Wananchi Bukombe waomba Rais Magufuli aongezewe muda wa kukaa madarakani

Hii nchi wapuuzi wengi sana.

Ndio maana watu wanagawana pesa na umma kwenye magunia wakati huko vijijini hakuna zahati, barabara mbovu, Shule hazina madarasa ya kutosha hadi wanafunzi wanasomea chini ya miti ujinga ujinga mwingi tu.




Wananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita,wameliomba Bunge la Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka kumi ya sasa hadi miaka ishirini ili kumuwezesha Rais Dk.John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani.

Wananchi hao wametoa ushauri huo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la bukombe mh. Dotto biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa namna alisimamia sekta ya madini,mkutano ambao umehudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh.Costantine Kanyasu.

Akiwahutubia wananchi,Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko,amesema kazi ya kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli si ya lelemama,huku Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh. Kanyasu akisema serikali ya awamu ya tano haiwachukii wawekezaji, bali inawachukia waporaji wa raslimali za nchi.

Ripoti ya kamati ya pili ya mchanga wa madini wa Makinikia,iliyowasilishwa Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof.Nehemiah Ossoro ilibaini taifa kupoteza shilingi Trilioni 252 kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia mwaka huu,huku ikiwahusisha baadhi ya mawaziri wa zamani wa nishati na madini waliohusika kuingia mikataba mibovu iliyoisababishia serikali hasara.
 
Back
Top Bottom