Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Wananchi wa Kijiji cha Muze, Kata ya Muze, katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa, wamezuia msafara wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya hiyo wakilalamikia mchakato wa uteuzi wa majina ya wagombea wa udiwani katika kata hiyo.
Tukio hilo limetokea baada ya orodha ya awali ya wagombea watatu iliyotangazwa Julai 29 kubadilishwa ghafla asubuhi ya Julai 30, na jina la mgombea wa nne kuongezwa.
Wananchi wamedai kuwa mgombea huyo amekuwa diwani kwa kipindi cha miaka 15 bila kuleta maendeleo yoyote yanayoonekana katika kata hiyo.
Wamesema wame lazimika kuzuia msafara huu ili kupate majibu ya wazi juu ya mchakato huu wa uteuzi ambao unaonekana kutozingatia maslahi ya wananchi.