Wananchi wazuia msafara wa Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wazuia msafara wa Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hamuyu, Aug 20, 2012.

 1. H

  Hamuyu Senior Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Na Ashton Balaigwa

  20th August 2012  Wananchi wa kata ya Hembeti Jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, juzi walizua kizazaa baada kuzuia gari la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuendelea na safari wakimtaka ahutubie mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Hamad Yusuph.

  Mbowe, aliyekuwa akitoka mkoani Dodoma baada ya kumaliza vikao vya Bunge, kiwa anaelekea katika kata ya Mtibwa kwenye mwendelezo wa operesheni vuguvugu la mabadiliko( M4C), alipofika katika kata ya Hembeti, gafla wananchi walimsimamisha wakitaka naye awahutubie kabla ya kuondoka.

  Kitendo hicho kilimfanya mmoja wa makada waliokuwapo mkutanoni hapo, Arcado Ntagazwa, kumpa kipaza sauti ili asalimie umati huo.

  Akizungumza na wananchi hao baada ya kupewa kipaza sauti, Mbowe alisema dhamira ya Chadema kuwa mkoani Morogoro ni kuwaondoa katika wimbi la usingizi wa kuishabikia Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

  Alisema hivi sasa Serikali inayoongozwa na CCM imeshindwa kutatua matatizo ya msingi ya nchi na kusababisha wananchi kuendelea kuishi katika hali ya umaskini wakati nchi imebarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa na rasilimali nyingi.

  "Tunakwenda kila kata ya mkoa wa Morogoro kujenga mtandao wa chama bila kujali dini, kabila wala rangi. Ujumbe wangu kwa wana-Hembeti ni kujua wajibu wa chama cha siasa ni kupata viongozi na sera mbadala zitakazowezesha nchi kusonga mbele," alisema Mbowe.

  Alieleza kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kuwaondolea wananchi matatizo mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa huduma za afya, maji pamoja kuboresha hali ya kilimo ili kuwapeleka katika neema katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru huku akiwataka wakazi wa Hembeti kujitafakari kwa kina chama hicho kimewafikisha wapi.

  Alisema mkoa wa Morogoro umefunga ndoa na CCM, hali inayowafanya wasiwe na sauti ya moja kwa moja huku matatizo yao yakiongelewe na wabunge wa vyama vya upinzani kutoka maeneo mengine.

  "Ninyi mmefunga ndoa isiyo na faida na CCM kwani mna matatizo mengi sana ikiwemo ya kilimo, lakini waliowaoa hawawasemei kule bungeni badala yake wabunge wa Chadema kutoka sehemu nyingine, ndiyo wanawasemea. Sasa tumekuja kuwaunganisha na wengine katika kuikomboa Tanzania," alisema Mbowe.

  Alisema ni makosa makubwa kwa wananchi kufikiria kuwa CCM ndiyo baba yao au mama yao na kuwataka wainyime kura katika uchaguzi mbalimbali na kuiweka Chadema na kwamba kama Chadema kitashindwa kusimamia maslahi ya wananchi, nacho kiwekwe pembeni.

  "Hata mimi Mbowe kesho nikiona Chadema haiendani na mahitaji ya wananchi katika kuwaondoa kwenye umaskini, sitakuwa na sababu ya kuendelea kuwa mwana-Chadema, nitatoka, ninyi mnang'anga'nia CCM, kwani ni baba yenu au mama yenu?," Alihoji Mbowe huku akishangiliwa na wananchi hao.

  Kwa upande wake, Ntagazwa aliyewahi kushika nafasi nyingi serikalini, alisema yeye ni mfano tosha kwa wananchi hao baada kutoka CCM kutokana na sera mbaya za kushindwa kuwasaidia wananchi na kuamua kujiunga na Chadema.

  "Mimi nilishakuwa Naibu Waziri wa Fedha na Waziri wa Mazingira katika Serikali ya CCM, lakini nimeamua kutoka na kuingia Chadema baada ya kuona hakuna mikakati ya kusaidia wananchi hasa ninyi wa vijijini. Hivyo mnangoja nini, jiungeni na Chadema tuing'oe CCM madarakani," alisema Ntagazwa.

  Awali, akiwa katika vijiji vya Kambala Hembeti na Mkindo kunakokaliwa na jamii ya wafugaji na wakulima, alisema migogoro ya ardhi nchi inakuzwa makusudi na watawala kwa kuwa wana maslahi nayo.

  Alisema watendaji na watawala wa Serikali ya CCM badala ya kuwakutanisha wakulima na wafugaji kuondoa tofauti zao, wao hutumia fursa hiyo kuchukua fedha kwa mmoja wao na kisha kuacha
  uhasama miongoni mwa wafugaji na wakulima.

  Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Hamad Yusuph, alisema sababu ya serikali kushindwa kutataua matatizo ya wakulima na wafugaji ipo siku nchi itaingia kwenye machafuko.

  Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, amejikuta akidondosha machozi mbele ya hadhara baada kuelezwa namna ambavyo wake na mabinti za wanaume wafugaji wanavyokamatwa kisha kupelekwa rumande na kutendewa vitendo vibaya ikiwa ni sehemu ya chanzo cha mapato.

  Dk. Slaa alitoa machozi hayo wakati akizungumza na wafugaji katika vijiji mbalimbali vya kata ya Msowero na Dumila wilaya ya Kilosa na Gairo ikiwa ni sehemu ya mikutano ya Operesheni Sangara-M4C inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Morogoro.

  Akiwa katika Kijiji cha Msowero, Dk. Slaa alidondosha machozi baada ya mfugaji mmoja kusimulia namna ambavyo wake na mabinti zao wanavyokamatwa kisha kupelekwa rumande na kufanyiwa vitendo vibaya, ambavyo alisema haviwezi kusimulika ili kuwa chambo kwa waume au baba zao watoe fedha kwa wakamataji hao.

  Alisema vitendo hivyo vinafanywa na baadhi ya askari wasiokuwa waaminifu, wakishirikiana na mgambo na viongozi wa serikali za vijiji katika maeneo mbalimbali ya wafugaji.

  Akizungumzia vitendo hivyo, Dk. Slaa alisema Serikali inastahili kubeba lawama zote kwa sababu imeamua kufumbia macho tatizo la wafugaji na wakulima kugombana.

  "Jana nikiwa Kilosa pale mjini, nilifuatwa na kiongozi mmoja wa wafugaji, na kunieleza vitendo hivyo vinavyofanywa na hao waliotajwa. Hii ni nchi gani sasa kama wafugaji nao wanakosa haki zao na kufanyiwa unyama?, Alihoji Dk. Slaa.

  Aidha, alitumia fursa hiyo kuwataka wafugaji kukiunga mkono Chadema ili kiwatetee na kuondokana na unyanyasaji huo.

  CHANZO:NIPASHE
   
 2. D

  DOMA JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mbele kwa mbele mpaka kieleweke
   
 3. N

  Ni Mimi Msiogope JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukombozi wa Kimbunga kisichokoma!..
  CHADEMA ni kama Moto ulao!
   
 4. C

  Concrete JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Safii,safi sanaaa!! Songa mbele hakuna kurudi nyuma. Wapelekeni mchakamchaka magamba mpaka wazimie.
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  safi sana..ukiona wananchi wa vijijini wanalilia mabadiliko ujue zama za ujinga zimeisha........
   
 6. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Zama za zidumu fikra za mwenyekiti'z no more..pamoja daima m4c
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  huyu mwandishi wa Nipashe ana lake jambo
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  itafahamika tu..
   
 9. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Jambo gani? Kuwa muwazi.
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Juzi ng'ombe wengi sana wamepigwa risasi mikumi serikali imekaa kimya mpaka leo!!!inatika uchungu sana!!Mfugaji hana lake tena nchi hii
   
 11. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Arcado Ntagazwa bado yupo?
   
 12. H

  Hamuyu Senior Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kamanda Arcado yupo na anaendelea vyema sana
   
 13. H

  Hamuyu Senior Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu hawa jamaa Magamba huku Vijijini hawana mpya mapokeo ya M4C ni makubwa sana, jamii ya wafugaji imebadilika sana na wana hasira sana yaani Mabadiliko Tanzania yanakuja,
   
 14. H

  Hamuyu Senior Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tuko pamoja makamanda baada ya mapumziko ya jana ya iddi, leo timu nzima ya M4c inajipanga ili kesho iingie porini kufyeka pori
   
 15. H

  Hamuyu Senior Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tuko pamoja Kamanda tuombeeni dua zenu dua zenu
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kuna watu watakufa kwa ugonjwa wa moyo kwa kasi hii ya chadema..
   
 17. H

  Hamuyu Senior Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  M4C imeshaeleweka, Vijijini kuna vitisho vingi sana kutoka kwa viongozi dhidi ya wananchi, hivyo usijali M4C kila inapopita inawapa ujasiri wananchi na kuhakikisha vitisho havipewi nafasi Tanzania
   
 18. M

  Molemo JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mpe heshima yake,jina lake linaanza na Kamanda....
   
 19. Micha

  Micha JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni kazi tu kwa kwenda mbele mpaka 2015.
   
 20. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mungu wa wanyonge yupo pamoja nasi,kila kheri makamanda wetu...
   
Loading...