mtumishiwaleo
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 1,545
- 1,778
(Ndugu zangu Watanzania,
Nawapeni tu taarifa ya kuwa kama kuna mtu ama watu ama kikundi cha watu iwe ni ndani ya Nchi ama kutoka nje ya Nchi kinachoweza kuwa na mawazo ama Dhamira ya kumhujumu Rais wetu na Kumkwamisha Rais wetu Mpendwa katika kulitumikia Taifa letu. Ni lazma wafahamu ya kuwa wanajisumbua tu na kamwe hawatafanikisha Dhamira yao ovu..
Watashindwa kwa sababu Rais Samia yupo hapo Alipo kwa mipango na kibali cha Mwenyezi Mungu. Katika Ulimwengu wa kiroho Mama Samia ni Rais Wa Taifa hili hata kabla hajazaliwa. Mama Samia ni Chaguo la Mungu hata kabla ya Ya 2021.
Hamjawahi kujiuliza ni kwanini wengine walitumia mapesa na mapesa kwa miaka mingi sana tokea kurejea kwa mfumo wa vyama vingi lakini hawajawahi kufanikiwa kuupata wala kukikaribia kiti cha Urais? Hamjawahi kujiuliza imekuwaje wengine pamoja na kutaka kuunua Urais ama kujijengea kambi na kuunda wafuasi wenye nguvu kuwaunga mkono lakini hawajawahi kuupata Uraisi?
Je ninyi siyo Mashuhuda wa namna baadhi ya watanzania wenzetu walijihakikishia Urais lakini wakaishia kuusikia Redioni?
Lakini angalieni Safari ya Mama yetu namna ilivyo ya Miujiza na yenye Thamani iliyochorwa na Mungu Mwenyewe. Angalieni njia alizopitia mpaka kuibukia kwenye Umakamu wa Rais 2015. Angalieni Safari yake tokea wakati wa Ubunge mpaka kubwa mwenyekiti Makamu mwenyekiti wa Bunge maalumu la Katiba. Angalieni namna alivyoibukia katika siasa na kuanza kukwea ngazi za uongozi kama Komandoo aliyetoka mafunzoni.
Hivi hamuoni Kuwa kuna mkono wa Mungu juu yake? Hivi hamuoni ni safari iliyopangwa na Mungu mwenyewe? Hivi hamuoni ya kuwa ni Chaguo la Mungu mwenyewe kuliongoza Taifa letu?
Sasa unafikiri unaweza mhujumu Mama huyu aliyepewa kibali na kuinuliwa Na Mungu? Mnafikiria kuna lolote linaloweza kupangwa sirini na likafanikiwa? Mnafikiria kuna mwanadamu anaweza kupindua mipango ya Mwenyezi Mungu? Mnafikiria kuna Siku Mungu atazidiwa uwezo na k wanadamu aliyowaumba yeye mwenyewe kwa mikono yake na kuwapa Pumzi yake?
Narudia kusema tena ya kuwa RAIS Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe. Kainuliwa kwa mkono wa Mungu. Yupo hapo kwa kibali cha Mwenyezi Mungu. Ataongoza Taifa letu mpaka Mwisho kwa uwezo wa Mungu Mwenyewe. Hakuna wa kumshusha wala Kumkwamisha. Hakuna baya litakalopangwa na mwanadamu sirini na likaweza kufanikiwa.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.View attachment 3535700
Isaya 48:22
[22]Hapana amani kwa wabaya, asema BWANA.
There is no peace, saith the LORD, unto the wicked.)Samia hawezi fanikiwa hata afanyeje,damu aliyoimwaga bure ya watanganyika itamtafuna tu.