredit.jpg

Wanaoishi mapipani Uingereza
George ni miongoni mwa idadi kubwa ya raia nchini Uingereza aliyepatikana akilala katika mapipa ya takata kulingana na kampuni hiyo ya kuzoa taka ya Biffa.

Mnamo mwaka 2014 kampuni hiyo iligundua watu 31 waliokuwa wakilala katika mapipa tofauti ya takataka.

Mwaka mmoja baadaye idadi hiyo iliongezeka na kufikia 93 na mwaka huu ambao unaisha mwezi Machi, idadi hiyo imefikia 175 kufikia sasa.

Chanzo:
BBC Swahili
 
Du! Bongo kuzuri,,hakuna sehemu nzuri kama nyumbani.Huyo Mzee kwenye hilo tanker Unaweza kuta aliuza nyumba yake ndo akaweza kusafiri kwenda uingereza.
Huyo Mzee ni Raia wa Uingereza majalal hana kazi huku nje ukiwa huna kazi mwenye nyumba anakufuza nyumba yake usipo lipa kodi ni kitu chakawaida ulaya kulala nje au kwenye nyumba mbovu njooni ulaya mujionee wenyewe ulaya kugumu kimaisha ikiwa huna kazi ya kufanya.
 
Chezeya uchovu wa kubeba box weye.acha nikalale kwenye pipa langu mie.
 
Huyo Mzee ni Raia wa Uingereza majalal hana kazi huku nje ukiwa huna kazi mwenye nyumba anakufuza nyumba yake usipo lipa kodi ni kitu chakawaida ulaya kulala nje au kwenye nyumba mbovu njooni ulaya mujionee wenyewe ulaya kugumu kimaisha ikiwa huna kazi ya kufanya.
Ila ni mweusi,,uraia wake Inawezekana aliuomba.Kama kuna nyumba mbovu si bora angeweka huko kambi!! Au labda ni chache au ameamua kukaa karibu na msosi.
 
Hata msemeje, ugumu wa maisha wa ulaya huwezi kufananisha na ushenzini Kama Tanzania.
Hao wanalala kwenye mapipa sawa, lakini wana serikali inayowapigania na kujipanga kila kukicha kuondoa hilo tatizo, huko hakuna ufisadi wala uonevu wa kijinga wa kubambikia watu kesi, ni haki bin haki.
Bado tu ulaya ni ulaya huwezi kufananisha na maisha ya kishenzi yasiyo na kichwa wala miguu Kama kwetu hapa nyambafu.
 
TUKOMAE HAPA HAPA KWETU TZ habari za ulaya waachie wengine huna mishe ulaya kwanini mishe zenyewe za kuunga unga
 
Dah...huyo engineer analala kwenye takataka nafikir nje ya box ndugu zetu ambao profesheni zao za kuunga wabeba box watakuwa wanalala kwenye kinyesi
 
Huyo jamaa ana nyumba Pall mall, Westminster chezea omba omba London na hapo anakula kodi tu cha ziada ni beer tu
 
Hata msemeje, ugumu wa maisha wa ulaya huwezi kufananisha na ushenzini Kama Tanzania.
Hao wanalala kwenye mapipa sawa, lakini wana serikali inayowapigania na kujipanga kila kukicha kuondoa hilo tatizo, huko hakuna ufisadi wala uonevu wa kijinga wa kubambikia watu kesi, ni haki bin haki.
Bado tu ulaya ni ulaya huwezi kufananisha na maisha ya kishenzi yasiyo na kichwa wala miguu Kama kwetu hapa nyambafu.

Mkuu nchi yetu pendwa hv unaiita ushenzini? Mkataa kwao mtumwa ujue!
 
Hiyo ni taarifa kwa wale ambao kila siku wanawaza kwenda nchi za watu kutafuta maisha.
 
Wao watu 175 tu wanashangaa, waje bongo wahesabu machokoraa wanaolala majararani ni zaidi ya laki tano.
 
Maisha yanafanana kila sehemu ingawa mazingira yanaweza tofautiana kwa kiasi kikubwa.

Hata Tanzania watu wengi wanalala nje
 
Hata msemeje, ugumu wa maisha wa ulaya huwezi kufananisha na ushenzini Kama Tanzania.
Hao wanalala kwenye mapipa sawa, lakini wana serikali inayowapigania na kujipanga kila kukicha kuondoa hilo tatizo, huko hakuna ufisadi wala uonevu wa kijinga wa kubambikia watu kesi, ni haki bin haki.
Bado tu ulaya ni ulaya huwezi kufananisha na maisha ya kishenzi yasiyo na kichwa wala miguu Kama kwetu hapa nyambafu.
Mkuu nafikiri unapata taarifa za kusimuliwa na watu kuhusu ulaya,sina hakika sana kama ulichokiandika unakiamini.
 
Back
Top Bottom