Wanandoa na ukimwi,kuchukua tahadhari ni muhimu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,842
2,000
ndoa.jpg
Pete ya ndoa ni sehemu kubwa katika ndoa


KWA UFUPI
Utafiti mpya juu ya maambukizi ya uganjwa huo umebaini kuwa, asilimia 47 ya watu walio katika mahusiano ya kimapenzi ambao mmoja anaishi na virusi vya Ukimwi, hawawaambukizi wenzi wao.

FWANANDOA wanashauriwa kupima maambukizi ya Ukimwi ili kuongeza tahadhari kwa kuwa bado kuna uwezekano mkubwa wa mmoja aliyeathirika kutomwambukiza mwenzake.

Utafiti mpya juu ya maambukizi ya uganjwa huo umebaini kuwa, asilimia 47 ya watu walio katika mahusiano ya kimapenzi ambao mmoja anaishi na virusi vya Ukimwi, hawawaambukizi wenzi wao.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na madaktari bingwa wa nchini Uingereza na kuchapishwa katika Jarida la Magonjwa ya Kuambukiza la Lancet, si lazima kila mwenye ukimwi amwambukize mwenzake, ila kuchukua tahadhari ni muhimu.

Utafiti huo uliofanyika katika nchi 14 ikiwemo Tanzania, kwa kuchukua sampuli za wenza 13,061 katika nchi 27, ulibaini kuwa asilimia 47 ya wanawake na wanaume wenye Ukimwi walioko kwenye mahusiano ya kudumu, walikuwa na wenza ambao hawana VVU.

Jarida hilo limeeleza kuwa zipo sababu za kibaolojia na kisayansi zinazofanya baadhi ya watu wasiwaambukize wenzao Ukimwi.

“Hii ni pamoja na aina ya seli za mwanadamu, virusi na iwapo mmoja anatumia dawa za kufubaza makali ya Ukimwi au la,” linaeleza Jarida hilo.

Utafiti huo unafafana na uliofanywa na Benki ya Dunia (WB), chini ya Dk Damien de Walque katika nchi tano za Afrika, zikiwemo Kenya na Tanzania ambao ulibaini kuwa, robo tatu ya wenzi wanaoishi na VVU, mmoja hakuwa na maambukizi hayo.

Novemba mwaka huu, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema kuwa, karibu nusu ya watu wanaoishi na VVU walio katika mahusiano wana wenza ambao hawana maambukizi.

Akizungumza tafiti hizo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwale alisema zipo sababu nyingi zinazofanya mwenzi mmoja akawa na maaambukizi na wengine hana.

“Baadhi ya sababu hizo ni aina ya virusi, vichocheo, upekee wa maumbile, idadi ya wadudu na tabia zao,” alisemna kuendelea;

“Pia muda ambao mwenye virusi ameishi na virusi hivyo, iwapo anatumia ARV, au hatumii na majeraha katika sehemu za siri.”

Daktari huyo alibainisha kuwa kuna virusi ambavyo vipo hai na vina kasi kubwa ya kuingia katika mwili wa mtu kwa haraka na vingine si vikali. Virusi hivyo hufa kabla havijaingia katika majimaji ya mwili wa binadamu, alisema.

“Tabia hizi za virusi ndizo zinazoweza kufanya mmoja kati ya wapenzi kuwa na maambukizi na mwingine asiwe navyo,” alisema.

Pia daktari huyo alibainisha kuwa, baadhi ya wanawake maumbile yao yana kiwango kikubwa cha alkali ambacho huviua virusi vya Ukimwi mara.

“Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa wapo watu wenye seli ambazo zinasababisha virusi visiingie katika miili yao, ingawa tafiti hizo hazijathibitishwa,”alisema Dk Shimwale

Hata hivyo, Dk Shimwale alisema tafiti za hakika zaidi zinaendelea kufanyika kujua sababu ya kuongezeka kwa wenza wa aina hiyo.

Dk Shimwale alishauri kuwa, wapenzi/wanandoa wapime afya zao kabla ya kuanza kufanya ngono na kila mara inapowapasa kufanya hivyo.

Tacaids yatahadharisha

Katika hatua nyingine vijana Tanzania wametahadharishwa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa vile ndilo kundi lililo kwenye hatari zaidi.

Tahadhari hiyo ilitolewa hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa Mwitikio wa Taifa wa Tume ya Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk Morris Lekule.

“Vijana wanatakiwa wajue kuwa, kuna adui anawanyemelea ambaye ni Ukimwi, hivyo wanapaswa kujihadhari,” alisema Lekule

Kwa upande wake Afisa uhusiano wa TACAIDS, Glory Mziray alisema takwimu za kasi ya maambukizi ya VVU kwa Tanzania zinatarajiwa kutolewa mapema Machi, 2013 na Mtakwimu Mkuu wa Taifa.

Alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa kasi ya maambukizi ni asilimia 5.7.
Wanandoa na ukimwi,kuchukua tahadhari ni muhimu - Kitaifa - mwananchi.co.tz 

Ubungo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
1,247
1,500
Jana nimesikia kiwango cha maambukizi mapya ya ukimwi kwa Dar es salaam kiko juu na ya pili kitaifa.Salaqmu kwa Mama Ngina
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
2,000
Msalimie Mama Ngina.

Upo Mzee mwenzangu......
Umeadimika sana mkuu, hata husomeki?
Huyo Babu DC Dark City, kanigeuka juzi kwenye mtanange wangu na akina lara 1 na Zinduna, kanishushua katika majibu yangu kuwa tangu niji commit kwa mama Ngina sijatamani vya nje..............

Babu mbaya sana yule, ametufanya wazee wote humu JF tuonekane mahayawani......................LOL
 
Last edited by a moderator:

Ubungo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
1,247
1,500
Pole sana ndugu yangu, niko mkuu. Naona umeishia na wakuda wengine....ila wewe haikuhusu.
 

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,292
2,000
Upo Mzee mwenzangu......
Umeadimika sana mkuu, hata husomeki?
Huyo Babu DC Dark City, kanigeuka juzi kwenye mtanange wangu na akina lara 1 na Zinduna, kanishushua katika majibu yangu kuwa tangu niji commit kwa mama Ngina sijatamani vya nje..............

Babu mbaya sana yule, ametufanya wazee wote humu JF tuonekane mahayawani......................LOL
kwani UONGOOOOOOOOOOO?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom