Wananchi wengi bado wanaitaka adhabu ya kifo` | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wengi bado wanaitaka adhabu ya kifo`

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, imesema wananchi wengi bado wanapendelea kuwepo kwa adhabu ya kifo kwa wanaothibitika kisheria kufanya kosa la mauaji.
  Kamishna wa Tume hiyo, George Mlawa, alisema hayo Ijumaa wakati akitoa mada juu ya haki za binadamu kwenye mjadala wa umma uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Tumaini (Iuco) cha Iringa.
  Mlawa aliwaambia wanajumuiya ya Chuo hicho kwamba maoni hayo ya wananchi nchini yamepatikana kufuatia Tume hiyo kuzunguka mikoa karibu yote ili kupata maoni yao juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa adhabu ya kifo inayokiuka haki ya msingi ya binadamu ya kuishi.
  Mlawa amesema wananchi wanadai kuwa endapo serikali inashindwa kunyonga watu wanaothibitika kufanya kosa la uuaji, basi waachiwe wao ili watoe adhabu hiyo. Hata hivyo, Mlawa amesema kuwa mjadala wa kuondoa au kutoondoa adhabu ya kifo unachukua muda mrefu kutokana na kuwepo pande mbili zinazopingana ambapo moja ikitaka adhabu hiyo ifutwe huku upande wa pili ukitaka adhabu hiyo iendelee.
  Mwanafunzi wa sheria mwaka wa kwanza, Adella Kimaro, alisema hukumu ya kifo inakiuka haki ya kuishi na ni ya kikatili na kwamba inapaswa kuondolewa. Naye Askofu we Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Odenburg Mdegella, alisema kuondolewa au kutoondelewa kwa adhabu ya kifo bado ni mjadala usio na majibu ya haraka kutokana na kuhusisha masuala ya dini.
  Mkuu we kitivo cha Sheria, IUCO, Renatus Mgongo, alisema mjadala huo umelenga kutoa taarifa juu ya mabadiliko yanayoendelea nchini hususani juu ya haki za binadamu na kuongeza uelewa juu ya shughuli za tume hiyo.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...