Wananchi wamshauri Magufuli kuongoza vipindi vinne mfululizo

Status
Not open for further replies.

Josorobert

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
629
215
Hatimaye maelfu ya wananchi wamezidi kupaza sauti wakimtaka Rais Magufuli kubadili katiba na kuweza kuongoza vipindi vingi zaidi kutokana na kasi yake ambayo imekuwa chachu ya matumaini na mabadiliko nchini.

Nimetizama clips moja ya wanakwaya wakiimba mbele ya mh rais Magufuli. ile clips kwangu imenitia moyo sana hata nimesahau ela ya marekani aliyotunyima..ule uzalendo na feeling anazoonyesha Magufuli ni kielelezo tosha kwamba tuna Rais wa Watanzania wote na si rais wa wachache!

Nimejifunza mambo makuu yafuatayo.

Rais Magufuli anapenda sana watu wake

Rais ana uzalendo mkubwa kuliko chochote kile.. amegundua kosa letu kubwa tunalolifanya nikuacha uzalendo tulioachiawa na Mwl.

Magufuli yuko kwa ajili ya watanzania. hotuba yake pale Chato ina mambo makubwa ambayo rais mjanjamjanja asingeyasema... magufuli hana miezi minne ikulu lakini furaha tuliyonayo utanzani tumekuwa nae baada ya Nyerere.. hakika makubwa na mazuri yanakuja..

Tunakoelekea mim naona/nadhani ni bora tubadirishe katika Magufuli awe Rais wa kudumu. Kwani nin bwana!
 
Ujinga huo ndio hatuutaki, tunawacheka nini Rwanda na sisi tunataka kufanya nini? Naamini Tz tuna kina magufuli wengi sana, muhimu kuondoa kikazi chote cha nyerere nchi itakaa sawa tu
Huyu rais jaman yupo vizur sana
 
Hatimaye maelfu ya wananchi wamezidi kupaza sauti wakimtaka Rais Magufuli kubadili katiba na kuweza kuongoza vipindi vingi zaidi kutokana na kasi yake ambayo imekuwa chachu ya matumaini na mabadiliko nchini.

Mh Magufuli usikubali, huu ni ulaghai. Hata Obama anapendwa sana USA BUT ANASTAAFU.
 
Atakuwa ni chaguo la Mungu huyu au sio? Pengine ni malaika kashuka au sio? Mwezi mmoja ambao umeleta mimba na mtoto hajazaliwa tayari mnanunua nguo za mtoto? Bado hata serikali yake haijaingia Bungeni kueleza na kujibu hoja watu wamepagawa? Kweli Tanzania na watu wake kama ndivyo walivyo basi inastahili kuingia kwenye Guinness book of record kama nchi ya majuha.
Nimesema hayo kwani JF inajinadi kama Home of Great thinkers, kwa hiyo mtoa hoja ndio GT wa nchi hii.
 
akiendelea na kasi hii maendeleo yakaonekana, watoto wetu wakasoma bure, uchumi ukakua, uzalishaji ukaongezeka, viwanda vikastawi watoto wetu wakaondokana na tatizo la ajira --- jamani kwani tunataka nini?? hata akitaka kuachia tutamlazimisha abaki aendelee kutumbua majipuuu
 
Ujinga huo ndio hatuutaki, tunawacheka nini Rwanda na sisi tunataka kufanya nini? Naamini Tz tuna kina magufuli wengi sana, muhimu kuondoa kikazi chote cha nyerere nchi itakaa sawa tu

Wewe ni mmoja wapo ya Watz wache wenye IQ kubwa na mambo kama hayo aliyo yasema mtoa mada yapo Afrika pekee kwa wenye akili huwezi yaona
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom