Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kagame styleTunajua hizo ndio chokochoko za madictator at a wakina kagame walianza ivi ivo na kusingizia wananchi nawaambieni watazania kuwa jpm ameanza kuandaa mpango yakubafili katiba aje kuongoza mpaka kifo
Wote huko ni wajinga wajinga hawajielewi wamekariri uwanja wa ndege chato na ununuzi wa ndege kienyeji kwa 10% za Bashite na GSMHao ndo kile kikosi cha TWAWEZA hawajui hata kuwa ndo ana miaka miwili madarakani.
Wote huko ni washamba na wajinga wajinga kwani walishangilia sanaNi watu wote wa bukombe au watu wawili watatu walio pata nafasi ya kukamata mic inakuaje mseme wananchi wa bukombe semeni watu wawili watatu ndio walisema ebbo!
Mkuu hayo Ni maoni tu Ni vile sie wazalendo na wananchi WA nchi hii tunavyoona magu inabidi aongezewe muda wa kuiongoza na kuivusha nchi hii. Suala la kusoma au kutokusoma halina mashiko katika hili. Chinese, they do not give a damn about democracy but she is the one of super power. Hata huko mnakocopy democracy wanalia daily eg.USA.Wore wanaodai kuongeza mda wa madaraka sijui ata kama waliitimu darasa LA saba
Sent from my HUAWEI Y336-U02 using JamiiForums mobile app
Wananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita,wameliomba Bunge la Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka kumi ya sasa hadi miaka ishirini ili kumuwezesha Rais Dk.John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani.
Akimaliza muda wake wamchague mbunge waoUpuuzi huo....
Geita ndo NYUMBANI,wenye mwana wanampigia CHAPUO MTOTO WAOWananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita,wameliomba Bunge la Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka kumi ya sasa hadi miaka ishirini ili kumuwezesha Rais Dk.John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani.
Wananchi hao wametoa ushauri huo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la bukombe mh. Dotto biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa namna alisimamia sekta ya madini,mkutano ambao umehudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh.Costantine Kanyasu.
Akiwahutubia wananchi,Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko,amesema kazi ya kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli si ya lelemama,huku Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh. Kanyasu akisema serikali ya awamu ya tano haiwachukii wawekezaji, bali inawachukia waporaji wa raslimali za nchi.
Ripoti ya kamati ya pili ya mchanga wa madini wa Makinikia,iliyowasilishwa Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof.Nehemiah Ossoro ilibaini taifa kupoteza shilingi Trilioni 252 kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia mwaka huu,huku ikiwahusisha baadhi ya mawaziri wa zamani wa nishati na madini waliohusika kuingia mikataba mibovu iliyoisababishia serikali hasara.
Wananchi wa kijiji. Teh teh teh
elimu yao sidhani km inafika darasa la 7.
Hawajui km kubadilisha katiba ni kosa? Watembelee Burundi wakaone. Wananchi km hawa ni mzigo kwa taifa. Ngozi nyeusi ni majanga sana. Mbona wenzetu huu ujinga haupo? Afrika tunasafari ndefu sana.
Shule zilijengwa za nn? Waache waandamane mpaka wachoke. Waende wakamuulize mwenyekiti wao wa mtaa na walimu wao watawapa jibu. Si lazima nifike huko kutoa elimu.Ujinga sio tusi, ila inafaa ujielimishe.
Jina lako lenyewe linakushtaki, hivi unasubiria ndani akasaidie jamii yako ijitambue.
Wewe wamekusomesha na ushamba wao huohuo badala ya kwenda kuwasaidia unawadharau.
Hujitambui
Kwa mtu mwwnye akili timamu na ni educated hawezi kufanya ujinga wa kuandamana ili kiongozi fulani aongezewe muda.tupe tathimini tu ya wananchi wenye elimu ya darasa la saba ni asilimia ngapi achana na hilo idadi ya wakaazi wanaojua kusoma na kuandika ni aslimia ngapi..basi