Wananchi wamshauri Magufuli kuongoza vipindi vinne mfululizo

Status
Not open for further replies.
Huo ni uchochezi kutafuta mauaji ya kimbari....wewe unastahili ukamatwe na kufikishwa Polisi kwa mahojiano
 
Daaah!! Ee bana ee. Bora hii katiba kipengere cha uraisi kiwe free yaan kama anauwezo wa kuongoza maisha yake yote aachiwe na sio misimu miwili kama ilivyozoeleka.
 
Hatimaye maelfu ya wananchi wamezidi kupaza sauti wakimtaka Rais Magufuli kubadili katiba na kuweza kuongoza vipindi vingi zaidi kutokana na kasi yake ambayo imekuwa chachu ya matumaini na mabadiliko nchini.

Sema watoto wako siyo wananchi
 
Hebu muache ukichaa.....tunataka kama kweli magufuli anaipenda hii tz siyo kujiongezea muda....aweke mifumo ya ukweli.....yaan sheria ya kushulikia ufisad na mafisadi iwekwe ndani ya katiba.....hala aondoke hata likitawala jiwe itakuwa jamna shida.........
 
Hakuna hapo ya msingi ,kwanza ndio jana kamaliza uteuzi. Mngesubiri hata matokeo ya kazi za serikali yake basi !!

Nilichoona waTz ni nyani kama nyani wengine hawayaoni ya kwao bali ya wengine. Tunawashutumu kina Mseveni, Kagame, Nkurunzinza, Kabila etc kubadili katiba zao waendelee na huku sisi tukihimiza yafanyike hayo hayo kwa uongozi wetu. Tusemeje kama si unafki (SHAMEFUL)

Mkuu siyo watanzania woote labda sema hao manyumbu wa lumumba
 
Hatimaye maelfu ya wananchi wamezidi kupaza sauti wakimtaka Rais Magufuli kubadili katiba na kuweza kuongoza vipindi vingi zaidi kutokana na kasi yake ambayo imekuwa chachu ya matumaini na mabadiliko nchini.

Abadili katiba ili awe kama Museveni, Kagame, Nkuruzinza, Kabila na waovu wengine. Habari za Milembe.
 
JK alianza kwa kasi ipi? Mie siikumbuki. Ila haya ya Magufuli yatabaki kwenye memory za wananchi kwa miaka mingi ijayo

Kinacho nifurahisha mimi ni kwamba Lizaboni sasa tunaimba wimbo mmoja, heko magufuri kutufanya watamzamia wamoja.
 
Last edited by a moderator:
Hivi Magufuli amefanya nn mpaka sasa kinachoweza kumfanya mtu makini atamani magufuli abadili katiba kuongeza awamu???

Ni ujinga na unyumbu tu wa kufuata mkumbo na kutojitambua na hiyo yoote inasababishwa na mihemuko ya itikadi
 
Hatimaye maelfu ya wananchi wamezidi kupaza sauti wakimtaka Rais Magufuli kubadili katiba na kuweza kuongoza vipindi vingi zaidi kutokana na kasi yake ambayo imekuwa chachu ya matumaini na mabadiliko nchini.

Hayo mabadiliko umeyaona wapi wewe?
 
Magufuli ndiye kiongozi tuliyemsubiria kwa miaka mingi tangu uhuru, huyu anaweza kumzidi hata Nyerere kwasababu approach zake za kutatua changamoto ziko more pragmatic, he is not an ideology driven leader like Nyerere. Huwapati viongozi wa namna hii kila wakati,wanapatikana mara moja kila baada ya miaka 100,nasema ndio aongezewe miaka zaidi ya kuiongoza hii nchi ili aiweke ktk sehemu nzuri kimaendeleo.Miaka 10 haitoshi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom