Wanandoa wasisitizwa kupima ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanandoa wasisitizwa kupima ukimwi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rutashubanyuma, Feb 15, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Wanandoa wasisitizwa kupima ukimwi


  Na David John

  SERIKALI ya Marekani kupitia Shirika lake la Misaada (USAID) kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali nchini Engender Health kupitia mradi wa
  Champion wamezindua programu mpya kwa wanandoa kujenga tabia ya kupima UKIMWI na kupanga uzazi ili kujenga familia iliyo bora.

  Akizungumza Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa programu hiyo jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Bi. Blandina Nyoni alisema kuwa virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi ni moja ya matatizo makubwa kwa Tanzania na hii inatokana na kutokuwa na tabia ya kupima mara kwa mara na wanandoa kutokuwa na uaminifu katika mahusiano yao ndani ya nyumba.

  "Kupitia Valentine Day (Siku ya wapendanao) nawaasa Watanzania hasa wanandoa kukaa pamoja kupanga malengo yao na kuwa waaminifu katika ndoa na kujenga tabia ya kupima mara kwa mara na kushirikishana katika maamuzi mbalimbali ndani ya nyumba," alisema.

  Pia alisema katika utafiti uliofanywa kuhusiana na Ukimwi pamoja na malaria mwaka 2007 na 2008 ilionyesha asilimia 6.6 kwa wanawake walio katika ndoa wameathiriwa na tatizo wakati kwa wanaume ni asilimia 4.6.

  Mwakilishi kutoka Marekani, Bi. Jens Schules alisema nchi yake kwa kutambua jitihada za serikali ya Tanzania wanaunga mkono na kusaidia katika kupambana na Ukimwi pamoja na malaria kupitia mradi wa Champion, na kuwataka Watanzania kutumia siku ya wapendanao kukaa pamoja kupanga mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa pamoja na uzazi ili kujenga familia iliyo bora.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Ukweli usiopingika ni kuwa kabla wapenzi hawajaamua kuoana wengi utakuta walikuwa ni mafundi kwa kiguu kwa njia: Kumega au wamegaji wazuri...............................na wengineo magwiji wa kuwamegea wengineo........................hivyo wengi wetu bila ya kukusudia utakuta wapo kwenye mtandao wa VVU ..................................hivyo wazo hili limekuja wakati mwafaka..........................na kwa kuongezea tuhimize sheria ya wachumba kupimwa kupimwa kabla ya kufunga ndoa.........................
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Watu hawataona kwa mwendo huu
   
 4. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,668
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  Haya tunawashukuru kwa hamasa tutajitahidi ila hiyo mara kwa mara sijui ndio ngapi sasa...
   
Loading...