Wananchi Monduli wamkataa mteule wa Lowassa, wadai waliichagua CHADEMA

uongo mwingine huu unauleta leo baada ya matokeo rasmi kutangazwa. kazi yenu kupandikiza vurugu kwa kuwakodisha watu wafanye vurugu na kufukuza wateule halafu mnasingizia aliyeshinda ni wa chadema..mlikuwa wapi siku zote au ndio umeamka usingizini?

Ninda kamlaumu mbunge wako alichokifanya ndio hukumu inaonekana sasa hivi
 
Hatimaye Taifa limeamka na elimu ya demokrasia inayosambazwa na Chadema imeenea nchi nzima.

Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ulipita wananchi wa Mto wa Mbu huko Monduli Arusha walipiga kura na kumchagua kwa wingi wa kura mgombea wa Chadema lakini katika hali ya kushangaza inadaiwa kwa maelekezo ya mbunge wa Jimbo hilo Edward Lowassa msimamizi wa uchaguzi alimtangaza mgombea wa CCM ndiye mshindi.

Leo kulikuwa na mkutano wa wakazi wa Mto wa Mbu kumtambulisha Mwenyekiti huyo wa CCM hata hivyo ilitokea vurugu kubwa sana na wananchi walimtimua Mwenyekiti huyo kama kibaka na kuapa kwamba hatowaongoza.

Mara baada ya kumtimua kama kibaka mteule huyo wa Lowassa umati huo ulimbeba juujuu mteule wao wa Chadema na kumpeleka kiti cha mbele.Kulikuwa na polisi wengi lakini waliogopa nguvu ya Umma.

Umati huo ulikuwa ukiimba Fukuza vibaka,Fukiza wezi.

Hii ni ishara njema kuelekea Ukombozi wa kweli oktoba mwaka huu.

Lowasa sasa ajifunze demokrasia Aache kuonea wapinzani wake na kuihujumu demokrasia maana asipojiandaa kisaikolojia na akafanikiwa kugombea urais japokuwa ni ngumu anaweza kuja kujikuta kifungoni kama Laurent Bagbo wa Ivory cost na hii itakuwa hatari sana.

Big up makamanda wa Monduli
 
Hii ni red light kwa ccm na mwaka huu hakuna kuibiwa kura kila kata maredbriged 200+ na mawakala ni makamanda walioiva kiukombozi hakuna kuhonga mtu hapo.

Wakitangaza aliyeshindwa pia hakuna kwenda mahakamani tena.
 
...red brigade 200 hawatoshi kulinda kura na vituo feki, tunawaomba usalama Wa taifa wenye mapenzi mema na nchi hii wafichue maasi ya mafisadi, kufanya hivyo haitakuwa uhaini Bali ni uzalendo kwa taifa sambamba na viapo vyao...
 
uongo mwingine huu unauleta leo baada ya matokeo rasmi kutangazwa. kazi yenu kupandikiza vurugu kwa kuwakodisha watu wafanye vurugu na kufukuza wateule halafu mnasingizia aliyeshinda ni wa chadema..mlikuwa wapi siku zote au ndio umeamka usingizini?
Kwani mkuu wewe hukuangalia taarifa ya saa mbili kamili ITV? Kwa hiyo unawaambia wananchi ni waongo? Hilooooooo jinga hilooooooooooo!!
 
Hao wahuni walioonyeshwa kwenye TV ni muendelezo wa Propaganda chafu za ITV na CHADEMA.
Kuna mambo ccm mjifunze,kazi kubwa ya viongozi ni kushawishi,kuweka malengo na kuyatekeleza,mto wa mbu ni sehemu tu ya eneo la jimbo la monduli lilivyotelekezwa.

Lowassa,kwa fedha anazomwaga makanisani na misikitini,zingetosha kujenga madarasa ya chekechea kila shule na kuweka umeme kwe'ye nyumba za walimu.

Halmashauri aliyoiacha Sokoine,imedumaa!,
 
Unafaihamu Halmashauri ya wilaya ya Monduli Kabla na baada ya Sokoine?

Au unaongea tu kujifurahisha?
 
Hao wahuni walioonyeshwa kwenye TV ni muendelezo wa Propaganda chafu za ITV na CHADEMA.

naomba ni kukumbushe wewe chooni kwa kitengo cha propar ganda kipo hapo lumumba tbccm tu,jiandae kisaikolojia kiufupi anza kutafuta kazi ya kufanya kabisa maana mkataba unaelekea mwisho.
 
Hivi hawa watu wa CCM huwa hawaoni aibu hata kidogo? Wewe watu hawakutaki na unajua hawajakuchagua kweli unaenda kukubali udhalilishwe hadharani namna ile nawe una familia yako ambayo ungependa ikuheshimu?
Kweli shetani akiingia moyoni mwako aibu kwako ni mwiko.
 
Back
Top Bottom