Corticopontine
JF-Expert Member
- Sep 20, 2019
- 664
- 1,272
Nimemuelewa Nape Moses Nnauye.
Nilivyomuelewa mimi silazimishi mwingine kumuelewa. Kila mtu abaki na uelewa wake.
Katika clip inayotembea mitandaoni, NAPE NNAUYE amenukuliwa akisema yafuatayo.
"Kama kuna watu wamefurahi, mimi mmojawapo, bahari imetulia, Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi, basi baki nyumbani tusonge mbele pamoja"
"Membe oyeee, Samiaaa oyeeeeeeeee, wangapi wanampenda Samia, mbona mmechekaa...!!!? Nyoosha kidole juuu, message sent eeeee, Mama Samiaaa Oyeeeee"
Kwanza nianze na kauli yake ya kwanza kwamba Mwenyezi "Mungu ameamua ugomvi"
Hii kauli imeniuma sana, imeniuma mno, sikutarajia kuisikia kutoka kinywani mwa Nape Nnauye, kuna kauli za kutolewa na viongozi na kauli za kutolewa na mashabiki ama wafuasi fulani wasio na cheo chochote ama nafasi yoyote ile.
Kauli hii kwamba Mwenyezi mungu ameiamua kesi hii ni kusema kwamba Bernad Membe amereje CCM baada ya Hayati Dr Magufuli kufariki. Kwamba bila Magufuli kufariki ama kuondoka Madarakani basi Membe asingerejea CCM.
Kiini cha haya yote ni nini? Membe aliondokaje CCM? Makosa aliyoondoka nayo Membe si ndo makosa hayohayo yeye Nape Nnauye alienda Ikulu kuomba msamaha kwa Magufuli? Hatujasahau mbona? Kuna nini kinaendelea kwenye hili la leo?
Baada ya kauli hii kuitoa Bwana Nape Nnauye, akawataka wananchi na wanachama wa CCM wanyooshe mikono juu kama ishara ya kumkubali Rais wa sasa Mama Samia, hilo wananchi waliligomea, ndo maana akasema mbona mnasita hivi, maana yake wananchi na wanachama wa CCM hawakukubaliana na hizi kauli tata anamchonganisha Mheshimiwa Rais ionekane kifo cha Magufuli kinafurahiwa na Mama Samia jambo ambalo ni hatari na halina afya kwenye chama na Serikali. Hili binafsi nalikemea.
Najua Nape Nnauye ana madaraka, ni kiongozi mkubwa serikalini ila siogopi na wala simuogopi na akitaka lolote anifanyie tu potelea mbali ila jambo alilolifanya ni la kulaaniwa na mtu yeyote. Jambo lisilokuwa na utu ndani yake. Hapo kwenye hizi kauli zake Mama Samia amehusikaje? Kwamba nini?
Kauli hii ni ya hovyo na siwezi kukubaliana nayo japo watu na viongozi wa chama wameikalia kimya. Nape atambue kuwa kauli zake anazozitoa ndizo zinazoifanya serikali hii inayoongozwa na Mama Samia isipendwe na wananchi. Ni kwa sababu ya kauli hizi, inawezekana Nape Nnauye alikuwa na ugomvi na Magufuli, hilo sisi wananchi halituhusu, kila siku akisimama ni kumsema Hayati Magufuli namna anavyojua yeye siwezi kukubaliana nalo.
Mimi ni kiongozi wa chama, kiongozi wa Chama chetu anaongozwa na kanuni za maadili za viongozi. Nitashangaa kama hatoitwa na kamati ya maadili ya chama. Furaha yake yeye Magufuli kufariki hakutufanyi sisi wengine pia tufurahie kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wetu taifa. Maamuzi ya kufukuzwa uanachama wa cCM kwa Benard Membe haukufanywa na Magufuli peke yake. Walikuwepo viongozi wengine.
Ni kawaida kwa CCM mwanachama akifanya makosa makubwa huwa anafukuzwa uanachama au kusimamishwa uongozi wake katika chama na hatua zingine za kinidhamu hufanyika ikiwepo kutumia haki ya kikatiba ya kusikilizwa kwenye kikao. Membe haya yote hakuyapitia?
Nape Nnauye ameelezea kwamba aliwahi kuingia katika hatihati ya kufukuzwa chama. Tukio hili nalikumbuka vizuri. Ilikuwa katika awamu ya nne na akatuhumiwa kwamba yeye na akina Membe walianzisha chama kipya. Ilikuwa enzi hizo za awamu ya nne. Magufuli hakuwa hata na ndoto ya kugombea Urais. Amekiri kwamba kulikuwa na wahuni kipindi hicho akiwa msaidizi wa Membe hadi Membe akaamua kusaini barua yake aende masomoni ili asiondolewe kwenye chama.
Wakati huo yeye akiwa Msaidizi wa MEMBE, Magufuli hakuwa hata Rais, Dr bashiru hakuwa Katibu Mkuu wa CCM, Humphrey Polepole hakuwa katibu mwenezi wa chama. Kauli hii inapingana na uhalisia wa matendo yake na mwenendo wake katika chama cha Mapinduzi. Nimeitimaza clip hii kwa muda kidogo na kuirudiarudia kuona alimaanisha nini, nilichokiona ni chuki binafsi dhidi Hayati Magufuli na wengine aliokuwa nao katika uongozi wa chama na serikali.
Naikemea kauli ya namna hii na kukiomba chama cha mapinduzi kitoe rai na onyo kwa mtu yeyote kuwasema viongozi wastaafu ama waliotangulia mbele za HAKI .