Wananchi kuchanga fedha kumaliza adha ya maji Njombe

Wananchi kuchanga fedha kumaliza adha ya maji Njombe

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Wakazi wa Kijiji cha Nindi, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, wamekubaliana kuchangishana fedha kiasi cha Shilingi Milioni 25 kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika kijiji hicho.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho, akiwemo Prosper Nkinga na Otilia Gowele, wamesema kuwa uamuzi huo umetokana na ukosefu mkubwa wa maji unaowakabili kwa muda mrefu.

Soma pia: Waziri wa Maji, Jumaa Aweso upo wapi kuzungumza ni lini huduma ya maji safi na salama itapatikana Jijini Dar-es-salaam?



Wameeleza kuwa pamoja na Wananchi kuchangia fedha hizo, wadau mbalimbali ikiwemo Serikali wameonesha utayari wa kuunga mkono juhudi hizo za Wananchi.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Olivanus Paul, amesema katika eneo hilo tayari kuna mradi wa maji unaofadhiliwa na Kanisa, hata hivyo mahitaji bado ni makubwa kutokana na idadi ya wananchi na uhitaji wa huduma hiyo.

Ameongeza kuwa amepokea ombi la wakazi hao na kuwataka kushirikiana kwa karibu na timu ya Serikali kupitia Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wakati utekelezaji wa mradi utakapoanza.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Joseph Kamonga, amesema ataunga mkono jitihada za wakazi wa Kijiji cha Nindi ili kuhakikisha wanapata huduma ya maji ya uhakika.

“Wenzetu wameibua mradi wa maji, nami ninawaunga mkono. Bunge tunaloanza Januari, nitaifikisha ajenda hiyo ili Kijiji cha Nindi kiweze kupatiwa mradi wa maji,” amesema Kamonga.
 
Back
Top Bottom