Wananchi Arusha wapanga foleni Bank ya CRDB kulipia sukari .

kama ni ukweli duh itarudi i enzi za sukari guru...hii kali

hahahahaha nimepita ubungo nkaziona leo.warudishe mambo ya maduka ya ushirika,ugali wa njano sisi tulikuwa tunaita ugali wa yanga,sukari ya duka la ushirika mnapanga foleni teheteheee,jamani
 
Mmmmmmmmmmmmmh tunarudi enzi za maduka ya kaya ****** ye hajui hayo yuko zake angani anaelekea Australia
 
hivi ni kwa watu wale watumiaji wa nyumba wanaohitaji kilo tano au 10 au ni kwa wale wakala wanaohitaji mifuko 1000 na kuendelea? mtoa mada hebu tujuze zaidi..maana sina sukati home nikapange fuleni ninunue hata kilo 2 wakuu
 
Mpwa, sorry are you serious?? Hapana mie siamini kama ni Tanzania hii na kwanini itokee Arusha?? wanamkomoa nani? Hata wawape na sumu hawataweza kugeuka nyuma tena na kuisujudia CCM
Unalipia bank unapewa kibali cha kwenda kuchukua kwa afisa mtendaji wa kijiji.kwahio unajiandikisha jina kwa mtendaji na mtendaji anaenda na list ya majina pamoja wahusika bank unasomwa jina unaenda kulipia dirishani ukishalipia unarudi na slep ya bank kwa mtendaji unamkuta wakala unamwonyesha karatasi ya bank unapewa sukari. Kwa karne hii haya mambo vip? jamani hii mpaka lini?
 
hivu ina maana hiyo nchi ya Kenya haina Sukari hadi ipelekewe kutoka Moshi na Arusha? fanyeni utafiti mtujuze ni kitu gani hasa kimeleta Uhaba wa Sukari Arusha na Moshi na siyo kusema eti kwa kuwa inavushwa kwenda Kenya. Mnafikiri hao majirani zetu wanafurahia tuhuma kama hizi? Mie nakumbuka enzi za MIEZI 18 YA SHIDA sukari tulikuwa tunaipata Kenya via panya ROUTE za huko msitu wa RONGAI.
 
Mpwa, sorry are you serious?? Hapana mie siamini kama ni Tanzania hii na kwanini itokee Arusha?? wanamkomoa nani? Hata wawape na sumu hawataweza kugeuka nyuma tena na kuisujudia CCM
Mkuu anachokisema Kipre ni cha ukweli na si Arusha Mjini tu mi nipo Maeneo ya Karatu toka jana tumekosa sukari na ni ya kupanga foleni tena si foleni ya watu wachache na kuna usimamizi wa askari ili watu wasilete vurugu........utaratibu uliowekwa na halmashauri sukari itatoka tu kwa wale wenye leseni za biashara na ni mfuko mmoja ndio unaopatiwa
 
TUMETHUBUTU TUMEWEZA NA TUNAZIDI KUSONGAMBELE! Miaka 50 ya shida ndani ya UHURU kulekuleee mambo ya zidumu fikra za mwenyekiti wa...?
 
Back
Top Bottom