Wananchi wapongeza trafiki wala rushwa kuonyeshwa kwenye televisheni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wapongeza trafiki wala rushwa kuonyeshwa kwenye televisheni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 5, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Date::10/4/2008
  Wananchi wapongeza trafiki wala rushwa kuonyeshwa kwenye televisheni
  Na Waandishi Wetu
  Mwananchi

  TAARIFA za kusimamishwa kazi kwa askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani 11 katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro walionaswa katika mikanda ya video wakipokea rushwa imezua hofu kwa askari wa kikosi hicho nchi nzima.

  Wakati Trafiki nchi nzima wakionekana kuingiwa na wasiwasi jinsi wenzao walivyonaswa na kamera hizo, wananchi mbalimbali wakiwamo wasafirishaji wa mizigo wamefurahia tukio hilo.

  Watu mbalimbali waliopiga simu chumba cha habari cha Mwananchi Jumapili jana kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Manyara,Tanga, Pwani, Morogorogo, Iringa na Mbeya walisema zoezi hilo lingefanyika nchi nzima.

  ''Wasingetoa kwanza hadi wakamilishe angalau mikoa 10, hata hivyo ni mwanzo mzuri na umeonyesha waandishi wanaweza wakiamua,'' alidai John Godson mkazi wa Dar es Salaam.

  Wakazi sita wa Wilaya za Hai, Moshi Mjini, Mwanga, Same na Rombo waliopiga simu kwa nyakati tofauti walienda mbali na kusema wamepata ujasiri na kwamba watatumia simu zao za mikononi kuwapiga picha trafiki wala rushwa.

  “Tulilalamika miezi kadhaa iliyopita lakini tukashangaa RPC (Kamanda wa Polisi) badala ya kuchunguza akatoa kauli ya kisiasa kwamba, hakuna jambo kama hilo ”alilalamika mmiliki mmoja wa mabasi ya abiria Mkoa wa Kilimanjaro.

  Mmiliki huyo wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya Rombo-Moshi na Arusha alisema kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ingekuwa makini haichukui dakika tano kuwanasa trafiki wa Kilimanjaro.

  “Leo wameonekana kama wamemwagiwa maji kile kiburi chao kimekwisha wanamuogopa kila mtu wanayemuona kwa kweli tunavishukuru vyombo vya habari hasa wapiga picha waliofanya kazi ile,”alisema.

  Wananchi wanaoishi Barabara Kuu za Tanga-Dar es Salaam, Dar es Salaam-Morogoro, Dar-Dodoma na Dar- Mbeya kupitia Iringa walitaka waandishi waliofanya kazi hiyo watunukiwe tuzo maalumu kwa uzalendo waliouonyesha.

  “Tumepita hapo Chalinze leo hatujasimamishwa wala ule utitiri wa trafiki kuanzia Kibaha hadi Mikumi haupo leo hii inaonyesha kuna jambo walilokuwa wanalifanya ndio maana wameogopa kiasi hicho,”alidai dereva mmoja.

  Kondakta wa mabasi ya kampuni moja maarufu inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma alisema kutoa Sh2,000 kwa trafiki ni jambo la kawaida iwe gari lina matatizo au halina.

  Mhudumu huyo wa mabasi alitoa wito kwa Jeshi la Polisi kubadili mfumo wa namna ya kuwapata askari wa usalama barabarani kwa sababu wengi ni watoto wa wakubwa na baadhi yao walitoa rushwa kupata nafasi hizo.

  ''Lazima Jeshi la polisi litazame upya mfumo wa Idara zake ili polisi wa kikosi cha kuzuia Rushwa asimuonee gere yule wa Trafiki kwamba ana maslahi zaidi…na dawa ni kuondoa tu rushwa na upendeleo wa ajira'' alisema.

  Wananchi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania walitoa changamoto kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa trafiki, James Kombe kukifanyia mabadiliko makubwa kikosi hicho.
   
 2. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Ina maana hata vijisimu vyetu tunaruhusiwa kuwamuvisha na kuwaanika TIVIINI.

  Heu tufafanuliwe ni nani atawamuvisha hawa "mapisadi" yaani polisi fisadi rodini!
   
 3. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hapo Chalinze leo hatujasimamishwa wala ule utitiri wa trafiki kuanzia Kibaha hadi Mikumi haupo leo hii inaonyesha kuna jambo walilokuwa wanalifanya ndio maana wameogopa kiasi hicho,"alidai dereva mmoja


  Jumamosi tarehe 4/10/2008 tulisafiri kutoka Moshi kwenda Arusha na hatukukuta hata traffic police mmoja njia nzima. Tofauti na siku nyingine ma-traffic police hujazana kuanzia Maili Sita Moshimpaka Daraja la Nduruma upande wa Arusha. TAKUKURU itaifishwe, ITV/TBC hongereni kwa kazi nzuri.
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwakweli kwa hili hongereni vyombo vya habari kwa kuwaumbua, na hakikia hata waomba rushwa wote hasa katika public services kama vile hosipitali ofice za kulipia ushuru na kutoa vibali mbali mbali zikiwemo pasi za kusafiria hii ndo dawa yao! waanikwe tu tena kama siyo picha basi hata tuwarekodi sauti zao ikibidi nazo zirushwe hewani, naamini hapo waomba kitu kidogo watapungua!

  Ombi ni kwa wenye vyombo, tutakapo waletea hizo picha na sauti za waomba rushwa muwe tayali kutunza siri kwa watoa taarifa!
   
Loading...