kiwatengu
Platinum Member
- Apr 6, 2012
- 19,489
- 18,372
- Thread starter
- #21
Mimi nadhani katika multiple choice yako jibu ni "B" yaani wabunge wa upinzani baaasi!! nitaishia hapo. Lakini ukitaka nifafanue zaidi ni kwamba Kabla hatujaingia kwenye Siasa za vyama vingi bunge letu lilikuwa halina mgongano wowote kila kitu kilikuwa kinapita kwa 100% na tulizoea kelele zozote bungeni zilikuwa ni za kupongezana na kugonga meza. Lakini baada ya kuingia Siasa za vyama vingi hasa kipindi hiki ambacho wamepatikana watu wanaozijua sheria na wajibu wao kama wabunge mfano watu kama Tundu Lisu, Mnyika, Machali na Mkosamali wamekuwa wakiisumbua sana Meza ya Spika.
Kutokana na Kiti cha Spika kutokuzoea hizi changamoto za kuhojiwa hojiwa hivyo kimeamua kutumia nguvu ili kukilinda chama tawala dhidi ya fedheha kwa wananchi inayopelekea wapinzani pia kupatwa na hasira kutokana na ukandamizaji huu hivyo kusababisha haya yanayotokea Bungeni kutokukiheshimu tena kiti cha Spika. Hebu chukulia mfano Hasira za Ndugai kumtoa nje Tundu Lisu kwasababu tu anasimama mara nyingi kuomba muongozo na kuitafsiri kama ni fujo je sheria zinasemaje kuhusu mtu kuomba mwongozo? zimeweka kikomo? Kwahiyo wanao lihalibu Bunge to me ni Wabunge wa Upinzani Watanzania hatukuzoea watu CRITICAL.
Mkuu wa kwa maelzo yako haya mazuri ni dhahiri sasa jibu ni A...na siyo B. kwa sababu hao ndiyo hawajazoea changamoto kama unavyosema..