TCRA naomba muangalie makato ya Vodacom na Tigo kwa wateja

Nukta5

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,180
1,276
Leo nimenunua salio nikaweka kwenye Vodacom nataka kujiunga kifurushi nikitakacho nashangaa naletewa sms kwamba salio langu halitoshi, nikapiga kuwauliza wananiambia nisubiri baada ya lisaa limoja nipige tena, kupiga wananiambia system yao inaonyesha kuna huduma nimejiunga nikawaeleza siijui hiyo huduma wala sijawahi kujiunga wala sitakaa nijiunge nayo wanasema system ndo inaonyesha hivyo so hapo inamaana ili niweze kujiunga tena inabidi niweke salio maana wanakata let say sh. 100 hapo ili kuifidia inamaana niweke sh. 500 na ikibaki sh.400 hakuna kifurushi cha 400 so wanaila bila huduma yoyote.
Nikaamua tena kununua vocha ya TIGO wakanikata tena kuuliza wananiambia nisubiri baada ya masaa 24 wajue kwa nin imekatwa sasa usumbufu wote wa kusubiria masaa 24 kwa nini TCRA msiingilie kati hii mitandao nafikiri inaingiza hela nyingi sana kwa kuumiza wateja pasipo TCRA kujua.
TCRA tafadhali naomba muwapige fine nyingine VODACOM na TIGO kwa kuwadhulumu wateja
 
hili swala lipo na ni njia ya upigaji... mimi huwa nawapigia na kuwa rekodi kuwa hizi huduma sijiungi na simu natumia mimi sichangii na mtu... nime wapigia kama mara tatu na kuwarekodi na kuwa fahamisha kuwa mna niibia... na kiswahili ni hiko hiko kama ulivyo eleza hapo juu et system ndio ina onesha...

sasa ita fika mahara tutaenda kwenye sheria kama wakina AY na FA... maana wana tukosesha madili ya pesa kwa ujinga wao...

na tuna andaa ushahidi ili tukienda kudai wakose kwa kuchomokea...
 
Huwa najiuliza hiyo system kwanini haikoseagi kutuongezea salio.isipokuwa inakoseaga kutubambikia madeni tu.
 
Back
Top Bottom