Wananchi wa Arumeru Mashariki kumsindikiza Nassari bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wa Arumeru Mashariki kumsindikiza Nassari bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AdvocateFi, Apr 2, 2012.

 1. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Habar wana Jf!
  Maelfu ya wananchi wa arumeru mashariki wanaanda utaratibu wa kuchanga fedha na kukodi malori ili waweze kumsindikiza mbunge wao bungeni aprli hii, uamuzi huo bado unaratibiwa na maelfu ya wakazi wa arumeru especially vijana wote na wananchi wengine wa kawaida, mchakato huu umetokana na wito ulotolewa na Mwenyekiti wa CDM taifa F. Mbowe ktk mkutano wa kuwashukuru wananchi wa arumeru ulofanyika leo jioni.
  my take
  kama mpango huu utafanikiwa basi itakuwa ni ishara na salam ya mabadiliko kwa CCM kuelekea 2015.
  CHADEMA 4 Life
  M4C
  solidarity forever.
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kila la kheri wana Arumeru chonde yawe mabasi na si maroli wasije magamba wakawatuma polisccm wakawazuia njiani na lengo lisifanikiwe
   
 3. M

  MWINUKA E Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika mkutano uliofanyika jioni ya tar 2/4/2012 walisema watakodi mabasi na si malori naomba mdau aweke kumbukumbu zake sawa.
   
 4. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  thanks mkuu! Ni mabasi.
  CHADEMA 4 critical changes
  M4C
  solidarity forever.
   
 5. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ...ilitaka kushangaza kukodi malori Arsh mpaka Dom? msingekuwa tofauti na magamba ambao wanawafananisha watanzania wao na nyanya toka Ilula zinazobebwa kwenye mafuso wakati wao wakitanua kwenye mav na mag X.
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hongera zao wanaArumeru!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hili siyo lazima kabisa; nguvu hii inaweza kutumika kwa namna bora zaidi badala ya kufurahisha hisia.
   
 8. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mie pia. Tunapoteza nguvu nyingi kwa mambo ambayo hayana tija. Wameshamchangua mbunge wao, basi waendelee kuchapa kazi. Hii kwenda hadi Dodoma kumsindikiza tu haina tija. Kote atakapopita hadi Dodoma kuna washabiki, waumini na wanachama kibao wa CDM ambao watamshangilia kwa sana.
   
 9. F

  Fowardever New Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono MM Mwanakijiji,vipi kama hiyo pesa ingeenda kuongeza idadi ya visima vya ndesamburo..VIVA CHADEMA..
   
 10. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Nawapongeza wana CDM wote kwa mambo matatu; 1. Kujitokeza kwa wingi wakati wa kampeni 2. Kujitokeza kupiga kura na kuchagua wagombea wa CDM, 3. Kuwa imara kulinda kura pasipo kujali vitisho. Si Arumeru Mashariki tu bali pia udiwani Songea, Rungwe na Mwanza.

  Baada ya uchaguzi kumalizika kumsindikiza mbunge ni jambo zuri ila lisiwe la kupoteza muda na gharama pasipo sababu wala tija. Waende wawakilishi wachache ambapo hakutakuwa na haja ya kudodi gari. Watumie magari au hcopter watumiayo viongozi wa CDM. Kurudi nyumbani watapanda mabasi.
   
 11. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Wazo zuri lakin wangelitumia kwa namna nyingine, badala ya kuchangia safari ya Dodoma wangeanza kuchangishana kwa ajili ya kutatua matatizo ya maji, madawati, madawa na vitanda mahospitalini.
   
 12. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hiyo inaweza kusababisha kitu fulani ku -'evolve' ambacho mimi binafsi nakitamani. Sijui kuna uhusianogani kati ya neno 'north' na 'revolution'. Hayo magari hata kama ni mawili yakionekana kwenye vyombo vya habari, watu nchi nzima watasisimkwa na damu then ccm may vanish b4 2015.
   
 13. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,934
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  ni kweli ila siyo malori keep in mind kwamba huku meru tumeendelea kwa hiyo tutakuja na usafiri mzuri
   
 14. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kumbuka ukifanya kazi ngumu kilichobaki ni kutuliza akili yako na akili haitulii tu kwakuilazimisha bali kwakitu ambacho roho yako itasuuzika let them spend hata kama hawana masalia ya jioni nafikiri wakirudi watajituma kwa moyo kwani kwenda kule itakuwa siyo tu kumuona Nassari akiapishwa bali watapata cangamoto nyingi za maisha. M4C
   
 15. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nafikiri tukubali matatizo yapo hata wakichanga na kupunguza lakini kumbuka kuwa inatakiwa kwa moyo mkunjufu. Naona bora wafanye moyo unavyowatuma kwasasa namaanisha waende Dodoma na hawa wakirudi wataleta chachu ya mabadiliko kwa Taifa. Naitamani Arusha kudadadeki
   
 16. d

  dada jane JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante mawazo mazuri ila ni muhimu kuzingatia ushauri wa MMM et al. Kuna member jana kanifurahisha kuwa anaenda kufanya kazi hadi bosi wake ashangae. Ndivyo tunavyotakiwa tufanye popote tulipo. Jamii inayonizunguka inashuhudia. I am a teacher iko siku nitashuhudia.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kudadadeki Huu ujinga! Hakuna sababu CDM Chama makini Huu utakuwa ujinga wa Magamba! Invest for 2015 Jenga shule! Madawati, madawa hosp visima maji etc kudadadeki

  M4C
   
 18. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sehemu kubwa ya watu wa Arusha imezoea kufanya utalii wa ndan na picnic hivyo sitashangaa kama swala hili litapata uungwaji mkono wa hali ya juu. Hata hivyo mpango huu unaweza kuionyesha Dunia kitu fulan, hasa mshikamano uliopo baina ya wananchi na viongozi wao waliowachagua wao, pamoja kutoa experience fulan ambayo itadumu kwenye mioyo ya washiriki (MM anasema kufurahisha hisia)

  Lakin bado najiuliza, kwan mkutano wa jana haukutosha? Kwan hatuwezi kufurahisha hisia kwa namna nyingine bila kupoteza muda na resources nyingi? Kwan hatuwezi kugeuza mshikamano huu katika namna ambayo itatuletea maendeleo ya kudumu zaidi? (mfano ujenzi wa zahanati kwa nguvu ya UMMA).

  Nadhan itakuwa ni suala la msingi kama viongozi wangetumia ushindi huu kuamsha ARI na Hamasa ktk mikoa mingine, na hivyo napendekeza jukumu la mapokezi ya Mh. J.N pamoja na kumsindikiza bungeni liratibiwe na CDM Mkoa wa Dodoma wakishirikiana na Makao makuu. Arumeru watoke wawakilishi wachache tu
   
 19. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  we si upo kamati kuu ya chama? kwa nini usishawishi viongozi wenzako humo ndani ya vikao wasifanye hivyo?. au hakuna platform mpaka utolee mawazo yako humu?. Impact ya maneno yako haya ni kubwa
   
 20. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hiyo pesa badala ya kunufaisha wenye magari ingetumika kuchimba visima kila kijiji na kujenga sekondari za bweni kila kata watoto wasome na kina mama wasisumbukie maji kama ilivyokuwa chini ya ccm. Karata ikichezwa vibaya bila focus itawagharimu cdm. Muda uliobakia kuelekea 2015 ni kidogo sana, mbunge mpya angeanza kusimika alama kila kijiji ili hata ccm wajue hawana chao huko tena. Akitapanya resource ya ukubaliko wake atakumbuka sana baadaye kwa uchungu. Akumbuke historia ya Mrema kusukumwa na umati wa watu kwenye gari lakini na amri ya siku saba mpaka kirarachi walimfuata huko na kuacha kitu kidogo, akasomwa tabia yake mbaya na akaandikiwa umarufuku kuwa rais milele hata haelewi mpaka sasa nini kilitokea. HUO NI USHAURI WA BURE KWA CDM Arumeru mashariki. Kuwa kimya lakini matendo yaseme sana, utaheshimiwa zaidi. mbwembwe zina madhara ya kudumu.
   
Loading...