Wanaochezesha promo ya vodacom wanatuibia wananchi wateja tunaoshindana

mjombajona

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
262
50
Mimi nimejiunga na shindano la PROMO linaloendeshwa na Vodacom kampuni ya simu za mkononi na ninazo point zaidi ya
milioni mbili.

Mwanzoni tulikuwa tunaenda nao vizuri lakini toka walipoongeza kinyemela kila sms ya swali gharama kuwa shs 300 badala ya 200 na wizi ukaanzia hapo hapo.

Utakuta mtu una jaza vocha za kutosha kujibu maswali sms hata 15, lakini ghafla ukijibu maswali kumi meseji haziendi tena yaani ndo umeliwa vocha zako zimekwisha. Hasira hunipanda hasa kwa kuwa huwa sielewi query kama hii niipeleke wapi kwani huku mikoani hawa watu wana mawakala tu wasiojua chochote kuhusu hilo, labda makao makuu.

Msaada wana JF namna ya submit query vodacom kwani nikipiga hata hiyo namba 100 huwa sifanikiwi kuwapata baada ya pale wanaposema kwa tatizo fulani bonyeza namba fulani.
 
Ninachoona hapa unaomba msaada jinsi ya kuibiwa na mtoa msaada mkubwa jinsi ya kuibiwa ni Vodacom wenyewe.
 
Mimi nimejiunga na shindano la PROMO linaloendeshwa na Vodacom kampuni ya simu za mkononi na ninazo point zaidi ya
milioni mbili.

Mwanzoni tulikuwa tunaenda nao vizuri lakini toka walipoongeza kinyemela kila sms ya swali gharama kuwa shs 300 badala ya 200 na wizi ukaanzia hapo hapo.

Utakuta mtu una jaza vocha za kutosha kujibu maswali sms hata 15, lakini ghafla ukijibu maswali kumi meseji haziendi tena yaani ndo umeliwa vocha zako zimekwisha. Hasira hunipanda hasa kwa kuwa huwa sielewi query kama hii niipeleke wapi kwani huku mikoani hawa watu wana mawakala tu wasiojua chochote kuhusu hilo, labda makao makuu.

Msaada wana JF namna ya submit query vodacom kwani nikipiga hata hiyo namba 100 huwa sifanikiwi kuwapata baada ya pale wanaposema kwa tatizo fulani bonyeza namba fulani.

ukitaka kuwasiliana nao achana na number 100. Piga 15366 ila hakikisha una salio la angalau tsh 100.itapokelewa nara moja
 
Back
Top Bottom