Wananchi kibaha wapongeza mfumo wa e-Ardhi

Wananchi kibaha wapongeza mfumo wa e-Ardhi

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
255
Reaction score
150
043e742e-af98-43dc-a340-edfff44b9c72.jpeg


Kibaha, Pwani

Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha wameipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuanzisha na kuendelea kutumia mfumo wa kielektroniki wa e-Ardhi, unaorahisisha upatikanaji wa hati miliki za ardhi kwa muda mfupi.

Kwa mara ya kwanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, mwananchi Mwira Abiud amekabidhiwa hati yake ya kielektroniki baada ya kufanya maombi kupitia mfumo wa e-Ardhi na kukamilisha mchakato huo ndani ya masaa 24.

Akikabidhi hati hiyo, Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Stella Tulio, amesema matumizi ya mfumo wa e-Ardhi ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha utoaji wa huduma za ardhi na kuwawezesha wananchi kupata hati miliki kwa urahisi na kwa muda mfupi.

" Mfumo huu unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za ardhi na kuhakikisha wananchi wanapata hati zao kwa urahisi na ndani ya muda mfupi,” amesema Bi. Stella.

Bi. Stella amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Pwani kutumia fursa ya Kliniki ya Ardhi inayoendelea katika Viwanja vya Stendi ya Zamani Mailimoja, Kibaha, kwa ajili ya kupata elimu, ushauri na huduma mbalimbali zinazohusu ardhi, ikiwemo huduma za hati za kielektroniki kupitia mfumo wa e-Ardhi.

Amesema Wizara imejipanga kutoa huduma kwa wananchi papo kwa papo kupitia timu ya wataalamu wa sekta ya ardhi, na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma hizo kwa wakati.

Kwa upande wake, Msajili Msaidizi wa Mkoa wa Pwani, Nw. Godfrey Mfalamagoha, ameeleza kuwa utoaji wa hati ya kielektroniki kwa mara ya kwanza katika Manispaa ya Kibaha unaonesha namna mfumo wa e-Ardhi unavyoweza kuongeza ufanisi na kuharakisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hati yake, Mwira Abiud ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha huduma za ardhi, akisema amefurahishwa na kasi ya upatikanaji wa hati yake.

" Nimefurahi sana kwa sababu nimepata hati yangu ndani ya masaa 24. Hii ni hatua nzuri na inarahisisha sana huduma za ardhi kwa wananchi,” amesema Mwira."

Kliniki ya Ardhi inaendelea katika Viwanja vya Stendi ya Zamani Mailimoja, Kibaha, Mkoa wa Pwani, ambapo wananchi wanaendelea kupata huduma, elimu na ushauri kuhusu masuala mbalimbali ya ardhi.
 
IMG_7112.jpeg

Habari chakii asante kwa kuwasiliana nasi. Huu hapa ni muongozo wa vitu muhimu unavyopaswa kuwa navyo ili uweze kuomba hati kupitia mfumo wa e-ardhi. Kumbuka, ili uweze kujisajili unapaswa kuwa na NIDA na namba ya simu. Kwa maelekezo zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu MLHHSD | Mwanzo
na upakue muongozo wa mtumiaji(user manual). Asante.
 
View attachment 3681803
Habari chakii asante kwa kuwasiliana nasi. Huu hapa ni muongozo wa vitu muhimu unavyopaswa kuwa navyo ili uweze kuomba hati kupitia mfumo wa e-ardhi. Kumbuka, ili uweze kujisajili unapaswa kuwa na NIDA na namba ya simu. Kwa maelekezo zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu MLHHSD | Mwanzo
na upakue muongozo wa mtumiaji(user manual). Asante.
Haya maombi ya e-Ardhi yanaweza kufanywa na mtu ambaye hajawahi kupata hati ya Wizara kabla?
 
Hongereni kwa hatua hiyo

Ila binafsi nina miaka 2 sasa sijafanikiwa kupata hati yangu ya kiwanja, tangu nilipoomba mwaka 2024

Mnataka tufe tuache mgogoro Viongozi??
 
Back
Top Bottom