Katika juhudi za kuimarisha usalama, Umoja wa Umbwe Sinde Community umeandika historia mpya ya maendeleo ya kijamii kwa kuchukua hatua madhubuti za kuboresha usalama na huduma za afya kwa wakazi wa eneo hilo, baada ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Kibosho.
Umoja huo umefanikiwa kuanzisha kituo hicho, hatua inayolenga kupunguza vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyokuwa changamoto kubwa katika Kijiji cha Umbwe Sinde.
Akizungumza kwenye mkutano wa umoja huo jana Desemba 31, 2025, Mwenyekiti Sisti Massawe amesema umoja huo ulianza kama kikundi kidogo cha WhatsApp kabla ya kukua na kuwa jukwaa muhimu la maendeleo ya kijamii.
“Baada ya kufanikisha kuanzishwa kwa Kituo cha Polisi, ambacho kimegharimu takribani Shilingi Milioni 25 kwa kukodisha jengo, sasa tupo kwenye mchakato wa kuboresha Kituo cha Afya ili wakazi wapate huduma bora,” amesema Massawe.
Ameongeza kuwa umoja huo tayari umepata eneo la kudumu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi, hatua itakayosaidia kuimarisha usalama wa muda mrefu katika Umbwe Sinde.
Kwa upande wake, mmoja wa Wanachama wa umoja huo, Protus Mboya, amesema umoja huo umekuwa na mchango mkubwa katika maisha ya wanajamii.
“Kupitia umoja huu tumeweza kushirikiana katika misiba, magonjwa, na sasa katika miradi ya maendeleo. Ujenzi wa Kituo cha Polisi ni hatua muhimu kwa sababu eneo letu lilikuwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani,” amesema Mboya.
Wananchi wa Umbwe Sinde wanaeleza kuwa wanatumaini jitihada hizi zitaendelea kuleta mabadiliko chanya na kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii nyingine nchini.