Wananchi Arusha wapanga foleni Bank ya CRDB kulipia sukari .

Kipre tchetche

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
238
40
Unalipia bank unapewa kibali cha kwenda kuchukua kwa afisa mtendaji wa kijiji.kwahio unajiandikisha jina kwa mtendaji na mtendaji anaenda na list ya majina pamoja wahusika bank unasomwa jina unaenda kulipia dirishani ukishalipia unarudi na slep ya bank kwa mtendaji unamkuta wakala unamwonyesha karatasi ya bank unapewa sukari. Kwa karne hii haya mambo vip? jamani hii mpaka lini?
 
Sukari hiyo si chakula cha lazima katika mwili wa binadamu, Sukari yenye umuhimu ni ile itokanayo na vyakula mbalimbali tunavyokula kila siku. Hata hivyo mazoea ni magumu, wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kuweka sukari. Hata hivyo ukijizoesha kutotumia sukari, hakuna madhara yoyote mwilini. Nanukuu:

'The answer to this question depends on your definition of "sugar." If you mean table sugar, corn syrup and other sweeteners common in processed and refined foods, then the answer is no. But if you are using the word "sugar" to describe carbohydrates -- a broad group of foods that includes fruits, vegetables and whole grains -- then the answer is yes. To understand why that type of sugar is a necessary part of your diet, you must understand how the body functions.'
Read more: Is Sugar Necessary In The Diet? | LIVESTRONG.COM
 
inazalishwa TPC moshi lakini Arusha hakuna Sukari na wamechukua hekta nyingi mbaya lakini ukienda UK unaipata kirahiiiiiiiiisi.

Basi bado hujaelewa ni kwanini sukari haitoshi.
Kiwango cha wingi wa sukari inayozalishwa TPC ni ule ule. Ila sukari wenzenu wanaivunja nje ya nchi kwenda Kenya.
Hivo wanaongeza scarcity ya sukari, creating high demand while the supply is low, the price comes up, TPC hawana lawama zozote.
Sukari zinavunjwa kwenda kenya kwa kutumia noah,pickup,fuso za mchanga,na landcruisers za watalii zinaondolewa viti, sukari inalazwa,inapitishwa kule tarakea.
Nyie bakini mkilalamika tu.
Wenzenu wanatumia fursa iyo, wanavunja sukari kupeleka kenya ambako bei yake ni nzuri sana.
Tumia fursa kama hizi, ni MAGENDO. lakini ina faida nzuri. Ila ujue kwanza A to Z ya jinsi ya kupata mzigo na kuuvusha bila ya mbwa wa said mwema kukunusa.
Serikali ilishawasahau wananchi wa chini, inakumbatia wafanya biashara tu.
 
Unalipia bank unapewa kibali cha kwenda kuchukua kwa afisa mtendaji wa kijiji.kwahio unajiandikisha jina kwa mtendaji na mtendaji anaenda na list ya majina pamoja wahusika bank unasomwa jina unaenda kulipia dirishani ukishalipia unarudi na slep ya bank kwa mtendaji unamkuta wakala unamwonyesha karatasi ya bank unapewa sukari. Kwa karne hii haya mambo vip? jamani hii mpaka lini?

Huuuuh hiii kama siamini vile
 
Mkubwa mambo vipi????????????????????? Ina maana ukiitaji sukari ni mpaka ukalipie bank ya CRDB kwa wakazi wa Arusha?????????????? Ama ni kwa wakala wa kuhitaji sukari nyingi kama walivyo member kama Dalia Company,,,, na wengine kama haooo????????? Maana Mi naona kama ni raia wote basi hii itakuwa jipya tena hapa A town
 
Ndg Arusha one ..waliowengi ni wale wenye maduka ya bidhaa za chakula kwa rejareja wengine ni watumiaji wa direct .
 
Nilijua kabisa athari ya mgao wa umeme ungeleta upungufu mkubwa wa bidhaa muhimu zinazozalishwa humu nchini kama sukari. Sasa bado utasikia saruji n.k. Ngeleja na wenzake wanadunda na kamwe hawaathiriwi na upungufu huu. Hata kikwete analalamika kuhusu tatizo la umeme!! Je hii ni kweli?
 
Back
Top Bottom