Wananchi wamkataa Mwenyekiti wa Kijiji. Wafunga ofisi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Wakazi wa kijiji cha Ngelenge kata ya Ruhuhu wilayani Ludewa mkoa wa Njombe,wamefunga ofisi ya kijiji pamoja na kumkataa mwenyekiti Thomas Mkinga kwa sababu ya kushindwa kusoma taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miaka miwili.

Tukio la kufungwa ofisi limetokea julai tatu majira ya saa tatu asubuhi katika kijiji cha Ngelenge.

Wakizungumza na Nipashe wa njia ya simu wananchi hao wamesema,wamechoshwa na uongozi wa mwenyekiti huyo ambaye wanadai anatumia madaraka vibaya kwa kuwa wamekuwa wakimuomba mara kwa mara aitishe mikutano lakini hatekelezi.

Casian Mahundi ni mkazi wa kijiji cha Ngelenge amesema kuwa wamekuwa wakimwambia asome mapato na matumizi lakini hatekelezi.
 
Back
Top Bottom